Kuna ile stori ya Chief yule - njia ya kwenda Mbeya, Tumekua tunaisikia toka Enzi za Primary.
Story za kitaa sasa, kila mtu anasema Tanesco walipitisha nguzo pale, umeme ukawa hauvuki.
Wakajaribu kuhamisha kaburi, asubuhi wakakuta limerudi palepale sababu ya uchawi wa chief, Hivyo wakavushia nyaya upande wa pili ndipo umeme ukavuka.
Kichekesho ni kwamba, Tanroads walihitaji kufanya marekebisho pale mwaka huu, hivyo wakakubaliana na familia lile kaburi lihamishiwe kijijini kwao.
Familia ikachukua vijana 10 [Walitafutizwa vijana wapambanaji wa sokoni tu], Tena halikufanyika Tambiko lolote.
Baada ya dakika 10,20,30,,, , mabaki ya mifupa ya chief yakatolewa na kupisha Tanroads waendelee na kazi.
Tanesco waliwahi kuulizwa hili suala waliwahi kusema "Tulipofika kwenye lile kaburi kwa heshima ya Chief tu, Tukaamua kuhamishia nguzo upande wa pili na sio sababu za kishirikina".
Kwahyo hata hayo mengine ni sawa na hizi Stori za kwenye kahawa tu.