Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Waniulize Mimi,nimewahi kuishi kwenye utajiri wa nguvu za kishirikina na Nina Wajua watu wangu wa karibu ambao wanaishi na utajiri huo!

Lakini pia,binafsi hadi hivi Sasa Nina Wajua watu wawili (wataalamu) ambao wanatoa utajiri wa nguvu za Giza,mmoja yupo Zanzibar na Mwingine yupo Malawi!

Mkuu maisha yangu ni simulizi tosha,sema kwasababu ya wapumbavu wa hapa JF huwa naamua tu kukaa kimya maana ukibishana na mjinga yawezekana ukawa mjinga zaidi yake!

Nimewahi hadi kulala na maiti hapo Malawi ili nifanikiwe na nilifanikiwa sema ndo hivyo maisha yangu yote ya mafanikio wanawake ndo huwa kikwazo kwangu !

Mtu anakuja hapa anabisha hata hajawahi Kutembea popote zaidi ya kutoka Mbeya kuja Dar au kutoka Dar kwenda Arusha !

Sihitaji kuuliza Kwa mtu Mimi mwenyewe ndiye ushuhuda !

Kama watabisha ngoja waendelee kubisha but for now Sina muda wa kubishana na Abharisya!
Kama ni kweli basi ulipolala na maiti uliongeza kiwango cha ujasiri kilichokusaidia katika mambo mengine, Hofu huwa ni mojawapo ya kikwazo kikubwa sana katika kufanikiwa.
 
Kuna ile stori ya Chief yule - njia ya kwenda Mbeya, Tumekua tunaisikia toka Enzi za Primary.

Story za kitaa sasa, kila mtu anasema Tanesco walipitisha nguzo pale, umeme ukawa hauvuki.

Wakajaribu kuhamisha kaburi, asubuhi wakakuta limerudi palepale sababu ya uchawi wa chief, Hivyo wakavushia nyaya upande wa pili ndipo umeme ukavuka.

Kichekesho ni kwamba, Tanroads walihitaji kufanya marekebisho pale mwaka huu, hivyo wakakubaliana na familia lile kaburi lihamishiwe kijijini kwao.

Familia ikachukua vijana 10 [Walitafutizwa vijana wapambanaji wa sokoni tu], Tena halikufanyika Tambiko lolote.

Baada ya dakika 10,20,30,,, , mabaki ya mifupa ya chief yakatolewa na kupisha Tanroads waendelee na kazi.

Tanesco waliwahi kuulizwa hili suala waliwahi kusema "Tulipofika kwenye lile kaburi kwa heshima ya Chief tu, Tukaamua kuhamishia nguzo upande wa pili na sio sababu za kishirikina".

Kwahyo hata hayo mengine ni sawa na hizi Stori za kwenye kahawa tu.
 
Hapo ndio utajua kwamba hakuna utajiri wa kishetani.

Maana watu wanaodai kuna utajiri wa kishetani ukiangalia huo utajiri wao bado ni wa kiwango cha chini sana.

Hawamfikii hata Mo Dewji, Bakhressa au Dangote.

Kama mtu anadai kuna utajiri wa kishetani, Kwa nini asiutumie kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett na wengineo?

Utakuta mtu anadai kuna utajiri wa kishetani lakini maisha yake ni ya kimaskini halafu anakomaa tu kuna utajiri wa kishetani!!!

Kuutumia atajirike, hataki.

Unajua hawa waafrika hasa watanzania maskini wana mentality za kijinga sana.
Au labda utajiri wa Mo Dewji, Bakhresa na Dangote ni wa kafara pia.
Wamewezaje kuwa matajiri hivyo katika nchi masikini?!
 
Au labda utajiri wa Mo Dewji, Bakhresa na Dangote ni wa kafara pia.
Kafara zipi? Za aina gani?

Kama utajiri wa watu ungekuwa una ongezeka kwa kutoa kafara, Basi Elon musk ndio angekuwa mtoa kafara namba moja duniani.

Na ndio angekuwa binadamu wa kwanza kutoa kafara nyingi hadi kuweza kuwa tajiri namba moja duniani kwa kuwapita matajiri wengine waliomzidi kabla ya yeye kuwa namba moja.

Na ingekuwa kwamba Utajiri wa tajiri unashuka, Asipotoa kafara.

Lakini sivyo, utajiri wa matajiri unakua kutokana na kupanda na kuongezeka uzalishaji na HISA za makampuni yao na maviwanda yao.

Ingekuwa kwamba Utajiri wa matajiri wakubwa unaongezeka kwa kafara, Aliko Dangote angeweza kutoa kafara za kutosha amzidi na kumpiku Elon musk.

Lakini hakuna kitu kama hicho. Na wala utajiri hauongezeki kwa utoaji kafara.
Wamewezaje kuwa matajiri hivyo katika nchi masikini?!
Wazazi wao walikuwa matajiri wakubwa tangu mwanzoni.

Baba yake Mo Dewji alikuwa tajiri akamridhisha utajiri mwanae.

Yeye ana uendeleza tu.

Wala hakuna uchawi wala ushirikina wowote ule.
 
Mbona wengi wanamuomba na wanafanya kazi kwa bidii na uaminifu sana ila bado wanakufa wakiwa masikini??
Sio kila anayemuomba Yesu anamuomba utajiri,ila ukisimama vizuri ukamuomba atakupa,but masharti na vigezo kuzingatiwa,unataka utajiri wa nini,ili ufanyie nini,na akisha kupa mpango wake wa kumtumikia utaendelea au ndio itakuwa mwisho,ukumbuke mpk anajua huyu ukimpa atakuwa mbaya au mzuri kwa watu n.k. kwahiyo humpa amtakaye...
 
Kutafuta Uthibitisho Katika Inshu Za Mambo Ya Kiroho Inahitaji Juhudi.Kwa Mfano Mtu Anaweza Akawa Mchawi na Ni Kweli Mchawi Kweli Kweli Lakini Hauwezi Kuthibitisha Kirahisi.Mambo Ya Kiroho Ni Mambo Ya Sirini.
Kuna Siku Kwa Macho Yangu Naked Kabisa Nlishuhudia Mchawi Namuangalia Ananiangalia.Mwaka 2013 Hiyo Magomeni
Una uhakika ulikuwa macho...maana kuna wakati huwa tunajikuta tumepiliza vituo vya mabasi wakati makondakta waliuliza Nani anateremka na tulikuwa macho
 
Kuna nyumba ya tajili niliingia, sebuleni hakuna makochi wala viti ni mikeka tu, unaambiwa hatoi pesa mchana, mpaka usiku, na anatoa pesa kwa kutumia mkono wa kushoto....Sijajua kama yeye alitoa kafala au masharti ya mganga wake.
Una ambiwa na nani?

Ulimuona na kuthibitisha kwa macho yako kwamba huyo tajiri hatoi pesa mchana?

Usiseme "unaambiwa au niliambiwa" unatakiwa kusema nilishuhudia na kuthibitisha na uwe na uthibitisho kabisa.

Hizi stori za kuambiwa ambiwa, Nyingi zimejaa uongo tu.
 
Uchawi/viini macho sidhani kama huwa vinaacha ushahidi anuai wa kutolea vielelezo vya kufanyika.Those people are too clever & trickier to ones mind,hence playing a fool!
Back in the days, Europeans came to your continent, enslaved, whipped and hanged many of your forefathers and your voodoo did them nothing. Why didn't you put hex (magical spell) on them and their entire generation??
 
Ila mkuu kwa nini utajirike mwenyewe halafu ndugu zako wengine ni masikini na wanakufa vifo tata ? Halafu wakifa au wakichanganyiwa ndio utajiri wako unazidi kuongezeka
mtegemea cha ndugu hufa maskini,....NAWATOA KAFARA MKUU😂😂🤣
 
Back in the days, Europeans came to your continent, enslaved, whipped and hanged many of your forefathers and your voodoo did them nothing. Why did you put hex (magical spell) on them and their entire generation??
Wanasema uchawi wa mzungu ni mkali zaidi, Wao wamefikia Kiwango cha Freemason wanaotoa kafara kwenye level za kimataifa!
 
Unajua mambo haya yapo na uchawi upo nyie mnaokaza mafuvu siku yenu ikifika mtaamini tu.
tumeisubiri sana hiyo siku mkuu,...naona imekuwa kama kurudi kwa masihi,...maana mpaka tumeanza kuzeeka tukisubiri,...🥲🙄🙄
 
Back
Top Bottom