Hamna majitu wa zamani! Hapo tumeshapata mifano ya kutosha ya mifupa iliyohifadhiwa tangu miaka mielfu.
Naomba usisambaze habari bila msingi. Hasa kutoka Misri kuna maiti nyingi zilizohifadhiwa (maana halihewa ni kavu kuna maiti nyingi zilizokauku tu badala ya kuoza jinsi ilivyo kawaida). Hizi mumia (mummies) za wafalme hakuna siri jinsi alivyosema hapa mwingine; maana walifunika maiti kwa chumvi na kutoa utumbo hadi imekauka vema.
Kuhusu urefu wa Wamisri wa Kale kuna utafiti wa juzi wa mchambuzi aliyepata PhD juu ya mada hii.
Karibu kusoma mwenyewe:
http://scholarcommons.usf.edu/cgi/viewcontent.cgi?article=4500&context=etd
Egyptian Body Size: A Regional and Worldwide Comparison (2011)
Alichungulia mabaki ya wati zaidi ya 1000 walioishi kati ya mwaka 5500 kabla ya Kristo hadi karne za kwanza baada ya Kristo. Picha inaonyesha urefu wa Wamisri (buluu wanume - nyekundu wanawake) na Wanubia (Sudan kaskazini). Wanaume Wamisari kwa wastani walikuwa na sentimita kati ya 160 na 170 kwa jumla. Nyakati za vita na njaa ilileta watu wafupi zaidi (maana urefu hutegemea chakula hasa protini na vitamini kwa watoto).
Hakuna dalili ya majitu (giants) hata kidogo. Wamisri wa leo ni warefu kuliko zamani maana chakula kimekuwa bora.
View attachment 677495