Unaweza soma Degree Huku ukiwa Kazini

Corse ni nayotaka kupiga ni shipping and Logistics Transport
 
Okay thanks ngoja niguatilie mkuu
 
Kama upo mjini na kuna vyuo soma evening class kama upo mbali na mjini soma OPEN UNIVERSITY
 
Vyuo vyote dar vina evening classes mchawi pesa tu.
Unauliza kusoma Dar nilidhani upo kitopeni huko.
Mda wa masomo wengi uanza saa kumi hadi saa mbili usiku na Sio lazima Kila siku uingie darasani.
 
Kozi za shipping labda chuo Cha bandari temeke vingine vina procurement and logistics shipping ikiwa ndani yake.
 
Vipo vingi ila inategemea na mkoa ulipo, mfano CBE Ina evening class, unatakiwa kuomba ruhusa kazini yakutoka mapema na umbali wa kituo Cha kazi na chuo pia unamata muda utaoomba kuwa unatoka kazini, siku za mitihani unakuwa unachukua likizo ila muda mwingine unatoka kazini mapema kuwahi mitihani, ratiba za maisha yako zitabadilika ni kazi na shule hivyo hutapata muda wa kupumzika, kazi yako itakusaidia kupata walimu wa tuition kwa Yale masomo magumu.
 
Unawaandikia barua ya kuomba ruhusa ya kwenda masomo. Utapewa ruhusa, utakwenda zako kusoma, na mshahara utakuwa unalipwa huku ukiendelea na masomo.
 
Walivyo maliza Diploma waliendelea na Bachelor Na Open University au kivipi
Maana Mimi Nina Diploma nataka kujiendeleza Bachelor na nipo Job so
Unaweza nambia hao jamaa hakuna changamoto walizo PATA zozote
Plz mkuu naomba ufafanuzi zaidi
Yani jamaa walipata ajira kwa sifa ya cheti ya kidato cha nne, baada ya muda kidogo waliji organise tu wakaenda OU wakapewa muongozo kila mtu alichagua alichoona anamudu na kwa wakati wake akaanza mafunzo.

Kiukweli walikuwa serious na walikomaa sana fikiria tokea Certificate hadi ufike Bachelor degree ni safari ndefu.

Baadae walipeleka vyeti vyao mahali husika taratibu zikafanyika.
 
kabisa ya mtandaoni ndo nzuri
 
Na mda wa Kuwa Darasani au wa Masomo unaruhusiwa kutoka kazin kwenda class au hapo inakuaje mkuu kuhusu Kusoma na Kwenda kazin
Samahan unaweza nifafanulia kidogo
Ukiwa serikalini unapewa ruhusa, hivyo inakuwa shule muda wote, na kazini ikibidi ni wakati wa likizo. Taasisi binafsi, ongea nao uone kama Wana utaratibu huo, au wa kukuweka likizo bila malipo n.k.
Ikishindikana, jaribu chuo kikuu huria au online.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…