Unaweza kufanya Uwekezaji gani kwa Milioni 50-500 na wenye faida ya kueleweka?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Mkuu,

Kuna watu/mtu ambaye wanaohitaji kufanya uwekezaji serious?

Je unaweza kufanya nini ukiwa na access ya Kiasi cha Milioni 50-500?Uwekezaji uwe endelevu,uzalishe ajira,uhifadhi mazingira uzalishe kwa soko la nje na la ndani.

Kama una wazo zuri hapa ndo pahala pake
 
Kwa mil400 ningeweza kununua ardhi na kuweka miundombinu ya kudumu ya maji kisha nilime pilipili kichaa naingia mkataba nakuwa main supplier kwenye viwanda vya maji ya kutawanya maandamano. Hili zao likipata matunzo, mpando mmoja huwa na michumo mitatu hadi minne kwa mwaka
 
Mkuu,Milioni 400 unaweza kulima heka ngapi za pilipili?
 
Heka 50 inamaana kwa kila heka nitawekeza kama milioni 8 kwa kununua na kulima?Bei ya heka 1 inaweza kuwa shilingi ngapi?
Kwa ardhi safi ni 250,000- 500,000 kwa ardhi inayohitaji kusafishwa bei itapungua zaidi
 
Unafahamu ilipo ardhi hio?Ni hectare au ni acre?

Linalohitaji kusafishwa linaweza kugharimu kiasi gani?
 
Mkuu,
Kuna watu/mtu ambaye wanaohitaji kufanya uwekezaji serious?

Je unaweza kufanya nini ukiwa na access ya Kiasi cha Milioni 50-500?Uwekezaji uwe endelevu,uzalishe ajira,uhifadhi mazingira uzalishe kwa soko la nje na la ndani.

Kama una wazo zuri hapa ndo pahala pake
Kwa million 50- 500 najenga lodge nzuri yenye vyumba 25 kwenye miji inayochipukia. Lodge ni fixed assets ya muda mrefu
 
Kwa harakaharaka hapa kilimo endelevu mseto. Miundombinu ya kisima cha maji, bwawa, stoo ya nyasi, stoo ya pumba na mashudu, nyumba ya wafanyakazi, geto la bosi, kupanda na kuvuna malisho, ng'ombe wa maziwa, kiti moto, sales point ya baadhi ya bidhaa zako. Mbolea itumie kupanda parachichi, papai, pilipili, ndizi mzuzu, n.k. Fanya processing kidogo kutumia hizo raw materials. Orodha ni ndefu.
 
Kufanya zote au kuchagua kati ya hizo?
 
Kwa million 50- 500 najenga lodge nzuri yenye vyumba 25 kwenye miji inayochipukia. Lodge ni fixed assets ya muda mrefu
Mkuu Vyumba 25 means kila chumba cha lodge milioni 20 italipa kwelie?au cjakuelewa
 
Kawekeze pale Simba SC naona mambo si mambo kabisa kwasisi Mashabiki wake
 
Back
Top Bottom