Unatumia sabuni gani kuogea?

Unatumia sabuni gani kuogea?

Zamani tulikuwa tunatumia Emperial toka Malawi na Zambia, nyingine ilikuwa kitu kama Vinolia Lavender kama sikosei toka Zambia.Pia Wengi tuliipenda Geisha, na enzi ya shule tulitumiaga Fa Wana wa CHAPUTA wataikumbuka.
Ila sasa hivi nami natumia Jamaa ni sabuni nzuri.
Binafsi natumia Jamaa pia.. ni nzuri sana
 
Wakati wa break ya taarifa ya habari inayosomwa na Betty Mkwasa ITV miaka ya 1997 na 1998, baada ya habari za kitaifa utaskia tangazo:-

Nieleze siiiri ya urembo wako......''sio sirii ni Revola''

Tinti..ndiiii
Betty Mkwasa pia kuna muda alikuwa anasoma marehemu Asha Mtwangi, au marehemu Julius Nyaisangah "Anko Jay". Dah nimekumbuka mbali sana
 
Wewe mtoto wa juzi, sisi enzi zetu japo ni wanaume, tulikuwa tunaogea GIV halafu ukioga hujifuti sana ili ukienda kumtongoza kabinti kasikie harufu ya GIV
View attachment 1263146
Aisee, nimeulizwa sabuni gani natumia inamaanisha sasa. Nikitaja sabuni nililizokuwa natumia we utachanganyikiwa maana zingine wewe unavyozaliwa hata hazikuwepo
 
Yangu hiyo hapo.

DBECD386-DC69-4E44-865E-8559147CBACF.jpeg
 
Back
Top Bottom