kajojo
JF-Expert Member
- Jun 9, 2012
- 2,946
- 5,470
Yapo karibu kwangu nikuelekeze
niwekee picha hapa kama mto mada ntaelewa tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yapo karibu kwangu nikuelekeze
ungeshea hiyo plan ya kulaAyo yote Tisa mkuu mazoezi ya tumbo ni chakula tu ukiwa unakula hovyo hata ufanyaje hutopata matokeo chanya hata kidogo nimehangaika sana na hili zoezi bila mafanikio nimekuwa muhudhuriaji mzuri wa gym napata matokeo chanya kote ila tumboo likanishinda kabisa ila sasa nimebadili life style yangu ya kula kabisaa huu ni mwezi wa pili sasa nina six packs zinakuja kwa speed na rate ya mazoezi ya sasa ni ndogo sana ukicompare na mara ya kwanza
Fanyeni yote usipojua kuheshimu chakula kitambi hakiepukiki
Yeap,Mazoezi ukiyazoea inakuwa ni kama starehe. Nilianza kuota kitambi mara tu nilipopata kiajira na kuanza kuzikunja noti na kubahatika kupata kausafiri kakutembelea, nikaona sasa huko ninapoelekea nitapasuka. Nikiangalia muda wa kufanya mazoezi nakosa kabisa, naingia kazini asubuhi narudi jioni. Nikaona chakufanya hapa ni kuamka alfajiri nifanye mazoezi ndio niende kazini. Nikaanza kuamka saa 11:00 alfajiri kila siku, naenda uwanjani kukimbia kuzunguka uwanja. Siku ya kwanza nilizunguka mara 6, siku zilivyozidi kwenda nikawa naongeza, hatimaye nikawa naweza kuzunguka mara 35, na nikitoka kukimbia nikifika home nafanya mazoezi ya tumbo kama crunches, sit ups, n,k.
Siku hizi nimebadili utaratibu, sihesabu tena mizunguko ninayozunguka uwanja bali nakimbia kwa saa 1 bila kupumzika. Kitambi kimeyeyuka na nina six-pack, najisikia vizuri muda wote, nimechangamka na ninajiamini. Nimezoea kufanya mazoezi hadi nikikosa kufanya nahisi kupungukiwa kitu kwa siku hiyo.
Ukichukulia mazoezi ni adhabu, utafanya kwa siku chache na kuacha. Mazoezi ni matamu asikwambie mtu. Tufanye mazoezi wakuu.
Nimeona nishee hii ili wengine nao wahamasike
Kaka/dada kumbuka fitness sio kuwa slim. unaweza fanya mazoezi ukawa fiti na usiwe slim, lakini kama unafanya mazoezi stahili huwezi kuwa na tumbo la kizembe (yaani ukitembea linatepeta) bali linakuwa gumu na unaweza kukimbia au kufanya kazi nzito au kunyanyua vitu vizito bila kusikia maumivu ya tumboHaya mazoezi nimefanya sana lakini tumbo halikubali kuwa flat hata kidogo zaidi linakuwa gumu sana kwa ndani.
Safi sana mkuuYeap,
Ratiba yako kama ya kwangu isipokuwa tunatofautiana aina ya mazoezi. Naamka saa 11 kasorobo, naruka kamba hata idadi simaindi sana, napiga push ups 100 daily (arobaini, napumzika, 30 namalizia 30). nasukuma kitairi mara 60 daily (round moja 10). Nanyosha viungo kasha natamatisha mazoezi. Niko fiti sitaki kuwa slim na sitaki kitambi ila niko fiti mwili hauna mabonde mabonde. Mazoezi ni raha kushinda unywaji wa pombe
Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia GymYeap,
Ratiba yako kama ya kwangu isipokuwa tunatofautiana aina ya mazoezi. Naamka saa 11 kasorobo, naruka kamba hata idadi simaindi sana, napiga push ups 100 daily (arobaini, napumzika, 30 namalizia 30). nasukuma kitairi mara 60 daily (round moja 10). Nanyosha viungo kasha natamatisha mazoezi. Niko fiti sitaki kuwa slim na sitaki kitambi ila niko fiti mwili hauna mabonde mabonde. Mazoezi ni raha kushinda unywaji wa pombe
Ok thanks. Hii ya ngumi huwa nafanya sema si kila siku sababu ya mudaChukua chupa la lita 1.5 la Kilimanjaro jaza mchanga,then uwe unalirusha mbele nyuma,nyuma mbele..kama unasukuma bembea sio kurusha udake[emoji3]
Au piga ngumi hewani...
Asante sana ngoja nikazaneFanya aerobics na kujog. Kwakua unataka kupunguza kilichoongezeka unahitaji kupunguza fat.
Usiache kuruka kamba.
Mimi hua napitisha miguu chini ya meza au kitanda.Mkuu hii unaweza kuipiga ukiwa peke yako? Yaani kila nikipiga najikuta nasogea ila wife akinishika mguu kwenye vidole kwa kukandamiza chini, hua nalala na kunyanyuka kwa wepesi sana na kwa harakaharaka. Vipi kuna njia ya kupiga nikiwa mwenyewe?
mkuu reps maana yake nini?reps .
Ni kama set ya mazoezi mkuu au roundsmkuu reps maana yake nini?
asante sana mkuu ila hii Crunches imenishinda kuinukaMfano unafanya sit ups, kile kitendo cha kunyanyua mwili na kuurudisha pale ulipoanzia ndiyo kinaitwa rep, zikiwa nyingi ndiyo reps.
Ni kama mdau alivyokwambia hapo juu.
Pia Ni kifupi cha repetitions.
The same here but sasa hivi yameshaachiaNakimbia uwanja Mara 15 kila siku jioni... Napiga mazoezi yote ya kukata tumbo... Napiga mazoezi ya stamina za miguu n.k
Najihisi nimezaliwa upya Niko poaaaaaaaa kabisa...
Fuatilieni comments zangu hapo juu muone maumivu niliyoyapata wiki ya kwanza... Sitasahau kwa kweli
poaNi ngumu au haujaielewa?
Hua nahisi hii ndiyo nyepesi kushinda zote.
Ila jitahidi kupiga hata tano zikiwa perfect utakua ukiongeza kidogo kidogo.
Hahahaha mkuu mbona mazoezi ya six packs ni miongoni mwa yanayoweza kufanyika nyumbani? Yaani siyo lazima uwe na vifaa vya gym ili upate unachotaka...Six packs yataka moyo sana mpaka kuzipata especially ukiwa unafanya mazoezi kwenye kagym kako ka maskani....
Njia ya haraka ya kupata hizi kitu ni kupiga zoezi la V...