Unatumia mbinu gani usipigwe na mafundi kwenye ujenzi?

Kuna fundi anaanza kukuibia kuanzia dukani mnanunua materials, anawaseti mapema kabisa jamaa wadukani..
Hii kitu umenikumbusha mbali sana ndugu yangu. Hasa pale Buguruni (Dar) kwenye mbao kuna Wezi Wabobevu. Unapigwa na kitu kizito kichwani huku unaona. Tena ni afadhali usiende na Fundi watakupiga kidogo, ukijifanya wewe ni mfuatiliaji na mbishi fundi anawatonya pale pale huku unaona na wanakushughulikia ipasavyo.
 
Tafuta MTU anayejua anataka nini katika MAISHA yake.

MTU anayejua anataka nini hatoweza kuiba hata msumari mmoja.

Kazi inajengwa ktk credibility and Trusting

Fanya kazi na MTU anayepambana kukua katika kazi yake na hao wapo wengi tu na wanafanya kazi vizuri.

Then zingatia kuwa recommendation ukihitaji MTU safi na ambaye anajua kuwa uaminifu ndo msingi wa yeye kupata kazi zaidi check me.

I will recommend to you the right person and you will never regret.
 

Lets say ndo ujenz wako wakwanza ni vipi utajua makosa na kujifunza tips za ujenzi bila kujipa muda kwenye site zako husika? Nafikiri idea zinapatikana kwenye ujenz kwenyewe ili hue pro badae usikae site.
 
Mm ningekutimua fasta na kumuita fundi mwingine
 
Kupigwa lazma upigwe tu, anapigwa mgonjwa mahututi itakuwa wewe mtu mwenye afya kabisa. Uadilifu ni tatizo kubwa sana nchini na tunaishi nalo hivyo hivyo tu bongo kila mtu mwizi hata kiongozi wako wa dini ni mpigaji. Usiangalie kupigwa hakikisha tu kazi imefanywa kwa ubora wa juu.
 
Mm ningekutimua fasta na kumuita fundi mwingine
Hii sekta ina vitu vingi sana mkuu, kuna maboss wengine wamepata zari tu la hela ghafla na kuamua kujenga, wakiwa hawana msingi, mtu anajenga bila kujua badget kamili ya jengo lake hivyo kuna boss kuishiwa pesa na fundi ukabaki unadai ama hata kuzulumiwa kabisa

Sasa miongoni mwa vitu nlikuwa nazingatia ni kuchukua advance mapema mkuu, maanake ukinitimua mm nakuwa sina hasara ila wewe utaingia hasara kumlipa tena fundi mwingine
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mkuu ujue suala la kuiba buana ni kama hulka tu,, nikiwaza kuna mkurugenzi wa halmashauri kafutwa kazi kisa mil 2, kwann mm nsiibe misumali
Kuibia mtu mmoja si sawa na kuibia Gavo. Mtu mmoja atasuffer sana ila Gavo angalau ingawa miradi ya maendeleo itakwama
 
Yaani unakuta anaeogopa kuibiwa na fundi,iyo ela ya kujengea nayeye katoka kupiga mahahali.hasa hawa wa serikalini.
 
Ntakupigaa makofi mbele ya saidia fundi wako
 
Unachosema ni kweli kabisa hata wagonjwa wa akili huwa wanajiona wako sawa kabisa kwa wanachokiongea na kukifanya ilhali ni tofauti na mawazo wanayojiona kuwa wapo sahihi.
 
utafanya hivyo kama fundi upo peke yako, ila kama kuna wenzio wanamezea mate hiyo hiyo nyumba, utakubali tu yaishe. bati niliagiza kiwandani kwa vipimo vya nyumba, vifaa vyote vya umeme nilienda kununua mimi mwenyewe. niko makini na haikuwa mara yangu ya kwanza kujenga, washaniibia sana miaka ya nyuma. hasa cement na nondo. kwangu mimi kama huendani na masharti yangu, nakufukuza naweka fundi mwingine. wala sisumbui akili wakati pesa nilitafuta kwa jasho langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…