Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Nikiona chapati za hivi nikalinganisha na zangu najiona sina bahati

Usihangaike na mie kwenye chapati,nishajikatia tamaa [emoji1784]
Usichoke bhana,je wakati wa kukanda unga huwa unakanda na mafuta kiasi au maji tupu.
 
Siko vizuri Sana kwenye uandishi hasa kwenye kueleza Jambo Kwa mtiririko.

Lakini,binafsi huwa ninatumia mafuta ya cowboy kukanda unga wa chapati.

Huwa Nina weka chumvi na sukari kidogo Sana,hii inaongeza ladha.

Baada ya kukanda Kwa muda usiopungua DK 20,ninafunika,Joto linasaidia pia kufanya chapati ziwe laini.

Wakati wa kusukuma matonge ili kuweka mafuta Kabla ya kukunja,huwa ninaweka mafuta na kunyunyiza unga wa ngano kidogo,kisha nakunja matonge.

Moto mdogo wakati wa kupika lakini pia mafuta mengi.

Lakini pia huwa ninaweka chapati zaidi ya 3 jikoni Kwa wakati mmoja,hii pia husaidia Joto kutoka chapati moja lisipotee,hivyo kufanya chapati kuwa laini.
 
Habari Wakuu,

Chapati za kusukuma ni pishi ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi, mtu anajitahidi alkini mwisho wa siku anatoa chapati ngumu na imesimama kama sinia[emoji23][emoji1787].

Mbinu ninayotumia mimi kufanya chapati iwe ni laini, ni kukanda unga na kuhakikisha umekuwa laini kabisa. Tumia hata muda mrefu kama huna nguvu sana mikononi ila hakikisha donge lako linakuwa laini kabisa. Na kipindi unakunja mwanzo fanya iwe nyembamba sana kama karatsi, muda wa kusukuma ili uchome iwe wastani, isiwe nene sana haitaiva na isiwe nyembamba sana itakua kaukau.

Pia wakati wa kuchoma, kama umeweka chapati kwenye kikaango na haifuri jua kuna kitu umekosea, inaweza kuwa hujakanda unga vizuri au umeweka nene.

Lete maujuzi yako mpishi, unatumia njia gani kufanya chapati yako inakuwa laini?
Ukitaka upate chapati nzuri tumia unga wa azam wa SPF,na usitumie mafuta ya kula tumia yale mafuta ya kenya inaitwa prestige

Then kanda unga wako na hayo mafuta kwa muda wa dakika 10 kisha acha mchanganyiko huo kwa mda wa nusu saa mpaka saa then anza kukata vipande na pika chapati zako japo kuna wengine wanalazaga mpaka asubuh
 
Siko vizuri Sana kwenye uandishi hasa kwenye kueleza Jambo Kwa mtiririko.

Lakini,binafsi huwa ninatumia mafuta ya cowboy kukanda unga wa chapati.

Huwa Nina weka chumvi na sukari kidogo Sana,hii inaongeza ladha.

Baada ya kukanda Kwa muda usiopungua DK 20,ninafunika,Joto linasaidia pia kufanya chapati ziwe laini.

Wakati wa kusukuma matonge ili kuweka mafuta Kabla ya kukunja,huwa ninaweka mafuta na kunyunyiza unga wa ngano kidogo,kisha nakunja matonge.

Moto mdogo wakati wa kupika lakini pia mafuta mengi.

Lakini pia huwa ninaweka chapati zaidi ya 3 jikoni Kwa wakati mmoja,hii pia husaidia Joto kutoka chapati moja lisipotee,hivyo kufanya chapati kuwa laini.
Naomba kavoice note 😍🙈
 
Imani huwa inanitoka kabisa nikifika mgahawani nikute mpishi anapika chapati kwa kuziwika tatu tatu wengine mpaka 4.
Bora hata 2 ila zaidi ya hizo mara nyingi haziivi, chuma cheupee kama sanda vile.

Ni migahawa michache wanapika chapati standard, kwingine tunakulaga basi tu hamna namna na unatamani chapati.
 
Nadhani kila mtu ana utalaamu wake. Wengine wamevamia hiyo staili. Ila ungemuona mama haji namna anazipanga chapati zaidi ya nne na zinaiva vizuri kabisa zinakuwa za brown zinaiva vema kabisa.

Mama haji yupo vema sana.
 
Maandazi ndio nimefanikiwa kuelewa. Chapati za kusukuma bado bila bila [emoji23][emoji23]

Ila nitakaza mpaka mwaka uishe huu niwe nimeelewa.
View attachment 2614294View attachment 2614297

IMG_8984.jpg

Nimejaribu leo
Kesho nitapika za maji ya uvuguvugu
Leo nimetumia maji ya baridii ila sio laini sanaa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom