Unawezaje kumsamehe mwanaume aliyekusaliti kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani mnakoishi?

Unawezaje kumsamehe mwanaume aliyekusaliti kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani mnakoishi?

Evidence zinatosha kabisa nyingine sijazisema tu na mbaya zaidi siku nimefika tu huyo mwanamke siku kama ya 3 alikuja Akanikuta nje ya nyumba napika huku nimevaa shati la bwanaetu niseme . Aliponiona alishtuka sana kaniangaliaaaaa hajasema kitu akaondoka .

"Aliponiona alishtuka!"

Kuna uwezekano mumeo kashampiga chini, otherwise asingekuja wakati upo...

Kuna uwezekano pia, alishakuwa huru sana na mumeo na sasa ametaka kuwa huru na hapo kwenu...

Pia kuna uwezekano kwa akili zenu wadada/wanawake, alikuja makusudi ili tu umuone, ujue huyo ndio bi mdogo 😥

Again, tafuta kujua kwa nini mumeo ameleta mbususu ya kando home kwenu...
 
Yani Najikuta nakosa raha kabisa. .hata sina hisia nae kabisa sikuhizi
Hilo sasa ni pepo lililoingia kwako kupitia mlango wa uzinzi aliofanya mumeo! Lengo la hilo pepo ni kuharibu urafiki wako na Yesu! Urafiki wenu ukishaharibika hapo kila kitu kitakuwa kimekwisha! Utapoteza furaha,utapoteza amani, utapoteza upendo, utapoteza mali na zaidi ya yote utapoteza ufalme wa Mungu! Muombe Mungu akusaidie kusamehe na kusahau!
 
Habari za weekend wanajamvi!

Unawezaje kusamehe kirahisi mwanaume aliyecheat tena kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani mnakoishi!! ???!!!

Ni mumeo wa ndoa na mna watoto. Katika harakati za kutafuta pesa ulisafiri kwa muda fulani ndipo alipotumia mwanya huo kufanya aliyofanya.

Uliporudi ukakutana nahizo habari! Na badae mwenyewe kukiri kabisa kufanya kitendo hiko eti hatarudia tena! Inauma sana. Kama wewe utafanyeje hapo!!?? Binafsi sijui hata nifanye nini tangu atubu sijamjibu chochote nipo kimyaa ila naumia sanaaaa!
View attachment 2024934
Polee sanaa mama natambua inauma [emoji26] ila nakushauri umsamehe muendelee na ndoa yenu madam amekiri kuwa ametenda na amelitambua kosa na kuomba msamaha ,,,,, tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu tuna genetic material ya Mungu na Mungu usamehee wetu usamehee na kusahau iweje ww usisamehe na kuachilia lipite
 
Kuna baadhi yetu wanaume ni wapumbavu sana,unapeleka malaya nyumbani?kabisa unakoishi na mke na watoto unaokota mwanamke unaenda kulala nae humo?na anadhihirisha upumbavu wake wa kukiri kufanya hayo!

Ni pombe au kitu gani!!!
Sina hakika kama uyo jamaa ni mwanaume.

Mwanaume wa kweli hawezi kufanya alichofanya jamaa, Hawezi kuokota malaya akampeleka kulala kitanda anacholala mkewe.

Mwanaume wa kweli hawezi kukiri ukweli Hata kama anajua mkewe ameshagundua, kihisia unapokiri ukweli mbele ya Mwanamke wako Kule kukiri kwako kutamtesa Sana, hisia zake juu Yako zitapungua Sana.

Jamaa alikosea Sana kukiri kuchepuka makosa kama haya hufanywa na vijana sio mwanaume aliyekamilika.
 
Polee sanaa mama natambua inauma [emoji26] ila nakushauri umsamehe muendelee na ndoa yenu madam amekiri kuwa ametenda na amelitambua kosa na kuomba msamaha ,,,,, tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu tuna genetic material ya Mungu na Mungu usamehee wetu usamehee na kusahau iweje ww usisamehe na kuachilia lipite
Shida sio kumsamehe, Atamsamehe vizuri.

Tatizo hana hisia nae tena, afanye nini hisia zirudi juu ya mumewe? Hilo ni Tatizo zaidi.

A nahitaji kusaidiwa Kwa hili.
 
Back
Top Bottom