Unatumia mbinu gani kusafisha sufuria lililoungua sana wakati wa kupika?

Unatumia mbinu gani kusafisha sufuria lililoungua sana wakati wa kupika?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Habari wana jukwaa hili

Wakati mwingine mtu unapika chakula inatokea bahati mbaya kinangua sana hadi chombo kinakuwa cheusi( kwa sisi wenye masufuria ya kaida). Au nje ya sufuria ukipikia mkaa inakuwa nyeusi, kusafisha kirahisi ili iwe rahisi kufaya sufuria zetu ziwe na mng'ao wa awali.

Wakati wa kuosha unasugua hadi unachoka ila chombo kinagoma kabisa kurudia ile hali yake ya awali.

Tujuzane njia rahisi ya kusafisha.

1671355710466.jpeg
 
Kama nimeunguza sufuria kwa ndani huwa nachemshia maji na chumvi ..kule kuungua kuna yeyuka halafu natumia sabuni ya vyombo ya maq (ya maji) na vile visugulia sufuria vinavyo uzwa kwasasa.... Yani sufuria zinang'aa na hutumii nguvu...... Hata sabuni ya magadi nayo nzuri kwa kungarisha.
 
Kama nimeunguza sufuria kwa ndani huwa nachemshia maji na chumvi ..kule kuungua kuna yeyuka halafu natumia sabuni ya vyombo ya maq (ya maji) na vile visugulia sufuria vinavyo uzwa kwasasa.... Yani sufuria zinangaa na hutumii nguvu...... Hata sabuni ya magadi nayo nzuri kwa kungarisha.
Asante sana Mkuu, nitajaribu njia yako hii.
 
Mimi huwa nailoweka kwanza na maji usiku kucha halafu baada ya hapo naisugua na steel wire na sabuni ya magadi inatakata inakuwa kama mpya. Jaribu hii hata kusugilia sufuria kawaida
 
Ngoja nitege hapa, nione wanaounguzaga mboga. 😅😅
 
Mimi huwa nailoweka kwanza na maji usiku kucha halafu baada ya hapo naisugua na steel wire na sabuni ya magadi inatakata inakuwa kama mpya. Jaribu hii hata kusugilia sufuria kawaida
Asante mkuu, nayo nitajaribu
 
Habari wana jukwaa hili

Wakati mwingine mtu unapika chakula inatokea bahati mbaya kinangua sana hadi chombo kinakuwa cheusi( kwa sisi wenye masufuria ya kaida). Au nje ya sufuria ukipikia mkaa inakuwa nyeusi, kusafisha kirahisi ili iwe rahisi kufaya sufuria zetu ziwe na mng'ao wa awali.

Wakati wa kuosha unasugua hadi unachoka ila chombo kinagoma kabisa kurudia ile hali yake ya awali.

Tujuzane njia rahisi ya kusafisha.

Wale mabechala wenzangu tunaoyatupaga kama boxer chafu tujuane 😃
 
iloweke na maji
kisha imwage maji
ikwangue huo ukoko wa kuungua sana chukua mkaa sugulia baada ya hapo tumia sabuni yamagad na steel wire
 
Back
Top Bottom