Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Nikiona chapati za hivi nikalinganisha na zangu najiona sina bahati

Usihangaike na mie kwenye chapati,nishajikatia tamaa [emoji1784]
Usichoke bhana,je wakati wa kukanda unga huwa unakanda na mafuta kiasi au maji tupu.
 
Siko vizuri Sana kwenye uandishi hasa kwenye kueleza Jambo Kwa mtiririko.

Lakini,binafsi huwa ninatumia mafuta ya cowboy kukanda unga wa chapati.

Huwa Nina weka chumvi na sukari kidogo Sana,hii inaongeza ladha.

Baada ya kukanda Kwa muda usiopungua DK 20,ninafunika,Joto linasaidia pia kufanya chapati ziwe laini.

Wakati wa kusukuma matonge ili kuweka mafuta Kabla ya kukunja,huwa ninaweka mafuta na kunyunyiza unga wa ngano kidogo,kisha nakunja matonge.

Moto mdogo wakati wa kupika lakini pia mafuta mengi.

Lakini pia huwa ninaweka chapati zaidi ya 3 jikoni Kwa wakati mmoja,hii pia husaidia Joto kutoka chapati moja lisipotee,hivyo kufanya chapati kuwa laini.
 
Ukitaka upate chapati nzuri tumia unga wa azam wa SPF,na usitumie mafuta ya kula tumia yale mafuta ya kenya inaitwa prestige

Then kanda unga wako na hayo mafuta kwa muda wa dakika 10 kisha acha mchanganyiko huo kwa mda wa nusu saa mpaka saa then anza kukata vipande na pika chapati zako japo kuna wengine wanalazaga mpaka asubuh
 
Naomba kavoice note πŸ˜πŸ™ˆ
 
Imani huwa inanitoka kabisa nikifika mgahawani nikute mpishi anapika chapati kwa kuziwika tatu tatu wengine mpaka 4.
Bora hata 2 ila zaidi ya hizo mara nyingi haziivi, chuma cheupee kama sanda vile.

Ni migahawa michache wanapika chapati standard, kwingine tunakulaga basi tu hamna namna na unatamani chapati.
 
Nadhani kila mtu ana utalaamu wake. Wengine wamevamia hiyo staili. Ila ungemuona mama haji namna anazipanga chapati zaidi ya nne na zinaiva vizuri kabisa zinakuwa za brown zinaiva vema kabisa.

Mama haji yupo vema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…