Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Nataman Sana watu wajue Utamu na raha nijisikiayo mm, mazoez ni raha jamani. Unakua na afya ya akili na mwili, pia ukivaa nguo zinakaa unaonekana mtu wa fashion
 
Tupe siri ya mafanikio, nasikia ukiacha unabaki skeleton ni kweli?
Hahaha ukiacha utabaki skeleton kweli, nijuavyo mimi Siri ya mafanikio ni kufuata program za mazoez kiusahihi, kula vzr hasa vyakula vya kujenga mwili, pata muda wa kupumzika, Mwisho ni Uvumilivu. Note: usikubali kupitisha siku tatu bila kufanya mazoez.
 
mazoezi yakifika kwenye kiwango cha juu raha sana fikiria umekimbia km 20 asubuhi halafu unanyoosha viungo baada unakunywa maji ya uvuguvugu raha sana kijasho kwa mbali
 
Sana sana inakua mwanzoni ila baada ya muda unakua unaona ni kawaida na utakua unaenjoy zoezi lako.
mkuu castr hiyo sit up nusu kwa nusu unapoanzia chini bila kufika magotini na unapoanzia kati kufika magotini ndani ya reps moja nifanye zote mbili au kila moja inajitegemea
 
mkuu castr hiyo sit up nusu kwa nusu unapoanzia chini bila kufika magotini na unapoanzia kati kufika magotini ndani ya reps moja nifanye zote mbili au kila moja inajitegemea
Hapo kila moja itajitegemea.

Mfano Utaanza nusu za kuanzia kati na kuyafuata magoti kisha unamalizia na nusu za kuanzia chini na kuishia kati.
 
mazoezi yakifika kwenye kiwango cha juu raha sana fikiria umekimbia km 20 asubuhi halafu unanyoosha viungo baada unakunywa maji ya uvuguvugu raha sana kijasho kwa mbali
Halafu unalala kidogo ukiamka unapata msosi kisha unaendelea na maisha ya siku hiyo.....
 
MAZOEZ YANAHITAJI MOYO WA CHUMA NA SALA...MIMI NILINENE MPAKA NIKITEMBEA KIFUA KINATIKISIKA NYAMA,,NIKAPIGA DIET PLAN YANGU MOJA KWA WIKI MBILI NIKAWA KAMA MODEL SASA NDO NATAKA NIINGIE GIM SEMA NATAKA MWALIM NIMWELEZE NAVOTAKA KUA MAANA MAFUTA YOTE NIMETOA
Mkuu ulipiga ile ya GM diet plan nini? Naigopaaaaa!!!
 
we manjagata kile kitairi kinauzwa 18000 kama upo dar tembea kwa miguu kuanzia karume kama unaelekea kariakoo utakuta vijana wanauza pia kabla hujafika kariakoo kuna duka la vifaa vya michezo upande wa kushoto
 
Inakuaje wadau?

Majukumu na lifestyles zetu hua zinaweza kupelekea fat ikajikusanya mno tumboni na kupelekea kutokea kitambi au tumbo ambalo tunakua hatujaridhika nalo.
Ikifika hatua hiyo tunachotakiwa ni kuiondoa hiyo fat hapo ilipo ili kupata lile tumbo ambalo litaridhisha macho yetu.

Haya mazoezi yanaweza kufanywa kokote na jinsi zote wanaweza wakafanya.

Jua kwamba.
Kuna mazoezi mengi ya kupunguza tumbo, haya ni yale ambayo nayatumia mimi hivyo mengine yapo modified kwa kadri mimi ninavyoyafanya.

Kisayansi six packs hazihesabiwi kama ni alama ya mtu kua ni mwenye afya, hii ni kwa kua unakua umeondoa fat yote tumboni ambayo tumbo lako huihitaji. But fvck science on this one.

Na-assume sisi ni beginners, kama uko advanced ongeza idadi ya reps (30).

Kanuni Yetu Ni Hii.
-Kila zoezi litakua na seti tatu.
-Kila seti moja itakua na reps 10 mpaka 12.
-Kupumzika kati ya reps na reps ni sekunde 15.
-Kupumzika kati ya zoezi na zoezi ni dakika moja.

Tuanzeni...

Kuendesha Tairi.
View attachment 465984
Utakua ukianza kwa kurudisha nyuma tairi na kukipeleka mbele kiasi mgongo wako unakua umenyooka. Ukipeleka mbele ukikirudisha hiyo ni moja.
Kwa sisi ambao hatuna balansi, napendekeza upande tunaojinyoosha kuwe na kitu cha kutuzuia ili tusiende chini moja kwa moja mfano kukiwa na ukuta itakua vizuri zaidi.
Hapa tunafanya reps 10 kwa seti tatu.

Crunches.
Unakua umelala chini magoti yameinuka, unaunyanyua mwili nusu, yaani sehemu ya kiuno inakua hauiinui.
View attachment 465986
Unakua unainuka lakini bila lengo la kuyafikia magoti yako. Ukinyanyuka na kurudi chini hiyo ni moja.
Hapa tunafanya reps 12 mara tatu.

Crunches Miguu Juu.
Unakua umelala ila miguu inakua juu ya kitu, sehemu miguu itakayokaa isikufanye kuuinua mwili wako iwe adhabu mimi huwa naweka juu ya kitanda.
Ukiwa gym unaweza chagua benchi la kuwekea miguu yako.
View attachment 465988
Kama utaweza kuinuka mpaka kuifuata miguu yako na kuishika itakua vizuri, kama hauwezi panda kiasi cha kiuno chako kisiwe kimelala chini. Kama bado hauwezi fanya kama ulivyotoka kufanya zoezi lililopita.
Hapa tunafanya reps 10 mara tatu.

Sit ups.
Unakua umelala na miguu umeinyanyua, hapa utanyanyua mwili wako wote wakati unayafuata magot yako lakini wakati unarudi chini mwili usiguse chini, sehemu ya kiuno na mgongo kidogo ndiyo utakua unailaza sakafuni.
View attachment 465990
Hapa kurelax hupatikana kutokana na ukali wa mbinuko wa magoti tuliouweka, mfano mbinuko wa kwenye hiyo picha kwa anayeanza ni mkali mno.
Tunafanya reps 10 mara tatu.

Sit Ups Nusu Nusu.
Hizi nilizimodify kutokana na mahitaji yangu, hilo jina nimetunga hapa hapa (sorry).
Inakua sawa na zoezi lililopita isipokuwa hapa tunanyanyua mwili na kuishia kati kisha tunarudi chini baada ya hapo tunaanzia pale kati tulipokua tunaishia na kuyafuata magoti.
View attachment 465993
(Samahani sijui kuchora.)
Hapa tunafanya za kutokea chini na kuishia kati reps 6 na kuanzia hapo kati kueleka magoti reps 6. Tutafanya hivyo mara tatu.

Sit Ups Tatu kwa Moja.
Hii ni nyingine ambayo niliimodify.
Utalala chini kama kawaida ila Miguu yako utaitanua kiasi cha kuweza kuona mbele.
View attachment 465995
Utakua ukinyanyuka mikono yote unapeleka upande wa kushoto, unarudi chini.
Ukinyanyuka tena mikono unapeleka upande wa kulia, unarudi chini.
Ukinyanyuka mikono utapitisha kati kati ya miguu.
Hiyo ni moja.
Tutafanya hivi reps 3 mara tatu.

Oblique Sit Ups.
View attachment 465991
Tunafanya kama zoezi lililopita, ila hapa utakua ukiinuka kuyafuat magoti yako kiwiko cha mkono wa kulia kitakua kinaenda upande wa goti la kushoto na kiwiko cha upande wa kushoto kitakua kinaenda upande wa goti la kulia.
Mfano, Utakua unanyanyuka kiwiko cha kulia kitaenda upande wa kushoto, utarudi chini, utanyanyuka tena kiwiko cha kushoto kitaenda upande wa kulia, utarudi chini. Hiyo ni moja.
Tutafanya reps 7 kwa seti tatu.

NB.
-Jiandae kwa Maumivu ya tumbo na kuharisha kwa siku moja au mbili.
-Kama una kitambi kikubwa sana napendekeza main dish ya zoezi lako iwe ni kukimbia mpaka baada ya muda, pia anza na zoezi la 1, 2, na 3 mengine utayaongeza polepole kadri utakavyokua unaendelea.
-Mapendekezo yangu ya reps na seti unaweza ukapunguza au ukaongeza kulingana na mahitaji yako na uzoefu wako.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako na sisi tujifunze.

Picha zimetoka mtandaoni.
Ok ntajarib
 
we manjagata kile kitairi kinauzwa 18000 kama upo dar tembea kwa miguu kuanzia karume kama unaelekea kariakoo utakuta vijana wanauza pia kabla hujafika kariakoo kuna duka la vifaa vya michezo upande wa kushoto
Ila mimi nilinunua 10,000
 
Ok ntajarib
Karibu kwenye Body For Life Challenge, kuna uzi nimeuanzisha wenye lengo la kutiana moyo. Itatuchukua wiki mbili kwa routine yote.
Challenge itaanza kesho.

Check username ya Castr angalia posts, kisha threads angalia uzi umeandikwa "Body For Life Challenge: Jiunge na Mimi"

##Body4LyfChallenge
 
Back
Top Bottom