Unayoyajua na usiyoyajua kuhusu wanyama wa kufugwa

Wakuu
Tumekuwa tukifuga sana wanyama majumbani mwetu kwa miaka mingi hasa jamii za kiafrika.
Ingawaje tumekuwa tukiwatendea unyama uhuni wanyama tuwafugao.

Hapa nitaeleza kwa ufupi niliyoyajua na kuyaona kwa wanyama wa nyumbani hasa wafugwao na tabia zao ambazo ni very rare kuziona ..!

PUNDA.
Kwanza huyu hafugwi. Ndiyo HAFUGIKI. Why? Twende taratibu.
Panda amekuwa akifugwa kwa muda mrefu sana na binadamu
Akitumika kwa shughuli mbalimbali kama kulima.na kubeba mizigo mbalimbali.

Ingawaje kuna tabia zake ambazo ni rare sana kuziona utazijua tu punde ukimtendea vizuri yaani usiwe mkatili kwake.

Kwanza ana akili kuliko ng'ombe na wanyama wengine

Kuna kipindi wakati nipo mdogo kijijini kwetu Punda wetu baada ya kuona kazi nyingi sana mtindo mmoja na viboko vingi sana
Akaona bhana eeh! Chakufia nini? Akasepa zake kama miezi miwili hatumuoni.

Kumbe alikuwa kaenda tu nyumba nyengine usiku karuka zizi kaingia kukaa na ng'ombe katulia!
Mwenye mifugo kaamka asubuhi wala hajauliza sanaaa. Kampa chakula kidogo then kamuacha maana anajua wazi kabisa ukimpa kazi nyingi huyo punda anasepa zakeee..!

Baada ya miezi miwili usiku tena punda yule akarudi maskani kwa mtindo ule ule wa kuruka zizi asubuhi mnamkuta katulia zake ...!

Alipokuwa na ujauzito tulitegemea atazaa tu vizuri guess what??
Tuliona tu punda karudi kutokea porini hana tumbo kubwa tena na hana mtoto! Kamuacha wapi??

Ikabidi wazee wamzunguke na kuanza kumtandika viboko mfululizo mpaka punda yule alipoenda kuonesha alipomuacha mtoto ambapo tungechelewa tungekufa kajifia zake.

Najua unajua au hujui lakini punda anakula sana ukoko ukitaka ahamie kwako mazima mpe kila siku!

Next time nilipokuwa nimekaa tu kariba na zizi nikaona punda wetu mwengine aliyekuwa na mimba , anahangaika sana yaani hatulii !

Ukweli mimi yule punda alinipenda sana na hata nikiwa nimetulia alikuwa akinifuata na kuanza kusugua shingo yake miguuni mwangu , it was my best friend..!

Akanifuata mbio mbio then anageuka ananionesha mbususu yake, nikajua moja moja kwa huyu punda anataka kusaidiwa kujifungua na mimi bwana mdogo sikujua how to do it, ikabidi niwaite wajuzi waje kumsaidia mtoto atoke.. kwa kweli nilishuhudia namna wanyama wakizaa ni tabu tupu wanapata..!

Unatakiwa ujue kuwa punda ni mchungaji mzuri wa mifugo hasa ng'ombe na mbuzi, anaongoza njia na kuwaelekeza pa kupita mifugo sababu anakariri sana njia.

Pia anafukuza sana wanyama pori hasa fisi wanaokamata mbuzi [shughuli yake wanaijua vizuri]

NG'OMBE..

Huyu ni mnyama ambaye tuseme anashika nafasi ya pili kwa kuchinjwa akiongozwa na nguruwe!

Ng'ombe ni mnyama ambaye yuko so friendly na binadamu.
Iwapo tu ukimpenda na kumjali sio kila mara viboko noo

Kwa wasukuma.ni kawaida kukuta ng'ombe mmoja kavunjika pembe kwa viboko

Ng'ombe hawezi kujifungua mwenyewe au akiweza atazaa kwa tabu sana au ndama kufa!

Kama akikuozea sana atakufuata then atakeukia kukuonesha "bwana eeh mwanangu anataka kutoka nisaidie" then utatakiwa kumsaidia kumvuta ndama atoke [hili nimeshuhudia personal]

Watu wa dar kuleni nyama tu hivi hivi tu lakini mngejua namna wafugaji wanavyopata tabu.

Ndama anapotoka inatakiwa mmoja anyonye haraka kwenye pua'mdomo' maskio ili ndama asife otherwise mtampoteza..!

MBUZI
Huyu yeye anafugwa sana sana kwa kitoweo au biashara unakuta mtu kakwama anauza chap mbuzi mmoja kama 70k kutatua kamzozo fulani.

Mbuzi yeye ni muoga sana Hali inayopelekea kuwa na akili
Mara nyingi mbuzi hukaa zizini na mifugo mingine ili kusudi kutoa alert iwapo litatokea tatizo mfano fisi ameingia zizini ama lah
Yeye akiona tu labda kondoo amedakwa na fisi [fisi anapenda kondoo kuliko mbuzi] basi atapiga yowe "jamani baba mwenye nyumba eeh huku kuna muujiza tumevamiwa"

Na kikawaida mbuzi ana Saudi tofauti tofauti ndani ya mlio mmoja! Ndiyo' skia mzee iko hivi.

Mbuzi anatoa Sauti tofauti kabisa ikiwa kuna hatari' either akiona kitu ama akidakwa hata na fisi utajua tu.

Ana sauti ya maumivu, nk
Shida ya kondoo huwa nj jeuri hata akidakwa anataka kufa kiume halipigi kelele, ndio maana unasked watu wanasema kufa kikondoo hence muweke mbuzi na kondoo wakae zizi moja..

PAKA...
Huyu anafugwa sehemu nyingi sana sanaaa
Anatumika kama urembo pia kama mlinzi dhidi ya wadudu waharibifu kama panya,
Kiufupi hili beef Lao halitokuja kuisha hata iweje..

Paka naye ni kiumbe anayepends starehe sana, asilimia kubwa ya maisha yake anayatumia kulala tu .
Jamaa hana mambo mengi akishiba analala zake.

Shida ya paka anapenda kudeka sana utakuta kalala juu ya kitanda chako au Kanyea unga hasa wakiwa bado watoto..

Hii nimeshuhudia personal...
In our childhood, mzee aliletaga paka mkubwa kabisa akiwa kwenye mfuko,yule.paka alikuwa ni tofauti kabisa na hawa wa kwetu mitaani mkia wenye manyoya mengi, uzito mkubwa, manyonya mengi mwilini! Alipendeza kumuangalia for sure..

Shida yake alikuwa jeuri wa kiwango cha kutupwa na alikuwa na urafiki na mimi na mzee wangu tu!
Wengine lilikuwa linawapa chechi sanaaa..!

Sikumoja bibi yetu yeye alikuwa ametoka akaacha mkeka wake chini then akaenda zake, kurudi anakuta paka hilo letu limelala kwenye mkeka wake lime relax...!

Ikabidi achuukue mfagio alitandike guess what!

Nilishuhudia paka akituna kama mpira unavyojazwa upepo then akamrukia mzee yule kifuani!
Bibi wa watu mpaka chini akaenda anabaki anapiga yowe tu mpaka mzee akaja anasema "acha acha"ndipo akaacha yule paka then likaondoka kijeuri taratibu kabisa.

Paka yeye kamwe hutamuona akizaa However mimi nimeshuhudia kwa macho yangu, na wala hahitaji msaada wa mtu anatafuta palipo na privacy atazaa
Kitu kama hicho kwa paka ni very rare kwahiyo nikajifunza kitu tangu that day.

Ingawaje yule paka alipotelea tu mtaani hakuonekana tena maskani I think alishakufa huko ..

Remember kucha za paka ni sumu kwa mwili wa binadamu hivyo usipende kucheza michezo na paka maana tabia zake ni ngumu kujua hata ukiamuangalia usoni ngumu sanaaa.

MBWA..
Mbwa amekuwa akitumika kwa miaka mingi sana kama mlinzi wa Mali na usalama wetu majumbani mwetu .

Ingawaje pia amekuwa mistreated sana na wamiliki wanaomfuga but let me tell you that mbwa ni kiumbe loyal sana kwa binadamu hasa ukimtreat vizuri ndipo utajua tabia zake haswa .

Binafsi kijijini tuliwahi kuwa na mbwa ambaye kwa kweli sikuwahi kumskia akibweka tangu akiwa mdogo mpaka anakua mkubwa! Never seen that!

Hata wazee hawakujua shida ilikuwa nini? Ingawaje tulimpenda sana maana alikuwa stadi sana wakati wa kuwinda!

Binafsi mbwa wetu yule nilimpenda sana naye alikuwa beneath sana na mimi muda mwingi kiasi kwamba asiponiona atanitafuta mpaka nilipo either porini au lah atanitafuta au kunisubiri , licha ya yote hayo sikuwahi kumuona akibweka bado..!

But siku moja jioni kidogo nikiwa nimekaa sehemu karibu na kama kichuguu yule mbwa amekaa pembeni yangu nikiwa napuliza filimbi [ ni zile filimbi kama zenye matobo matobo ipo kama bomba then huwa zinatumika sana madrasa ninapenda sana na nadhani mbwa yule pia alikuwa anapenda nikipuliza maana alikuwa anatulia sana na kuniangalia akiwa pembeni yangu]

Sasa nilipoendelea kupuliza zaidi filimbi yangu akawa ananiangalia sana na kama anahema kwa nguvu dizaini kama mapafu yanambana then akasimama anahangaika nikajiuliza huyu vipi tena .!

Guess what for the first time ever mbwa yule alibweka kwa nguvu sana akiwa mpaka anaruka ruka kwa furaha sana!

Binafsi nikabaki nimepigwa na butwaa kubwa sana maana hakuwahi kubweka popote pale ..!

Tukarudi nyumbani ilipofika usiku nikiwa ndani moyo ukawa unawazia sana tukio lile, kwamba mbona simskii akibweka tena? Ana shida gani huyu huko nje?

Usiku sana kama saa 8 usiku nikastuka usingizini baada ya watu kuamka kwenda nje haraka, tuliskia mbwa anabweka nje! Huyu huyu ambaye huwa habweki ..!

Lakini kilio kile kilikuwa ni cha maumivu means ishara ya maumivu , maana mbwa hubweka kwa namna mbalimbali ili bwana wake ajue ..

Kutoka nje tunaona kwa mbaaaali fisi wawili wanasepa huku bado akilia kilio kile ambacho binafsi mpaka leo bado nakumbuka sana..!

Na huo ndio ukawa mwisho wake ...!

Tujifunze kitu

Unajua nini kuhusu wanyama?
Katika vitu sipendi kuona kwenye maisha yangu ni mtu anaempiga mnyama. Nikiona naumwa kabisa aisee. Cpend cpend cpend. Hii dunia sio yetu tu aisee tumepewa na wanyama pia tusiwatesa.
 
Kuku wanakariri sura za wawafugao...ilikuwa ikifika saa 12 ,inatokea ndio unarejea home na umewakuta wapo hata umbali wa mita Mia toka home,wanaanza kukufuata wale walio wako tu mpaka getini ili waingie.

Ila majogoo ya sikuhizi yanawika hata saa 8.
 
Wakuu kwema?
Well
After a while.nilipata ka likizo kidogo nikaenda zangu kijijini kwetu kuisalimu mifugo ya mzee wangu na yangu pia.it was good and a learning trip. Maana wanyama huwa wana tabia mpya kila kukicha..

Mpaka sasa nina mbuzi 150 na kondoo 100, in such a way binafsi naona fahari kwangu na wananitosha, zaidi wanaongezeka.i love that man.

Tuanze na huyu hapa.
KONDOO..
Huyu mnyama bhana unaweza kudhani mzembe sana na kiburi , noo hayuko hivyo kabisa

Nilipofika mzee akaniambia "kijana kuna kondoo mzuri dume healthy, strong anauzwa na mzee mwenzangu amepata emergency kidogo, kamnunue uongeze mifugo yako"

Nikaona powa bhana twende tukamuone .
Eeh bhana eeh kondoo ameshiba kweli kweli , yaanj dume la mbegu, nikaona huyu atafaa kuzalisha majike yangu.

Mzee akaniuzia kwa laki 1 nikaona sio issue bado poa tu, tukambeba mpaka zizini kwetu, ilikuwa jioni, halafu tulipomnunua ni mbali sana..

Asubuhi mmoja wa ndugu zangu ambaye alikuwa na zamu ya kuchunga akawafungulia kwanza ng'ombe huku akiwahesabu na wengine wakikamuliwa maziwa .

Yule kondoo akachomoka zake.

Baadaye jioni naenda kukagua zizi na mzee , KONDOO HATUKUMKUTA.

guess what? Mzee akasema tukaangalie kule tulipomnunua, japo ilikuwa mbali hao tukaenda ,
Japo nilimbishia mzee kuwa kondoo huyu kurudi hawezi ni mbali sana hapajui..

Kufika bhana TUNAMKUTA KONDOO KATULIA TULI ZIZINI HANA HABARI, MEANS ALIKARIRI NJIA YA KURUDI MPAKA HUKO KWAO KWA ZAMANI ANAPAJUA VIZURI SANA...!

WAKUU HILI NALO LILINISHANGAZA SANA UMBALI WOTE ULE ANAJUAJE???

Tuwapende wanyama wetu, nao watakupenda ,
DO THE RIGHT AND SHAME THE DEVIL..

wife Hannah yeye anapenda kuku wake tu basi
 
Kuku wanakariri sura za wawafugao...ilikuwa ikifika saa 12 ,inatokea ndio unarejea home na umewakuta wapo hata umbali wa mita Mia toka home,wanaanza kukufuata wale walio wako tu mpaka getini ili waingie.

Ila majogoo ya sikuhizi yanawika hata saa 8.
Kuku wana akili sana wanakariri sana hili nimeshuhudia sana wife Hannah anawafuga ni shahidi pia
 
Katika vitu sipendi kuona kwenye maisha yangu ni mtu anaempiga mnyama. Nikiona naumwa kabisa aisee. Cpend cpend cpend. Hii dunia sio yetu tu aisee tumepewa na wanyama pia tusiwatesa.
Mkuu
Wanyama wetu huwa tunajisahau kuwa ni asset kubwa kwetu sana
Matokeo yake tunawatendea unyama sana na wao wana hisia sana

Mfano leo hii mimi na kamshahara kangu mambo yakiwa hovyo nauza ng'ombe wangu mmoja kwa 1 million tu challenge solved..

Do the right and shame the devil
 
Kwa mara ya kwanza nimesoma uzi ulionimotivate kuwa na mifugo na me niexperience hii bond na wanyama
Why not now mkuu?
Anza sasa hutajutia kabisa

Mifugo ni asset zaidi ni comfort zone yako.

Hakuna kitu kinafurahisha kama kuiona mifugo yako ikiwa na afya tele na nguvu hakika hawatakutupa utakapokwama
 
Hao Germany Shepherd nasikia wanang'ata watu. Nataka nifuge wa kitanzania nimpe malezi
Sisi tunafuga hao hao kina Bobby ila mlishe vizuri tangu akiwa mdogo
Chanjo ya anti rubbies

Halafu awe na banda lake asiwe anazurura kujitafutia majalalani ,huyo sio mbwa tena atakuwa jibwa koko.

Mzoeze tangu akiwa mdogo
Muda wa kula labda asubuhi na jioni,
Muda wa kusafisha banda
Asijisaidie bandani na akifanya hivyo mtandike huku ukimnyooshea uozo wake.(usimtandike kama unaua noo yaani kafimbo kadogo dogo kama unamfokea hivi)

Atakuwa a good dog
 
Wakuu
Tumekuwa tukifuga sana wanyama majumbani mwetu kwa miaka mingi hasa jamii za kiafrika.
Ingawaje tumekuwa tukiwatendea unyama uhuni wanyama tuwafugao.

Hapa nitaeleza kwa ufupi niliyoyajua na kuyaona kwa wanyama wa nyumbani hasa wafugwao na tabia zao ambazo ni very rare kuziona ..!

PUNDA.
Kwanza huyu hafugwi. Ndiyo HAFUGIKI. Why? Twende taratibu.
Panda amekuwa akifugwa kwa muda mrefu sana na binadamu
Akitumika kwa shughuli mbalimbali kama kulima.na kubeba mizigo mbalimbali.

Ingawaje kuna tabia zake ambazo ni rare sana kuziona utazijua tu punde ukimtendea vizuri yaani usiwe mkatili kwake.

Kwanza ana akili kuliko ng'ombe na wanyama wengine

Kuna kipindi wakati nipo mdogo kijijini kwetu Punda wetu baada ya kuona kazi nyingi sana mtindo mmoja na viboko vingi sana
Akaona bhana eeh! Chakufia nini? Akasepa zake kama miezi miwili hatumuoni.

Kumbe alikuwa kaenda tu nyumba nyengine usiku karuka zizi kaingia kukaa na ng'ombe katulia!
Mwenye mifugo kaamka asubuhi wala hajauliza sanaaa. Kampa chakula kidogo then kamuacha maana anajua wazi kabisa ukimpa kazi nyingi huyo punda anasepa zakeee..!

Baada ya miezi miwili usiku tena punda yule akarudi maskani kwa mtindo ule ule wa kuruka zizi asubuhi mnamkuta katulia zake ...!

Alipokuwa na ujauzito tulitegemea atazaa tu vizuri guess what??
Tuliona tu punda karudi kutokea porini hana tumbo kubwa tena na hana mtoto! Kamuacha wapi??

Ikabidi wazee wamzunguke na kuanza kumtandika viboko mfululizo mpaka punda yule alipoenda kuonesha alipomuacha mtoto ambapo tungechelewa tungekufa kajifia zake.

Najua unajua au hujui lakini punda anakula sana ukoko ukitaka ahamie kwako mazima mpe kila siku!

Next time nilipokuwa nimekaa tu kariba na zizi nikaona punda wetu mwengine aliyekuwa na mimba , anahangaika sana yaani hatulii !

Ukweli mimi yule punda alinipenda sana na hata nikiwa nimetulia alikuwa akinifuata na kuanza kusugua shingo yake miguuni mwangu , it was my best friend..!

Akanifuata mbio mbio then anageuka ananionesha mbususu yake, nikajua moja moja kwa huyu punda anataka kusaidiwa kujifungua na mimi bwana mdogo sikujua how to do it, ikabidi niwaite wajuzi waje kumsaidia mtoto atoke.. kwa kweli nilishuhudia namna wanyama wakizaa ni tabu tupu wanapata..!

Unatakiwa ujue kuwa punda ni mchungaji mzuri wa mifugo hasa ng'ombe na mbuzi, anaongoza njia na kuwaelekeza pa kupita mifugo sababu anakariri sana njia.

Pia anafukuza sana wanyama pori hasa fisi wanaokamata mbuzi [shughuli yake wanaijua vizuri]

NG'OMBE..

Huyu ni mnyama ambaye tuseme anashika nafasi ya pili kwa kuchinjwa akiongozwa na nguruwe!

Ng'ombe ni mnyama ambaye yuko so friendly na binadamu.
Iwapo tu ukimpenda na kumjali sio kila mara viboko noo

Kwa wasukuma.ni kawaida kukuta ng'ombe mmoja kavunjika pembe kwa viboko

Ng'ombe hawezi kujifungua mwenyewe au akiweza atazaa kwa tabu sana au ndama kufa!

Kama akikuozea sana atakufuata then atakeukia kukuonesha "bwana eeh mwanangu anataka kutoka nisaidie" then utatakiwa kumsaidia kumvuta ndama atoke [hili nimeshuhudia personal]

Watu wa dar kuleni nyama tu hivi hivi tu lakini mngejua namna wafugaji wanavyopata tabu.

Ndama anapotoka inatakiwa mmoja anyonye haraka kwenye pua'mdomo' maskio ili ndama asife otherwise mtampoteza..!

MBUZI
Huyu yeye anafugwa sana sana kwa kitoweo au biashara unakuta mtu kakwama anauza chap mbuzi mmoja kama 70k kutatua kamzozo fulani.

Mbuzi yeye ni muoga sana Hali inayopelekea kuwa na akili
Mara nyingi mbuzi hukaa zizini na mifugo mingine ili kusudi kutoa alert iwapo litatokea tatizo mfano fisi ameingia zizini ama lah
Yeye akiona tu labda kondoo amedakwa na fisi [fisi anapenda kondoo kuliko mbuzi] basi atapiga yowe "jamani baba mwenye nyumba eeh huku kuna muujiza tumevamiwa"

Na kikawaida mbuzi ana Saudi tofauti tofauti ndani ya mlio mmoja! Ndiyo' skia mzee iko hivi.

Mbuzi anatoa Sauti tofauti kabisa ikiwa kuna hatari' either akiona kitu ama akidakwa hata na fisi utajua tu.

Ana sauti ya maumivu, nk
Shida ya kondoo huwa nj jeuri hata akidakwa anataka kufa kiume halipigi kelele, ndio maana unasked watu wanasema kufa kikondoo hence muweke mbuzi na kondoo wakae zizi moja..

PAKA...
Huyu anafugwa sehemu nyingi sana sanaaa
Anatumika kama urembo pia kama mlinzi dhidi ya wadudu waharibifu kama panya,
Kiufupi hili beef Lao halitokuja kuisha hata iweje..

Paka naye ni kiumbe anayepends starehe sana, asilimia kubwa ya maisha yake anayatumia kulala tu .
Jamaa hana mambo mengi akishiba analala zake.

Shida ya paka anapenda kudeka sana utakuta kalala juu ya kitanda chako au Kanyea unga hasa wakiwa bado watoto..

Hii nimeshuhudia personal...
In our childhood, mzee aliletaga paka mkubwa kabisa akiwa kwenye mfuko,yule.paka alikuwa ni tofauti kabisa na hawa wa kwetu mitaani mkia wenye manyoya mengi, uzito mkubwa, manyonya mengi mwilini! Alipendeza kumuangalia for sure..

Shida yake alikuwa jeuri wa kiwango cha kutupwa na alikuwa na urafiki na mimi na mzee wangu tu!
Wengine lilikuwa linawapa chechi sanaaa..!

Sikumoja bibi yetu yeye alikuwa ametoka akaacha mkeka wake chini then akaenda zake, kurudi anakuta paka hilo letu limelala kwenye mkeka wake lime relax...!

Ikabidi achuukue mfagio alitandike guess what!

Nilishuhudia paka akituna kama mpira unavyojazwa upepo then akamrukia mzee yule kifuani!
Bibi wa watu mpaka chini akaenda anabaki anapiga yowe tu mpaka mzee akaja anasema "acha acha"ndipo akaacha yule paka then likaondoka kijeuri taratibu kabisa.

Paka yeye kamwe hutamuona akizaa However mimi nimeshuhudia kwa macho yangu, na wala hahitaji msaada wa mtu anatafuta palipo na privacy atazaa
Kitu kama hicho kwa paka ni very rare kwahiyo nikajifunza kitu tangu that day.

Ingawaje yule paka alipotelea tu mtaani hakuonekana tena maskani I think alishakufa huko ..

Remember kucha za paka ni sumu kwa mwili wa binadamu hivyo usipende kucheza michezo na paka maana tabia zake ni ngumu kujua hata ukiamuangalia usoni ngumu sanaaa.

MBWA..
Mbwa amekuwa akitumika kwa miaka mingi sana kama mlinzi wa Mali na usalama wetu majumbani mwetu .

Ingawaje pia amekuwa mistreated sana na wamiliki wanaomfuga but let me tell you that mbwa ni kiumbe loyal sana kwa binadamu hasa ukimtreat vizuri ndipo utajua tabia zake haswa .

Binafsi kijijini tuliwahi kuwa na mbwa ambaye kwa kweli sikuwahi kumskia akibweka tangu akiwa mdogo mpaka anakua mkubwa! Never seen that!

Hata wazee hawakujua shida ilikuwa nini? Ingawaje tulimpenda sana maana alikuwa stadi sana wakati wa kuwinda!

Binafsi mbwa wetu yule nilimpenda sana naye alikuwa beneath sana na mimi muda mwingi kiasi kwamba asiponiona atanitafuta mpaka nilipo either porini au lah atanitafuta au kunisubiri , licha ya yote hayo sikuwahi kumuona akibweka bado..!

But siku moja jioni kidogo nikiwa nimekaa sehemu karibu na kama kichuguu yule mbwa amekaa pembeni yangu nikiwa napuliza filimbi [ ni zile filimbi kama zenye matobo matobo ipo kama bomba then huwa zinatumika sana madrasa ninapenda sana na nadhani mbwa yule pia alikuwa anapenda nikipuliza maana alikuwa anatulia sana na kuniangalia akiwa pembeni yangu]

Sasa nilipoendelea kupuliza zaidi filimbi yangu akawa ananiangalia sana na kama anahema kwa nguvu dizaini kama mapafu yanambana then akasimama anahangaika nikajiuliza huyu vipi tena .!

Guess what for the first time ever mbwa yule alibweka kwa nguvu sana akiwa mpaka anaruka ruka kwa furaha sana!

Binafsi nikabaki nimepigwa na butwaa kubwa sana maana hakuwahi kubweka popote pale ..!

Tukarudi nyumbani ilipofika usiku nikiwa ndani moyo ukawa unawazia sana tukio lile, kwamba mbona simskii akibweka tena? Ana shida gani huyu huko nje?

Usiku sana kama saa 8 usiku nikastuka usingizini baada ya watu kuamka kwenda nje haraka, tuliskia mbwa anabweka nje! Huyu huyu ambaye huwa habweki ..!

Lakini kilio kile kilikuwa ni cha maumivu means ishara ya maumivu , maana mbwa hubweka kwa namna mbalimbali ili bwana wake ajue ..

Kutoka nje tunaona kwa mbaaaali fisi wawili wanasepa huku bado akilia kilio kile ambacho binafsi mpaka leo bado nakumbuka sana..!

Na huo ndio ukawa mwisho wake ...!

Tujifunze kitu

Unajua nini kuhusu wanyama?
Nimepata kitu hata hivyo
 
Pia kuhusu NG'OMBE
Nimegundua mengine mengi

Hawa jamaa wakiwa zizinj hawalali wote pamoja never!

Yaani tuseme usiku zizini walale wote chini hakuna!

NG'OMBE huwa wanawekeana zamu kulinda hivyo hawawezi kulala wote pamoja
Wawili au watatu watabaki kusimama wakilinda na zamu wanapangiana inategemea kwa muda gani let's say siku 2 zamu.

Wengine watalala then wengine watalinda! Nimeshashuhudia sana hili tangu udogoni na wazee waliniambia hili sana .

Ushirikiano wao ni kama wa binadamu pia hivyo wanalindana...
 
Mimi kuku wamama nilikua nikihisi wataka kutotoa nachukua yi nalipasua natoa kifaranga kamakipohai nakirudisha kwamamake nalipasua lingine kama kimekufa natupa ndionajua kua bado mudawake haujafika nasubiri kwanza
 
Duh mkuu why doing that? Nadhani mayai yanapasuka yenyewe tu

Au ngoja tumuulize wife Hannah
 
Back
Top Bottom