Unasubiri nini kuwa mwana CCM?

Sijajua labda unipe darasa, natumia simu kuchart jamii forum, nashindwa kutag paragraphs kwenye texts ili nikujibu vizuri kama unavyofanya wewe. Lakini usijidanganye, viongozi CCM hawajashushwa toka kwenye mwezi, ni sisi wananchi haohao tunaovianzisha hivi vyama vya siasa. Sikulahumu kuwa CCM, lakini nipongeze mimi pia kuwa na chama chenye mlengo thabiti na msimamo imara wa kuwatumikia wananchi, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo "CHADEMA".
 
sawa muungwana mbussi mwanachama wa chadema, nadhani umeeleza vizuri sana na bilashaka kwa uzuri wa sera na mipango yenu Pascal Mayalla ataamua mwenyewe abaki au ajiunge nanyi kawasababu ni hiari kujiunga na chama chochote.

washaurini wanachama wenu wawe waungwana waache matusi. wa vyama vingine pia wajibu hoja kwa hoja.
 
Migogoro ya hifadhi na Wananchi imewashinda,wanatatua migogoro ipi au ya ndoa!
 
Kwanini tusiwape CHADEMA ili nao tuone ability and capability yao.Chama chenye capability hakiwezi kuwalinda viongozi Wala rushwa na wababaishaji wanaoingiza nchi kwenye mikataba ya ovyo.
 
Uongozi wa JF kama vile wanavuta weed wakiwa ofisini
 
Tlaatlaah, naomba uwe hakimu mzuri na uhukumu kwa haki. Chadema siku zote ni waungwana sana tena sana. Watukanaji wazuri ni CCM, waanzisha fujo ni CCM, uongo, propaganda chafu nk. ni CCM. Nikukumbushe tu, ni nani alianzisha propaganda kwamba Lowasa ni mgojwa atafia madarakani na wengine wakaanza kupiga push up, je, ni Chadema.? Ni nani utuma polisi kuwapiga mabomu kwenye mikutano yao ya adhara? Nichukue mfano wa juzijuzi; Chadema akiwa na mikutano halali wa adhara viwanja vya Furahisha Mwanza, CCM wakamleta Daimond apige bure mziki uwanja wa CCM Kirumba, mita mia toka kwenye mkutano. Hivi hapa mchokozi ni nani? Katika chaguzi vijana wa Chadema ukatwa na kubambikiwa kesi. Bado yote hayo uoni. Let's be realistic, ata kama si mwanachama wa hicho chama.

Nikuambie ukweli, CCM kwenye sanduku la kura bila kutumia hira, wizi na mabavu hawana chao. Kimebaki chama Cha watafuta vyeo na maslahi, si chama kinachowatumikia wananchi tena. Paskali amesema CCM ni ileile, jana, leo na kesho. Nampa big no!!
 
Ili uwe sehemu ya maendeleo ya nchi lazima uwe mwanaCCM? Sijajua umesema kwa utani au umedhamiria...hakuna mwanaccm yeyote anaependa maendeleo ya nchi hii.
Wanaccm wanataka maendeleo ya CCM kama Chama pamoja na maendeleo yao binafsi.
 
Last but not least, ndugu Mayalla, natatika kutag paragraph moja badala ya text yote ili ni kujibu, lakini nimeshidwa. Umesema hakuna chama chenye uwezo wa kuchukua madaraka nje ya CCM?? Big no my brother.

Katika kutafuta maisha nilibahatika kufanya kazi na mtu mmoja nje ya nchi, ambae kwa nafasi yangu tulikuwa tuki-interact mara kwa mara japokuwa yeye alikuwa boss mkubwa sana kutokana na jukumu alilokuwa amekabidhiwa kulisimamia. Sikujua kama huyo mtu angekuja kufanya aliyoyafanya.

CCM inakuwa madarakani kwa Sababu ya wizi wa kura, ubabe na mabavu ya vyombo vya dola. Lakini uwezi amini huyo mtu niliyemsimulia hapo juu nae alikuja kuwa mtu mkubwa aliyeaminiwa na serikali yake ambaye ndiye huyohuyo Jenerali Brice Oligui Nguema aliyeipindua Serikali ya Alli Bongo wa Gabon. Tumikieni watu, msitegemee kubaki madarakani kwa Sababu ya bunduki. Chama kizuri na kiongozi mzuri ni yule anaejenga Imani kwa watu, si yule anaetumia mabavu kuhalalisha utawala wake.

CCM kwa sasa ina sera zilibakia kwenye makaratasi. Kila Rais anaekuja anafanya anavyotaka yeye. Badala ya kujenga mifumo na taasisi imara, nyie mnasubiri fix za viongozi na matamko. Tuliona sarakasi na matamko ya kila aina kwenye hawamu iliyopita. Ni chama kinachoongoza nchi bila dira. Nikuulizeni maswali mafupi: Sera ya elimu ni hipi? Je, Afya, je huduma nyingine za jamii. Kifupi ni kwamba hakuna sera, kila awamu inajiendea inavyojua na mbwembwe kibao. Tuliona elimu bure, sawa shule zikajegwa sawa lakini shule nyingi za pembezoni wanafunzi elfu moja, walimu 10. Hivyohivyo kwenye mahospital nk. Hivi mnamkomoa nani?Tumeona watu wakipiga dawa za kuuwa mende kwenye maghoropha ya Kariakoo eti kuuwa wa COVID 19, walimu wakipigwa viboko na kuswekwa ndani na wengine kushwa vyeo baada ya wanafunzi kufeli badala ya kutafuta chanzo. Hiyo ndiyo CCM mnayojivunia, yaani akili zimewagota? hatuwezi tena kufikiri zaidi? Yule alifuta masomo ya kilimo na biashara, hatui atakaekuja atafuta yapi.....

Nikikuuliza tena sera ya CCM, je Tanzania ni nchi inayofuata mfumo upi wa uchumi. Je, ni ubepari au ujamaa. Nadhani mtajiuma na mpaka kesho jibu sitopata. Kuna tatizo kubwa Ila hamulioni. Mmtekwa na ghiriba za wanasiasa. Badilikeni acheni ushabiki na ubinafsi wa kutafuta teuzi. Watoto na wajukuu zetu watatulilia.
 
Rubbish
 
Watanzania wote ni sehemu ya maendeleo ya nchi na wala si kwa sababu ya CCM na asilimia 80 walishaachana na CCM siku nyingi ndio maana CCM imebaki na kete moja tu ya Wizi wa kura tu kwenye uchaguzi maana wanajua bila hivyo hawawezi kuongoza dola ,nje ya hapo ndani ya CCM hakuna kitu.Kama huamini maneno haya omba chama chako cha CCM na serikali yake kilete Tume huru ya Uchaguzi na katiba mpya kama kweli kina nia njema na watanzania,alafu baada ya hayo kufanyika Uje tujadili maendeleo ya Taifa hili.
 
Kama ni kikongwe huoni kuwa kitakuwa kimepitwa na wakati?
 
Umesahau sifa nyingi za ccm moja wapo bila kutoa rushwa jinalako linakatwa hata kama unagombea ubalozi wa nyumba kumi,lazima uwe na mtaji wa kitita cha hela ya rushwa kupitisha jina lako pia ccm bila kuwa,mwanga,mlozi na mshirikina utoboi
 
Ninazo hapa kadi yangu na za vijana wangu walinibwagia hapa, tena za ki electronic, anayezitaka aje nitampa
 
Taifa hili ni maskini hadi leo.. miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru kwa sababu ya hiki chama! ni huzuni kwakweli
 
Matarajio yapi mkuu ?
 
Bado unaendelea tu kung’ata na kupuliza kuhusu CCM?! Ukipata teuzi utakuwa kama Sabaya, kwa kweli wewe sio mtu mzuri ndani ya moyo wako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…