Unaweza kula chakula alichobakiza mwajiri wako mezani?

Unaweza kula chakula alichobakiza mwajiri wako mezani?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Wakati nikiwa shule ya msingi, nilipata bahati ya kukutana na babu mmoja aliyenihadithia maisha enzi za ukoloni. Babu aliajiriwa kama mpishi wa familia ya mzungu.

Ajira ilikuja na mkataba wa kazi na alipewa nguo za kazi. Ajira hii ilikuwa ni ya J3 mpaka J’mosi. Alianza kazi 12:00 asubuhi na kumaliza saa nne. Baada ya hapo alirudi saa kumi jioni mpaka saa mbili usiku. Ajira hii ilimuwezesha kupata mkopo benki na kujenga nyumba ya vyumba sita mtaani yenye maji na umeme.

Asubuhi alitengeneza chai baada ya hapo boss na mke wake walikwenda kazini. Baada ya kusafisha vyombo vya chai alirudi nyumbani kwake mpaka saa kumi. Alirudi kutengeneza chakula cha jioni ambacho ilikuwa ni kuku, minofu ya ng’ombe au samaki wa kuoka na mboga mboga. Hapa ndiyo alinieleza kuwa, mzungu alikula kwa uma na kisu hivyo kuku au samaki alibaki na minofu mingi tu na alikuwa anamalizia kula jikoni.

Niliwaza hivi huyu mzungu alimchukuliaje mtu anaekula mabaki yake ya mezani!
 
Maisha ya zamani yalikuwa magumu sana aiseee! Enzi hizo hakuna chai wala kula chips....ni ugali maharage tena yasiyoungwa au mboga za majani chukuchuku! Ni sahihi huyo mzee kula hivyo vitu.

NB: Nazungumzia ile mikoa ambayo hakuna ziwa wala bahari, halafu ni ukame na njaa i.e Dodoma ya enzi hizo!
 
Kama boss ni wa kike, nakula vizuri sanaa tena akikaa vibaya sio chakula tu hata na yeye namtafuna.



Let's meet at the top, cheers [emoji482]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
tatizo huwa mtazamo tu.

hata kuona nisahihi paka kula ukichobakiza kwa mwingine inawezakuwa tatizo.
 
Ninaweza kula walichobakiza wanangu kwenye sahani basi.
 
Kipindi barehe inaniwaka moto,kulikuwa na Toto moja hivi yakike niliielewa siambiliki.. she was so hot and lovely kindy and cute (mpk nimeandika kiingeleza jueni komamanga wa watu nilidata nikadatika!)

Lkn sio siri mtaani tulipata tabu.. siku moja ilikuwa sikukuu ya x max toto la watu likaja home akapakuliwa akala then akabakiza na kijiko chake vilevile kile chakula kikawa kimewekwa mahali tu maana hapo kila mtu alikuwa bize kutaka kutoka kasoro mimi.

Sasa wengine wakawa wameshaondoka komamanga nikabaki pekee hapo nikazama jikoni nikavuta ule upilau aliobakiza mrembo yule na kwa hasira ya udomo zege nikagumia kijiko kilekile alichokuwa akitumia! Wala sikuona hatari na hapo ndo nikaelewa kipendacho roho hula hata nyama mbichi..😂

Popote ulipo wewe dada jua nilikupendaga sijapata kuona! Tatizo udomo zege wangu na wenyewe umekaa Kama kinyeramumo tu!😂
 
Kipindi barehe inaniwaka moto,kulikuwa na Toto moja hivi yakike niliielewa siambiliki.. she was so hot and lovely kindy and cute (mpk nimeandika kiingeleza jueni komamanga wa watu nilidata nikadatika!)
Lkn sio siri mtaani tulipata tabu.. siku moja ilikuwa sikukuu ya x max toto la watu likaja home akapakuliwa akala then akabakiza na kijiko chake vilevile kile chakula kikawa kimewekwa mahali tu maana hapo kila mtu alikuwa bize kutaka kutoka kasoro mimi.. Sasa wengine wakawa wameshaondoka komamanga nikabaki pekee hapo nikazama jikoni nikavuta ule upilau aliobakiza mrembo yule na kwa hasira ya udomo zege nikagumia kijiko kilekile alichokuwa akitumia! Wala sikuona hatari na hapo ndo nikaelewa kipendacho roho hula hata nyama mbichi..😂

Popote ulipo wewe dada jua nilikupendaga sijapata kuona! Tatizo udomo zege wangu na wenyewe umekaa Kama kinyeramumo tu!😂
😂😂😂
 
Wakati nikiwa shule ya msingi, nilipata bahati ya kukutana na babu mmoja aliyenihadithia maisha enzi za ukoloni. Babu aliajiriwa kama mpishi wa familia ya mzungu.

Ajira ilikuja na mkataba wa kazi na alipewa nguo za kazi. Ajira hii ilikuwa ni ya J3 mpaka J’mosi. Alianza kazi 12:00 asubuhi na kumaliza saa nne. Baada ya hapo alirudi saa kumi jioni mpaka saa mbili usiku. Ajira hii ilimuwezesha kupata mkopo benki na kujenga nyumba ya vyumba sita mtaani yenye maji na umeme.

Asubuhi alitengeneza chai baada ya hapo boss na mke wake walikwenda kazini. Baada ya kusafisha vyombo vya chai alirudi nyumbani kwake mpaka saa kumi. Alirudi kutengeneza chakula cha jioni ambacho ilikuwa ni kuku, minofu ya ng’ombe au samaki wa kuoka na mboga mboga. Hapa ndiyo alinieleza kuwa, mzungu alikula kwa uma na kisu hivyo kuku au samaki alibaki na minofu mingi tu na alikuwa anamalizia kula jikoni.

Niliwaza hivi huyu mzungu alimchukuliaje mtu anaekula mabaki yake ya mezani!
Dah,ugumu wa maisha husababisha MTU kufanya chochote ikiwa hata kudhalilisha utu wake.

Ni kama viongozi wa polisi (Afande Mroto) alituambia Mbowe kutekwa na kupigwa badae baada ya bosi kula na kushiba Afande alikuja na makombo ya Boss eti alijiangukia ,
Kweli sometimes ajira ni utumwa
 
Back
Top Bottom