Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Ngoja leo nizipike nione nami hunishinda hivi nusu natakiwa nitoe chapati ngapi ?
 
Maandazi ndio nimefanikiwa kuelewa. Chapati za kusukuma bado bila bila 😂😂

Ila nitakaza mpaka mwaka uishe huu niwe nimeelewa.
0E4370D3-EF33-4179-95E9-EB9B2989B3E4.jpeg
59F5F655-CCF8-4F13-A2F4-7E883E21A95B.jpeg
 
Nikiona chapati za hivi nikalinganisha na zangu najiona sina bahati

Usihangaike na mie kwenye chapati,nishajikatia tamaa 🤧
Usinichekeshe bhaana kamamaa, tutaongea vyema siku moja ukipata moyo tena wa kujaribu, tuone ni wapi panatatiza,

You can do better than that I know,
 
Nikiona mada za chapati namkumbuka dada yangu Carleen
Binafsi mbinu zote nimemaliza lakini tokeo la mwisho ni lile lile either kaukau ama ugumu...nimeamua kukubali kushindwa
Usikate tamaa rudia tena kujifunza. Kuna watu ni watalaamu wa kupika chapati. Zungumza na mojawapo aje kwako au uende kwake akupe usimamizi wa hatua kwa hatua hadi upatie. Na ukipatia fululiza hata miezi mitatu kwa kila wiki uwe unapika chapati walau mara 4 hii itakufanya uweze kufuzu na kumudu kuwa mpishi mzuri wa chapati.
 
Kuna kijiji moja nlienda, kuna migahawa miwili.
Wa kwanza n mams mmoja anajidai mjanja mjanja, akipika chapati anaweka kama 10 hv kwenye kikaango, zikitoka n kama shuka za gesti, nyeupee af mbichi!
Wa pili n mmama mtu mzima, ye hana haraka, taratiibu hatauwe mia, atachoma moja moja. Changamoto yake ni hygiene. Anaeza akasukuma, ghafla akajikuna mguu af akaendelea. Lakini zake zimeiva na tamu.
But kwa hawa wadada wa siku hz kabla hujaeka kambi bora ujue kwanza anaju kuzisukuma au la. Maana unaoa pisi kali, af anakupikia "amoeba" instead of chapoo
Mwanamke asipojua kupika chapati ni changamoto sana babu.
 
Ipo waarabu hutengeneza kama hiyo ya yesu wanaita mikate migumu sijawah ona ladha yake kiukweli ila waarabu wanapenda ni chakula chao
Ile hailiwi kavu kavu, lazima uwe na nyama ya kondoo, mbuzi au kuku ya mchuzi ule mchuzi dikodiko ndio unalia hizo chapati.

Kulikuwa na mgahawa pale mitaa ya upanga walikuwa wanauza hiyo unapewa kuku mzima na huo mkate mmoja. Ilikuwa ni 10,000.
 
Chapati Kanda na maji ya kawaida au vuguvugu(warm water) tia sukari kidogo sana (a pinch of sugar)chumvi maji unaweza tia maziwa ya unga kiasi kama unayo au cream ya maziwa ile ya juu na mafuta ya kutosha yasiwe mengiii kama hauna chumvi sukari maji mafuta inatosha Kanda unga wako ukisha kandika Sasa sukuma ukunje napo tia mafuta au samli ya kutosha mpaka umalize madonge yote Kisha yafunike na cling firm au nguo safi Vitambaa vya jikoni kisha unga ukiona madonge yameregea ndio usukume na ukisukuma usigeuze unga juu chini endelea kama yalivyokuwa juu juu chini chini Anza kuchoma upande mmoja ukiwa wa brown ugeuze upande wa 2 napo ukibadilika tia mafuta yasiwe mengi sana itajaa mafuta ya kiasi choma ukinyima mafuta inakuwa kavu na usijaze mafuta Kisha kunja ×4 iwe kama pembe 3 itoe.(nb ukunjanji wa chapati kila mmoja ana ukunjanji wake.
 
Back
Top Bottom