Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Jamani wanajamiiforums ninapokea mshahara laki tatu na nina mke na watoto wawili ninalipa kodi 30,000 kwa mwezi, kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hiyo hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niweze kubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..

Sembe robo mchana 600/=

Mchicha 1,000/= ( napika wa mchana na usiku kabisa kulinda gas)

Dagaa 500/ ( wa mchana na usiku)

Nyanya 200/=

Kitunguu 100/=

Mchele wa usiku 2,000/=

Kodi 1,000/=

Nauli 1,000/=

Total 6,400/= per day ningekua mimi ningetumia hivi mpaka wote wate wawil
tupate kazi au kipato kiongezeke

Mambo mengne yote ningejibana bana ilimradi matumizi yote yasizidi elf8 yani piga ua lakini nibakishe elf2 kwa usiku ama elf1 miatano hata kaka nile mlo mmoja tu mimi na mume wangu ama nikipika mara moja hakuna kurudia
 
Suala la kuweka akiba ni suala muhimu na zuri sana katika maisha yetu! weka asilimia 5% ya kipato chako iwe akiba yako kila mwezi. Zinazobakia...mpe mke wako 150,000/ hela ya matumizi kwa Mwezi mzima ( sifa za mwanamke ni kuhakikisha anabalance fedha hiyo kwa Mwezi mzima na itoshe) jitahidi chakula Cha familia kinunuliwe kwa ujumla, sabuni za kufua zisisahaulike, mpe nafasi mkeo atafute chochote kitu ili kuongeza Pato la familia. Inawezekana!; Baba lipa maji na umeme, lipa Kodi, hakikisha una emergency ya sh. 10,000 tu kila mwezi.
Kama kaoa mzaramo hiyo 150 itanunua vijora yote
 
Aisee, Kuna Muda inabidi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa alilokujaalia. Kuna watu hiyo 300k ni posho yake ya mawasiliano au ndio posho ya kikao cha siku mbili...

Bajeti ya 300k kwa mwezi.
Kila siku utumie 10k.
Ina maana hapo unatakiwa upige hesabu kwa siku 10k unaitumiaje?
Chakula pekee tenga 6k
Kodi tenga 1k, hapo inabaki 3k.
Chukua 1k weka akiba.
Chukua 2k ifanye nauli na contingency.
Ishi na huu ushauri 👆👆
 
Ukitaka kuishi bila stress ukipokea tu mpe mkeo hela yote hata matumizi yako akupangie yeye. Wanawake wanajua kubana na kutunza pesa
Hawa hawa wanawake wenye vikundi vya kufa na kuzikana jumlisha vikoba! Ukiwa na hasira utamtimulia mbali.
 
Hakikisha unakodi shamba ekari moja. Lima mahindi nusu eka na maharage nusu eka.
Hapo utakuwa kwanza umetatua changamoto ya misosi.
Wapigie simu ndugu zako kijijini wakutafutie shamba la kukodi.
Tuma hela ya kulimia, mbegu na mbolea.
Kwa mwaka utaweza kuokoa hadi Tsh milioni moja kwenye gharama za chakula.
Ndugu siyo wa kuamini sana, kilimo Cha simu ni kigumu kupita maelezo, siku unaenda unaomba akupeleke shamba mnatembea vizuri mnafika sehemu anakwambia shamba lilikuwa hapa sijui limeenda wapi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndugu siyo wa kuamini sana, kilimo Cha simu ni kigumu kupita maelezo, siku unaenda unaomba akupeleke shamba mnatembea vizuri mnafika sehemu anakwambia shamba lilikuwa hapa sijui limeenda wapi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah. Kama mke wake ni mama wa nyumbani, anaweza kumtuma afuatilie mambo ya shamba...
 
Laki tatu unatoboa vizuri tu na akina unaweka.....fanya hv nunua mchele kilo 15 @2200 =33000...ings kilo 10 @1300=13000 sukari kilo 1 = 2800 lipa umeme 10000 maji 5000 mafuta lita tano sh 23000 vyote hvyo jumla 86800.....inabaki sh 213200....mpe mkeo laki moja awe anapangilia mboga....inabak 113200....weka gsi mtungi mdogo wa 24000...inabak 89200.....chukua elfu 30000 weka akiba na iliyobak hapo kama 59200 fanya nauli na matumizi yako mengine kama vocha......Maisha mipango tu
 
Back
Top Bottom