Unaweza kurudisha Muamala wa Fedha iliyotumwa kimakosa kwenye akaunti yako ukiwa umefulia mbaya?

Unaweza kurudisha Muamala wa Fedha iliyotumwa kimakosa kwenye akaunti yako ukiwa umefulia mbaya?

Mimi sitaitoa wala sitairudisha nitakuomba uwasiliane na mtoa huduma wako kama ni mtandao wa simu au benki ili wao ndiyo wanipigie..unaweza ukatuma ukashangaa umewapa watu access kwenye account yako na kila siku ukawa unaibiw...
 
Kwa hakika inahitaji Roho ngumu sanaaa kula pesa ya mtu, maana Kama hayajawahi kukutokea unaweza hisi ni maigizo lakini pia inategemeana hiyo Pesa imekukuta ukiwa katika situation gani maana unaweza kuta imekuja hauna hata 100 afu upo na vijishida Kama vyote hapo ni naweza kugawa ubinadam😀😀 ili twende sawa, maana inaweza kuwa Mungu akawa ameamua kukutoa au kukutatulia changamoto kwa style hiyo.......
 
Pesa au Mali ya watu lazima nirudishe.
Niwape ushuhuda wangu.
Miaka kama miwili nyuma nilipokea muamala kutoka Safaricom kama laki na vipoint.
Nilimtafuta aliyetuma bila mafanikio na hapo nimenunua Bando la kimataifa 5000tsh kama dk 5 na meseji chini ya 12.
Niliwasiliana na Safaricom na Vodacom mpaka tukafanikiwa.
Yule mama mtu mzima alikuwa anamtumia mjukuu wake aliyekuwa anasoma Tanga alinishukuru na alifurahi kupita kawaida.
Funzo.
Usiwahi kuhisi mtu kukosea kutuma pesa ni Mungu amemtuma.ni ajali na lazima uhusike kuonyesha kuwa Si Mali yako na kwamba utatumia gharama mpaka uhakikishe umemrudishia mtu mali yake.yule mama alisema "kijana wangu ubarikiwe na Mungu,Siamini kama Dunia hii Kuna watu wenye moyo kama wewe tena kijana walahi."
Siku ukidondosha Hela ya matibabu alafu mtu akakufia Kwa kukosa huduma, au mtu akakurudishia mwishoooni ukanisuru maisha ndo utaelewa utu ni Nini.
 
Hii hali imewahi kunitokea mara 3 na zote nimepigwa ! Mara ya kwanza alipokea kijana nikamfahamisha nimekosea nimetuma pesa kimakosa , akanijibu ngoja aangalie, baadaye nilipompigia akanijibu ni kweli ila ameitoa na kaitumia akipata atanirudishia !! Nikamjibu sawa ila isimuumize kichwa akiona ni haki yangu anirudishie lkn akiona ni haki yake sina KINYONGO.

Mwingine nilikosea yy hakutaka hata kupokea simu yangu. Nikamuandikia sms kuwa ni fedha kwa ajili ya mgonjwa hakujibu.

Mwingine nilipokosea nikamjulisha yule niliyekuwa namtumia nikampa namba ya simu , alipopiga AKAOGA matusi nikawasiliana na VODA nikapewa jibu Jamaa kesha itoa .

Live nikiwa natembea barabarani nikaiona 5,000/= nikaiokota, halafu nikahisi yawezekana ni ya hawa vijana wanaouza miwa barabarani wakati nataka kwenda kuwauliza kijanja.

Nikamuona jamaa mbele yangu kwa mbali anajipekuapekua , nilipomsogelea nikamuuliza vp, akajibu nimepoteza fedha nikamuuliza shilingi ngapi?

Akajibu 5,000/= nikamwambia haya hii hapa basi tukaendelea kupiga stori nikamwambia kwangu mm ni ngumu ssna kula fedha kama hiyo yaani sitapata AMANI ya moyo kabisaa
Endelea na moyo huo.mara nyingi matokeo ya tabia hizi uenda Kwa vizazi vyetu vijavyo.watu waaminifu.
 
Mimi nimesharudisha mara kadhaa ila kuna mmoja sijarudisha mpaka leo na mhusika namjua.

Ilikuwa hivi, kuna mtumishi mmoja aliazima laini yangu ya voda akaweke hela 2000 ili aunge bundle la intaneti maana mimi nilikuwa na modem ya voda.
Alipoenda wakati anarudi akaniitia pembeni akasema braza tuongee kwanza.

Ile kumsikiliza akaniambia wakala amekosea ameweka 20,000 badala ya 2000 kwa hiyo nitoe hiyo hela tugawane. Nikamwungia bundle lake halafu nikamwambia dogo mwenyewe aliyemhudumia ni mfanyakazi tu yule itakuwa hasara kwake au atalipishwa, kamwambie akancel muamala. Jamaa akaona mimi bonge la mjinga akawa anaongea peke yake ananung'unika, nikaachana naye.

Siku ya pili ilikuwa tarehe 22 nilikuwa na safari ya kukaa miezi miwili nje ya mkoa so nikamwachia laini.
Baada ya kurudi namwulizia laini anasema ashapoteza, ikabidi ni-renew. Kucheki salio bado lipo, sasa nikaona kwenda kumwambia dogo anaweza kuona mimi nataka kumtapeli nikampotezea mpaka leo toka tarehe 22 julai 2021.
 
Chukulia umekata ringi balaa halafu mtu kajichanganya katuma fedha kwako iwe kwenye akaunti ya Benki au Simu halafu akaomba urudishe, utatuma hiyo hela?

Uaminifu ni kitu kizuri na kingine kwa imani yangu itakuwa nakula pesa ambayo si halali yangu na ni deni ambalo kama sitolilipa hapa duniani basi siku ya hukumu nitalipia kwa thawabu zangu (AND TRUST ME HAKUNA ANAYEOMBEA HILI LIMKUTE) kwa hofu ya Allah (the almighty) ningeirudisha licha ya nafsi yangu kunianbia tofauti.
 
Chukulia umekata ringi balaa halafu mtu kajichanganya katuma fedha kwako iwe kwenye akaunti ya Benki au Simu halafu akaomba urudishe, utatuma hiyo hela?

The Drowning Man

A fellow was stuck on his rooftop in a flood. He was praying to God for help.

Soon a man in a rowboat came by and the fellow shouted to the man on the roof, “Jump in, I can save you.”

The stranded fellow shouted back, “No, it’s OK, I’m praying to God and he is going to save me.”

So the rowboat went on.

Then a motorboat came by. “The fellow in the motorboat shouted, “Jump in, I can save you.”

To this the stranded man said, “No thanks, I’m praying to God and he is going to save me. I have faith.”

So the motorboat went on.

Then a helicopter came by and the pilot shouted down, “Grab this rope and I will lift you to safety.”

To this the stranded man again replied, “No thanks, I’m praying to God and he is going to save me. I have faith.”

So the helicopter reluctantly flew away.

Soon the water rose above the rooftop and the man drowned. He went to Heaven. He finally got his chance to discuss this whole situation with God, at which point he exclaimed, “I had faith in you but you didn’t save me, you let me drown. I don’t understand why!”

To this God replied, “I sent you a rowboat and a motorboat and a helicopter, what more did you expect?”
 
Kuna dada alikoseaga kutuma muamala nikautoa nikajinunulia nguo ikapita kama siku mbili akapiga nikamwambia nimeitumia alilalamika sana nikamwambia kama anaweza asamehe tu maana nimenunua nguo alafu kali nikamtumia picha za nguo ye mwenyewe akasema ni nzuri basi ikaisha hivyo tukaendelea kuwasiliana kila siku anaomba nimtumie ile hela namwambia sina mpaka akachoka akakata mawasiliano
 
Kuna dada alikoseaga kutuma muamala nikautoa nikajinunulia nguo ikapita kama siku mbili akapiga nikamwambia nimeitumia alilalamika sana nikamwambia kama anaweza asamehe tu maana nimenunua nguo alafu kali nikamtumia picha za nguo ye mwenyewe akasema ni nzuri basi ikaisha hivyo tukaendelea kuwasiliana kila siku anaomba nimtumie ile hela namwambia sina mpaka akachoka akakata mawasiliano
Sasa nguo zimekusaidia nini? Kama alikuwa anatuma kwa mgonjwa alafu kwa wewe kununua nguo zako yeye akafa inakusaidia nini? Kwani hukuwa na bajeti ya kununua nguo mpaka mtu akosee? Nawe unaona fahari kabisa kuandika mbele za watu kuwa ulinunulia nguo kali? Shwain wewe.
 
Mi narudisha hata mtu akikosea akatuma shilingi 500 au hata Bilioni. Kwangu pesa haina thamani kama utu. Kuna watu niliwashangaa sana. Kuna mmoja nilikosea kutuma pesa kwenye simu ili ninunue vocha kwa app za kibenki nikamtumia yeye. 2000 tu ikamtoa imani na mwingine tena mtu mzima tu nilikosea baada ya kutuma kwa wife 3000 ikaenda kwake. Niliwashangaa sana.
 
Kiukweli ikiwa chini ya laki na nusu inarudi mda huo huo tofauti na hapo utanisamehe
 
Sasa nguo zimekusaidia nini? Kama alikuwa anatuma kwa mgonjwa alafu kwa wewe kununua nguo zako yeye akafa inakusaidia nini? Kwani hukuwa na bajeti ya kununua nguo mpaka mtu akosee? Nawe unaona fahari kabisa kuandika mbele za watu kuwa ulinunulia nguo kali? Shwain wewe.
Shwaini mama ako mzazi angesema kama zinakwenda kwa mgonjwa zaidi alikua anaomba nirudishe na kiondacho kwa mganga hakirudi naona umeumia sana mimi kununua nguo 😂😂😂 wivu utakufanya ufe vibaya.

Alafu acha tabia za kifukara nguo hazinaga bajeti
 
Chukulia umekata ringi balaa halafu mtu kajichanganya katuma fedha kwako iwe kwenye akaunti ya Benki au Simu halafu akaomba urudishe, utatuma hiyo hela?

Kuombana kurudishiana pesa kwa kutuma miamala kimakosa ni njia wanazotumia scammers ama kwa jina jingine matapeli.
Kila mtandao walishaelekeza njia za kufanya pindi utumapo fedha zako kimakosa na si kuhangaika na zilikoenda kuingia.
Kwanza namba unayoitumia yaweza kuwa imefungwa haipo hewani kwa muda huo, pili namba ya mtumiaji huyo yaweza kuwa na deni, kuweza kukata automatic.

Mi niliwahi kukosea kutuma, cha kwanza nilichokifanya ni kublock muamala na ndipo nikampigia jamaa, na bahati akawa hewani akanijibu mbofu mbofu nikaachana naye.
 
Mimi niliwahi kukosea no,pesa ikaenda sehemu nyingine,nika mpigia jamaa akasema nakutumia kesho asubuhi ili nijilizishe,kama hatatokea mwingine wa kunipigia,nikaandika maumivu lakini jamaa alikua mwema sana kweri alinitumia.

Tangu siku hiyo akawa lafiki yangu,badae nika muuliza aliwezaje kuludisha? Akasema asingeweza kula pesa ambayo sio jasho lake pia labda pesa ilikua inaenda kwa mgonjwa ili akapate matibabu,jamaa anaishi ukerewe Mungu ampe maisha malefu.
Watu wanatakiwa kuishi kama huyu hapa.
 
Tuko tofauti ila mimi kusema ukweli hela ambayo si jasho langu ni nuksi tu.
Narudisha mapema tu huwezi jua labda ilikuwa inaenda kwa mtu amekosa chakula, au mgonjwa.

Uaminifu unalipa kuna wana kibao wametoboa life kwa uaminifu tu.
 
Back
Top Bottom