Unayependa kumiliki silaha angalia hili tukio kisha jiulize unaweza kuwa mvumilivu?

Yes Conrad na Mlay.
Kuna kipindi fulani ila muda kidogo tulikuwa tumekaa pale uhr peak bar tunapiga maji!
Kuna mida fulani alikuja mama mmoja akashuka
Kwenye gari akaja wangu wangu...pale
Alitoa Bomba alipiga nia yake ilikuwa ampige kidem fulani pale kalikuw kahudumu inasemekana alikuwa anachepuka na mme wake
Alimkosakosa risasi ya tako...yule mhudumu alitoka nduki alipotea na kupotea...
Disi wenyew pale kila mtu alikimbilia anapojua yeye...
Mambo ya silaha hayafai kabisa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ushamba mwingine ni mzigo. Kwa kuwa kwako ni gharama sana na shida kuwa na kitu fulani haimaanishi kuwa nacho ni ukichaa. Kule kwao unaenda dukani kununua aina ya bunduki unayo itaka. Kama ni basola unakuwa nazo 4 kutokana na matumizi yake na uwezo wa kuibeba.
Zipo ndogo tu za wanawake kubebea kwenye mikoba. Zipo za kiume za kubebea ndani ya suti.
Zipo bunduki za kudungulia, zipo za kuwindia. Rafiki yangu anazo 8 za aina tofauti. Nyiye ndio mnashangaa mtu kununua magari 4 tofauti kumbe kila moja lina kazi yake na wakati wake wa kulitumia.
Hapo kichaa ni yule mama kwani mumewe alimwambia tukimbie yeye kajiona kidume mbele ya risasi. Kuna kitu inaitwa"Provoking" ndiyo iliyotokea hapo. Jamaa alishindwa kuwavumilia
 
bunduki 8 kwa matumizi tofauti!! [emoji23][emoji23], subiri aje kukugonga kichwa na smg ndio utajua zote kazi yake ilikuwa moja tu, kama alivyofanya huyo mgonjwa wa akili kwenye video.

wewe ni miongoni mwa watanzania wachache wanaoamini silaha ni ufahari kuwa nayo,ona huyo mpuuzi kazifuga ndani anapigia picha kila siku, leo kaona azitumie kupigia mwanamke anayemchamba.

halafu sio kila mtu hana uwezo wa kununua silaha nyingi, za nini???
 
Soma taratibu maelezo yangu. Kila silaha imetengenezwa kwa matumizi fulani japo mlengwa n imwanadaaaaaamu. Hivi wajua.Kifaru kazi yakeni kumuua askari mwenda kwamiguu? Infantry??? Hivi wajua piandege ya vita kazi yakeni kumuua huyo huyo infantry??
Nimekuambia kuna bastola zinazobebwa na wanawake na kuna bastola za wanaume.Zote kuulia watu. Kazi ya bastola ni kuulia mtu sio kuwindia.
 

Kabisa kumiliki chuma labda uwe unakaa nje ya mji huko kwa jili ya kujilinda au ni Dereva mtu wa masafa marefu unakuwa na mzigo wa maana wa transit kwahiyo ni kwa ajili ya kujilinda na vibaka ila kama unaishi tu hapa town na una hasira kama mkizi basi haifai kumiliki BOMBA.
 
Daaah...yani wazungu walishaona bunduki ni kama manati tu...yani mtu anasikia kwa jirani zinaitika alafu baada ya dakika chache anaenda kuuliza eti “…ARE YOU OK?…” lakini kwakweli watu wanaomiliki hizi manati za kizungu huwa wajiamini kiasi cha kuhisi hata ushirikina wanaweza kuungamiza kwa manati zao
 
ndio sababu nikakwambia silaha sio sawa na yard ya magari, kwamba utanunua kila moja na kazi yake. huku sana mtu akiwa nazo ni mbili tu, usalama wake (pistol) na ya kuwindia shortgun nk.

hao vichaa wenye mpaka vifaru kwao wana nia gani kama sio matatizo ya akili!!! ndio haya sasa unagombana na wenzako bar unafata grenade nyumbani, simply huwa ipo tu haitumiki.
 
RIP kwa hawa couple. Inasikitisha sana japo pia marehemu nao walitakiwa watizame usalama wao.Unaona mtu kaja na silaha bado unazidi mjaza hasira na kumuambia jaribu.

Tukirudi kwenye umiliki wa silaha ,ndiyo maana kuna nchi kama Tanzania zinajitahidi katika kuhakikiasha wanaoomba kumiliki kweli wanastahili. Umiliki wa silaha kwanza ulazima wa muombaji ni upi, akili kichwani maana ukimpa kichaa kama huyu mzungu ni balaa. Pia silaha ndogo ambazo siyo nzito au za kivita (AK47). Silaha kama silaha haina madhara ,madhara ni mtumiaji wake. Shida ya silaha kwanza utunzaji wake maana usipokuwa makini hata wewe mwenuewe inaweza kukudhuru, utulivu wa kichwa chako hasa unapokuwa umechokozwa kutofikiria kuitumia au unapokuwa umelewa.Wenzetu Marekani sheria zao ndizo zinazowaletea shida mtu anamiliki AK47 ya nini! Tena unakuta unafanya maombi ndani ya saa tu unapewa mzigo wako na marisasi kibao.
 

Hao jamaa hapo juu siyo wanajeshi au askali kanzu labda ila ni raia wamebeba silaha nzito za kivita wakiwa kwenye viunga vya mitaa huko Marekani tena ni siku moja kabla ya kuapishwa ndg Joseph Biden.

Nashukuru kwa komenti yako inadhihirisha kweli kuwa si kila mtu anastahili kumiliki hiki chombo, maana umiliki wa panga, rungu nk ni tofauti na silaha hizi tunazozungumzia.
 
Kwenye suala la umiliki wa silaha US wameonyesha ujinga wa hali ya juu. Bowling for Columbine.
 
Ujinga upi mkuu?
Kuruhusu watu kumiliki silaha kama vile ni kifaa cha kurekebisha vitu nyumbani eti kisa sheria zina ruhusu. Kwenye hili documentary bowling for columbine lilipigiwa kelele sana hilo suala.
 
Mambo ya kawaida,kwa sababu gari zinapata ajari na kuua,ndio tusinunue ndinga?!!!wewe ulisikia wapi?!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu watu wa mataifa makubwa hasa America wana stress sana
Hata Tanzania stress ipo sana. Lakini watu watapigana ngumi, yataisha. Nchi ambayo unanunua chuma (bastola, bunduki kali) kama mtu unanunua pipi, mtu akiwa na hasira ni rahisi sana kuua mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…