EMMANUEL ZACHA
Member
- Sep 6, 2021
- 24
- 111
Na Elivius Athanas.
0745937016.
Tatizo "connection" umekuwa ni wimbo ambao unaimbwa na vijana wapambanaji wa mtaani, wahitimu wa vyuo, wasanii na watu mbalimbali kuwa ni moja ya kikwazo kinachowachelewesha wao kupata kazi au kufanikisha jambo fulani.
Ni kweli kuwa "connection" ina mchango mkubwa kwa mtu kupata kazi au kufanikisha jambo fulani, lakini utafanyaje kama huna "connection"?
Utafanyaje kama huna ndugu wa kukuunganisha ili upate kazi?
Wakati kijana mpambanaji akiumiza kichwa ni jinsi gani atapata "connection" ili afanikishe kazi au 'mchongo' fulani, nikualike sasa kuzisoma mbinu tano (5) za kijanja na akili ambazo unaweza kuzitumia kujitengenezea na kupata "connection" ya kazi, pesa na 'michongo'.
Moja, tumia mitandao ya kijamii kutangaza ubunifu na bidhaa zako. Mitandao ya kijamii ukiitumia vizuri ni "connection" tosha ya wewe kupata kazi, pesa na 'michongo'.
Mfano, watu wengi wanaofanya vichekesho (comedy) mitandaoni, walianza kwa kuweka (kupost) vichekesho vyao mtandaoni, baada ya vichekesho vyao kufahamika na kukubalika, wakaanza kutafutwa na watu wa redio na runinga, wakaingia makubaliano ya kazi na wanapata pesa kwa ajili ya "connection" ya mitandao.
Wachekeshaji wengine kupitia kuweka vichekesho vyao mtandaoni, wamepata "connection" ya kufanya mahojiano kwenye vituo vikubwa vya redio na runinga. Kuna "connection" kubwa zaidi ya hiyo kwa msanii?
Mfano, Mc Mboneke (mzee wa irudiwe irudiwe) amepata "connection" kwenye vituo vingi vya redio na runinga baada ya kuwa anaweka video zake mtandaoni.
Siyo hao tu, wachekeshaji wengine baada ya kuweka video zao mtandaoni, wamefahamika na kupata kazi za kuwa Mabalozi wa Taasisi na Makampuni makubwa kwa ajili ya kuyatangaza.
Sio hao tu walioneemeka na "connection" ya mitandao, kuna wasanii wa kuiga sauti walioitumia mitandao ya kijamii vizuri kuiga sauti za viongozi mpaka wakapata "connection" ya kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Kuna watu walianza kuandika makala mtandaoni, kutokana na makala zao nzuri wakapata "connection" ya watu mbalimbali wakiwemo wamiliki wa magazeti, sasa ni waandishi wa makala magazetini.
Kuna wanamitindo wa kushona nguo za kisasa, walianza kujitangaza mitandaoni kwa kuonyesha ubunifu wao, wakapata "connection" ya kukutana na kuwashonea nguo watu maarufu na viongozi wa Serikali.
Mifano ipo mingi mno, nikiamua kuiandika yote nitajaza mnakasha (thread) hii kwa mifano ya "connection" za mitandaoni.
Uwe mwalimu, uwe injinia, uwe fundi ujenzi na kadhalika, ukitumia mitandao ya kijamii vizuri, ni "connection" tosha ya wewe kupata kazi.
Pili, jitolee kwanza na usitangulize pesa mbele. Linapokuja suala la kupata kazi zinazohitaji taaluma, kujitolea kunaweza kuwa ni "connection" ya mtu kubaki na kuajiriwa kwenye Kampuni au Taasisi aliyojitolea.
Marehemu Ruge Mtahaba aliyekuwa Mkurugenzi wa "Clouds Media Group", aliwahi kusema kuwa "tafuta nafasi kwanza, ukishapata nafasi onyesha uwezo, baada ya kuonyesha uwezo, pesa zitakuja zenyewe".
Mfano mzuri ni Millard Ayo, Mtangazaji na Mwanahabari kutoka hapa Tanzania. Millard alianza kutangaza kwa kujitolea kwenye redio moja ya Dini hapa Jijini Dar es Salaam.
Alipopata nafasi akaonyesha uwezo, kujitolea kwake kukawa ni " connection" ya yeye kusikika na kuajiriwa na redio nyingine.
Nina mfano wa kinyozi mmoja maeneo ya Ubungo, yeye aliingia saluni moja akasema anaomba ajitolee kunyoa hapo bila malipo yoyote. Kumbe huyo kinyozi alikuwa fundi kweli, alinyoa kwa siku tano tu kila mteja akamkubali, ikabidi tu mwenye saluni aongeze kinyozi mmoja bila kupenda.
Hizo ndizo mbinu za kijasusi za mtu kutafuta "connection" ya kazi.
Katika fani yoyote ile, jaribu kujitolea. Najua pesa ya nauli ni changamoto, najua pesa ya kula ni tatizo lakini jikaze kwani mvumilivu hula mbivu.
Hivyo ndiyo ambavyo kujitolea kunaweza kuwa "connection" ya wewe kupata kazi.
Tatu, jipendekeze (kuwa chawa) wa mtu, watu, Chama au Kampuni fulani. Tupo katika Dunia ya ushindani sana ambapo mtu unahitaji mbinu nyingi sana ili uweze kuishi.
Kujipendekeza kwa kufanya au kuongea mambo mazuri kuhusu mtu au watu ili upate "connection" ya kazi au pesa siyo dhambi.
Dhambi ni kujipendekeza kwenye mambo ya kijinga.
Wanasiasa wengi chipukizi wametumia hii mbinu kupata nafasi za uongozi.
Vijana wengi wametumia hii mbinu kupata vyeo.
Wanafunzi wengi wametumia hii mbinu kuwa viranja. Si jambo baya, maisha ni vita na hiyo ni silaha inayotumiwa na baadhi ya watu kupata "connection" ya kazi.
Usishangae kuona mtu akisema kuwa yeye ni "chawa" wa msanii fulani au chawa wa kiongozi fulani.
Usishangae, hizo ni mbinu za kijasusi zinazotumiwa na watu wenye njaa ya mafanikio kupata kazi au kubaki sehemu walizopo.
Kamsi inaeleza kuwa, kujipendekeza ni kitendo cha mtu kuwa mstari wa mbele kusema au kufanya jambo fulani. Kwahiyo, kujipendekeza siyo dhambi, dhambi ni kujipendekeza kufanya mambo ya kijinga.
Acha wakucheke kuwa unajipendekeza ila mwisho wa siku watakuona unapata kazi.
Hata katika familia mtoto anayependwa ni yule anayejipendekeza kufanya kila kazi.
Kujipendekeza ni "connection" tosha.
Nne, jitokeze sehemu mbalimbali za jamii ili kukutana na "connection" ya watu tofauti tofauti. Usijifungie chumbani tu halafu ukategemea kupata "connection" ya watu tofauti tofauti. Hiyo itakuwa ni ndoto ya mchana kweupe.
Hudhuria mikutano ya kisiasa, hudhuria semina za fursa na maendeleo, hudhuria sehemu za kuabudu, hudhuria matamasha ya burudani na kadhalika.
Sehemu zote hizi utakutana na marafiki na watu tofauti tofauti ambao wanaweza wakawa "connection" ya wewe kupata kazi.
Rafiki yangu mmoja alisomea masuala ya masoko, yeye ni mtaalam sana wa kuandaa mawazo (proposal) za biashara. Siku moja alihudhuria semina moja ya fursa na biashara. Sehemu aliyokuwa amekaa, kwa mbele yake akamuona Meneja masoko wa Vodacom. Baada ya semina, akamganda Meneja masoko huyo kumuonyesha mawazo (proposal) zake. Kwa ajili ya mda ikabidi Meneja huyo ampe namba za simu huyu kijana ili amwambie siku gani atakuwa na mda wakutane ofisini.
Huwezi amini, "connection" ilianzia hapo.
Wakawasiliana akapeleka mawazo yake ofisini. Na sasa huyo kijana ni mfanyakazi wa Vodacom.
Kumbe kushiriki kwake ile semina ya fursa na biashara ndiyo kulimfanya akutane na "connection" ya kazi.
Tano na mwisho, uaminifu wako, sifa toshelevu, vigezo vya kutosha na uwezo wako mkubwa ni "connection" moja wapo ya wewe kutafutwa na kupata kazi.
Safisha wasifu wako, boresha uwezo wako, tengeneza uaminifu, tengeneza jina, utapata simu za kazi na 'michongo' ya pesa.
Ahsanteni.
Na Mungu awabariki.

Upvote
18