Unawajua Wanyama wasiolea watoto wao

Unawajua Wanyama wasiolea watoto wao

Hii chai tulipigwa sana enzi hizo, ila Tanganyika kuna vi stori uchwara sana.
HIvi unajua kwanza staili ya kinyonga kuzaa ?

Kinyonga ili azae inabidi yeye kama mama afe/apoteze maisha, na ni lazima siyo hiari.

Kinyonga akiona siku za kuzaa zimefika, anapanda juu ya mti mrefu, anajirusha chini kwa nguvu anapasuka alafu ndiyo watoto wanatoka.

Hivyo ili kinyonga azae inabidi afe mama ndo watoto watoke
 
Acha ngonjera umesoma biology kweli au story za vilinge?
Kinyonga ni jamii ya reptilia kundi lao kubwa hutaga mayai
Wachache ndio huzaa na hio kupasuka haina ushahidi wowote
Huu uongo ni maarufu sana mitaani na wengi wanauamini sababu tu jamii yetu haipendi kusoma
 
Punda ukimtenganisha na mtoto wake anasusa hafanyi kazi.

Na ukitaka uone balaa lake mkamate mtoto wake mbele yake, akikufikia anakuuma vizuri tu na yale meno yake ya kukatia nyasi.
Hahaha ,
Aisee nyie jamaa mliowahi ishi na wanyama mnaburudisha.🤣🤣
 
Kuna utafiti unadai kwamba nyoka aina Cobra ndiye kiumbe mwenye sifa ya juu ya wale wasiojua kulea.
Inadaiwa baada yai la kwanza kufunguka na kichanga kutoka mama hutimua mbio.

Watafiti wamebaini kwamba akibaki eneo hilo hula vitoto vyake, hivyo huamua kuondoka eneo hilo haraka iwezekanavyo kumuepusha na tamaa ya kula wanawe.

Utafiti umebaini kwamba, vitoto vya Cobra ni nyoka hatari zaidi maana kitu pekee kinacho walinda ni sumu waliyonayo.
 
Kuna nyoka, mjusi, kinyonga hawa wakishazaa au kutaga mayai hao wanaondoka hawana Tena time na watoto wao. Sungura na panda wao watakaa kidogo na watoto labda week then wanawaacha wajitegemee. Nyani ye akiona mtoto mlegevu mlegevu anamwachia toka juu ya mti. Buibui yeye sometimes sio tu ana mu abandon mtoto ila anaweza akamla kabisa.


Wanaoongoza Kwa ku care ni simba na tembo hawa wanalinda sana watoto zao.
Simba hunifurahisha sana jinsi wanajali watoto wao, hasa watoto wale wenye afya. Huhangaika nao sana mpaka wafikie umri wa kujitegemea.
 
Kuna nyoka, mjusi, kinyonga hawa wakishazaa au kutaga mayai hao wanaondoka hawana Tena time na watoto wao. Sungura na panda wao watakaa kidogo na watoto labda week then wanawaacha wajitegemee. Nyani ye akiona mtoto mlegevu mlegevu anamwachia toka juu ya mti. Buibui yeye sometimes sio tu ana mu abandon mtoto ila anaweza akamla kabisa.


Wanaoongoza Kwa ku care ni simba na tembo hawa wanalinda sana watoto zao.
Hata cheetah , na twiga, nawengi wengi tu
 
Naona kwa sasa wanyama wanaoongoza kuwakimbia watoto ni binadam
Yaani tuna maisha ya fake kabisa kwani hatufuati nature
Ilikuwa sisi ndio tuwe na maadili na kuzingatia yetu ila tumekuwa kama KASA tu
 
Punda unamwibia mtoto kwa mbele sio kwa nyumba.
Nliendaga kupigaga mishe fulani mitaa ya ruvu ndani huko,kulikuwa na ka zoo fulani cha mtu
Kuna kijana nlikuwa naye,kumbe alichukua yai la mbuni,ebwanaa
Huo mtiti mama mtu aliyotuletewa ilikuwa si mchezo
Mpaka kugundua ikaonekana yai
Lake limechukuliwa...
Mbona yule kijana aliirudisha

Ova
 
Hawapo

Nadhani Hawapo africa.. Sana nchi zenye barafu na uchina huko wapo sana tu google mkuu mbona maarufu sana China ni kama symbol yao
Panda wanapatikana CHINA PEKE YAKE.
Huwezi wakuta popote zaidi ya China.
 
Back
Top Bottom