Unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi?

Unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi?

Maandazi ya mafuta ni yakoje hayo?
Dah! Sijui hata nikueleweshe kwa lugha gani uelewe maana kwetu tunaita hivo kwenu sijui mnaitaje. Lakini ninayozungumzia ni yale maandazi unayokuta yanaingizwa kwenye mafuta ya kupikia na mengine yanaekewa mkaa kwa juu bila kuingizwa kwenye mafuta hujayaelewa?
 
Heshima yenu wadau.

Nimekaa muda huu nikakumbuka kifungua kinywa changu. Nimekula vitumbua 10 na supu ya utumbo.

Kitumbua kimoja shilingi 100 hivyo nimetumia 1000 kwa ajili ya vitumbua. Supu ni 500.
Jumla asubuhi nimetumia 1500.

Mwenzangu unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya asubuhi?

Sitaki niwe choo chako, jamaa unatisha yaani vitumbua 10 na supu peke yako?
 
Dah! Sijui hata nikueleweshe kwa lugha gani uelewe maana kwetu tunaita hivo kwenu sijui mnaitaje. Lakini ninayozungumzia ni yale maandazi unayokuta yanaingizwa kwenye mafuta ya kupikia na mengine yanaekewa mkaa kwa juu bila kuingizwa kwenye mafuta hujayaelewa?
Kweli umenikamata mi najua skonzi na mkate ndiyo unaandaliwa hivyo sikujua na maandazi yanaweza kuandaliwa hivyo hivyo
 
napenda sana kiporo cha wali maharage kama nipo hom na kama wali ulibaki...

kama Sipo hom inategemea na someday buku.. buku 2.. buku 3 ila haizidi buku 5. labda nipewe ofa

cc Smart911

cc Smart911
 
Usawa huu chai ya nini, nakula katikati ya mchana na usiku inatosha.
 
Mihogo ya tsh 500 na azam cola tsh 500 na maji ya uhai ya 500 jumla 1500 mchana napiga long pass jioni naenda kula kwa wife msosi mtamu
 
Chai mia andazi mbili za mia mia (100+200=300)
Jiti tatu tu mkuu
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom