Haijalishi kama wewe ni KE au ME, kama unafikiria kuingia kwenye mahusiano au tayari uko kwenye mahusiano na kuna vitu havieleweki au unajiuliza maswali na hupati majibu, basi habari hii inakuhusu. Iko hivi, kama ukipewa uchaguzi wa kuingia kwenye mahusiano na mtu unayempenda au anayekupenda, usichelewe! ingia na mtu anayekupenda - utakuja kunishukuru.
Hapa nazungumzia mtu anayekupenda kwa dhati, si mbabaishaji, hivyo inabidi ujiridhishe kama kweli upendo wake ni wa dhati kwako. Lakini pia inategemea tafsiri ya upendo kwako ni nini (Hii yaweza kuwa mada ya siku nyingine). Uzoefu unaonesha kwamba ni nadra sana kuwa kwenye mahusiano (Ya Kawaida au hata ya ndoa) na mwenza ambaye wote mnapendana kwa nguvu sawa, mara nyingi mmoja atapenda zaidi kuliko mwingine. Hivyo, ni bora wewe uchague upande wa kupendwa kuliko wewe kupenda. Anayekupenda ameshakutafiti, ameshajiridhisha na amefanya maamuzi ya kuwa na wewe. Atajenga na kupalilia upendo wake kwako, atakuheshimu, atakusikiliza, atakujali bila masharti. Anayekupenda atakuwa flexible kwako, atapanga ratiba zake ili akujumuishe wewe maishani mwake. Anayekupenda yuko tayari kwa ajili yako, atayaona mengi mema yako na kufurahia kila mafanikio yako.Atakuonea huruma wakati wa matatizo na atakusaidia kutafuta uvumbuzi wa changamoto zako. Hata mkitofautiana mtazamo na anayekupenda na kusababisha mfarakano, namna ya kusuluhisha kwa anayekupenda ni tofauti na unayempenda. Kuwa na mtu anayekupenda ni salama na amani. Sasa kama hutaki salama na amani unataka nini?
Ukiingia kwenye mahusiano na mtu unayempenda ni sawa na kucheza kamari, unabahatisha, upate ama ukose, na unauweka moyo wako hatarini. Unayempenda atakuweka kwenye mizani, ataendelea kukupima kila siku bila ukomo. Utakumbana na visingizio vingi kwa unayempenda kuliko anayekupenda. Unayempenda atakupa kazi ya ziada kuthibitisha kama kweli wewe ni mtu sahihi kwake. Utake au usitake, unayempenda atakuwekea masharti, na hana sababu ya kukuheshimu wala kukusikiliza, na hana sababu ya kukujali - si unampenda? Unayempenda ni rahisi kuona mabaya yako kuliko mema yako, na ni mzito kufurahia mafanikio yako. Unayempenda bado hajafanya maamuzi ya kudumu kuwa na wewe, na ataendelea kupepesa macho yake mahali pengine, si unampenda? Kumbuka wakati mwingine anafanya yote si kwa roho mbaya, bali moyo wake ndio unavyomtuma.
Chagua usalama na amani ya moyo wako, nenda na anayekupenda na kiroho safi mpige chini unayempenda.