Mpaka unamuoa ulishindwa kumjua kua ana kiburi na umteme kabla haujajicommit kwake!? Jengeni tabia ya kuchunguzana na kujipa mda kabla hamjafanya maamuzi magumu ya kuishi pamoja.
Kuna vitabia vya mwanamke lazima utavijua tu hata aigize vipi kabla ya ndoa. Wazungu huziita "Red Flags". Hizo ukiziona inatakiwa uweke hisia pembeni upambane na uhalisia sasa kama mwanaume na ku-abort mission ya ndoa haraka.
Haya turudi ktk mada yako. Hakuna mbinu ya kuishi na mwanamke mwenye kiburi zaidi ya kuachana nae. Mwanamke mwenye kiburi maana yake hakuheshimu huyo. Sasa ya nini kugandana na jitu ambalo halikuheshimu. Utaishi kwa stress na utakufa mapema.
Unaweza sema utamnyoosha tabia kwa kumfanyia hivi ukashangaa na yeye ana mipango ya kukunyoosha zaidi. Wanaume wanahitaji mwanamke anaemuheshimu tu, vitu vingine ni ziada.