Okay🤣🤣🤣 nilipouona huu uzi niliudharau lakini leo nikasema ngoja nione kilichoandikwa kumbe ni thread moja nzuri sana oky lets me share baadhi ya vitu juu ya hawa wanyama .
PAkA.
Huyu ana akili sana japo ni mbinafsi . Mara nyingi anapomkamata panya anapenda amchezee sanaaa na ndipo mwishowe aweze kumlaa . Mara nyingi huwafanya hivi kwa lengo la kumvunja panya mifupa yotee. Hivyo kila anapomchezea panya na kumuacha huwa anamuangalia je ni sehemu gani ya mwili bado inafanya kazi ili aendelee na zoezi la kumvunja .
- Paka jike Mara nyingi huwa na dume moja tu . Na hili dume mara nyingi huwa ni lile lilombikiri , sisemi madume wangine hawawezi kula mzigo . Ili dume jingine lile mzigo moja inabidi liwe na nguvu na mwanzoni lazima liangushe kipigo kikali sana kwa huyu jike. Na hapa ndiyo utakapo sikia mapaka usiku yanalia nyaaaaaau nyaaaaauu yakipigana lakini pia halii hutokea hata kwa lile dume la kwanza lilombikiri kwani kuna wakati kwasababu azijuazo jike mwenyewe kama vile kuchoka au kutotamani tendo kwani mara nyingi maani(mbegu) za paka dume huwa ni za moto sanaa na hupelekea paka jike kuungua pindi zinapomuingia wakati wa tendo ( ndiyo maana mara nyingi paka dume baada ya tendo ikishamuachia paka jike utamuona paka jike anagaragara chini ni kwasababu zile mbegu zinapokuwa zinaingia ndani zaidi ya paka jike hupelekea paka jike kuungua ) na kupelekea paka jike kuwa mkali na mwenye hasira sanaa ambayo hutaka kumjerui paka dume kwa kucha lakini mara nyingi hushindwa kwani paka dume kabla ya kumuingia huhakikisha kamdhibiti vyema kwa kumshikilia sehemu ya shingo na ndyo maana dume hupaswa kuwa na nguvu nje na hapo hawezi kula mzigo . Kwa wale mliowahi kukaa mabibo hostel hasa kule kwenye zile block za watu wa masters basi hili swala la paka kulana mzigo mbele za watu nadhani mtakuwa mmeliona sana na kuwa mashahidi juu ya hichi nacho kiandika hapa na hata wale ambao hawajawahi kuona paka wakifanya mapenzi nawashauri waende mabibo hostel wakajionee utaliii wa bure kabisaa .
hivyo paka jike kuna wakati hujikuta tu hataki kutoa mzigo kwasababu ya kuchoshwa na kuungua hivyo halii hupelekea dume kukasirika sana nakuangisha kipigo huku akimvizia paka jike azubae tu ili akamate shingo na kujilia zake mzogo . Maana paka mara nyingi ushikapo shingoni huwa anakuwa hana ujanja .
kuku
huyu mengi yameshazungumzia na wadau huko juu . Ila lakuongezea tu ni kuwa huyu usiku mdomo wake huwa na sumuu hivyo inabidi kuchukua tahadhari sanaa wakati wa usiku asije kukudonoa . Maana anaweza kukuachia sumu ambayo inaweza kukudhuru kiafya hapo baadae .
Jogoo na tetea .
Lakini bado tukiwa hapa kwenye kuku . Huku nikuulize shwari je umeshawahi kujiuliza kwanini ukiambiwa umkamate tetea inaweza kuchukua nusu saa pengine hata saa nzima kuweza kufanikiwa kumkamata au wakati mwingine ukashindwa kumkamata kabisa ? . Lakini jogoo anapo mfukuzia tetea huchukua dakika 5 au mbaka 10 kumkamata tetea ?..
Jibu .
Mara nyingi jogoo anapomfukuzia tetea . Pale kuna mchakato wa kibiolojia unaofanyika kama ilivyokwetu tu binadamu . Pindi ukutanapo na mwanamke huwezi tu kumvua nguo mwanamke na kuchomeka ni lazima umuandae basi sasa turudi kwenye mada yetu . Basi hata jogoo pindi anapomfukuzia tetea zile dk 5 au 10 za kumfukuzia tetea husaidia kumuandaa tetea kiakili na kimwili ili jogoo anapokuja kumuingia asiweze kumuumiza na kumchubua 🤣🤣 ina chekesha lakini ndyo hivyo .
Mbwa .
Mengi yaliyosemwa juu ya mbwa na wadau yapo sahihi kabisa . Lakini cha kuongezea ni kwamba . Umfugapo mbwa nyumbani kwako basi na yeye huwa anatabia ya kuweka mipaka ya kiutawala tena hii hufanywa mara nyingi na mbwa dume ( kama ni wale wasiofugiwa bandani ) . Mbwa dume huweka mipaka ya kiutawala kwa kunya mavi au kukojoa kaskazini , kusini mashariki na magharibi ili kutoa ishara kwa mbwa wengine wageni na yeyete atakaye ikililia mipaka yake basi hapo kipigo kitamuhusu labda awe mbwa jike hapo msamaha utahusika kama mjuavyo tena
Njiwa wa nyumbani .
Jamani wengine naona tumezungumzia mbwa , ng'ombe punda lakin tumemsahau njiwa. Hawa nao wana tabia zao za kushanga sana .
1) mara nyingi njiwa hutaga mayai mawili tuuu . Na katika mayai haya moja huwa njiwa dume na jingine huwa njia jike .
2) njiwa hawa wawili hukuwa pamoja na kuwa wapenzi . Na pindi njiwa jike atakapo taga mayai swala la kuatamia na mayai ni shwala la wote . Na maanisha nini ? . Mayai yatahatamia na njiwa dume huku njiwa jike akiwa kaenda kitafuta chakula na kuna muda mayai utahatamiwa na njiwa jike huku njiwa dume akiwa kaenda kutafuta chakula hukuna kutegea na dume akileta tu utegezi kwenye kuatamia hushushiwa kipigo na njiwa jike vizuri tu na hii huendelea hata pindi wapatapo makinda shwara la kuwalisha ni swala la woteee ( hapa wanatufundisha mgawanyo wa kazi katika malezi )
3) hapo juu tumeona njiwa huwa wanakuwa wawili wawili toka utotoni mbaka katika maisha yao ya ukubwani . Sasa nini hutokea pindi njiwa dume anaondokewa na njia jike ??. Kimsingi kama aliekufa au aliyepotea ni njiwa jike basi inashauriwa ni bora ukamchinja huyu dume maana hali ya upweke ambayo hubaki nayo huweza kupelekea njiwa huyu dume hata kufa . Kwani humchukua muda mrefu sana kumpata mwenza mwingine . Lakini kama ni jike wala huwa hamnashida sana kwani hueeza kupata dume jingine mapema sanaa.
4) kama utafuga njiwa inashauriwa kila asubuhi ni bora ukawa unawarushia kiasi fulani cha nafaka kama vile mchele huku ukiwaambia mawili matatu . Hii itakusaidia pindi ukutwapo na majanga kama msiba kwani ukipata msiba unaweza kutumia ile fursa ya asubuhi kuwa wapa taarifa kuwa umepata msiba hivyo wakiona watu wengi na makele ya vilio wasistuke . Kwani usipofanya hivyo hupelekea njiwa kuhama na kuamia kwa mfugaji mwingine .
Nguruwe .
Wengi wamemzungumzia huyu . Lakini ningependa kuongezea kuwa kama utataka kumfuga huyu basi ni bora ukamjengea banda la juu kwa kutumia mabanzi au mbao . Kwani kama utatumia matofari ya kuchoma au ya cement basi inaweza kuwa hasara maana nguruwe akiwa na njaa huyageuza matofari kama chakula na kuyala .
- pua ya nguluwe ni ngumu kuliko hats uionavyo . Hutumia kufukulia hasa kwa yale mabanda ya chini yaliyosakafiwa na hata kusafisha banda lake pindi lijaapo kinyesi .
- wafugaji hawashauriwi kumzoesha kumpa mabaki ya nyama ya ng'ombe nguruwe kwani hii huleta shida sana pindi awapo na watoto wadogo . Kwani pindi atakapochelewesha chakula au akawa na njaa ya ghafla hupelekea kula kitoto chake mwenyewe .
- Samaki ni moja ya kitoweo kikubwa sana wakitumiacho wezi kumuiba nguruwe . Wezi huvamia banda la nguruwe na kutengeneza uwazi utakaomuwezesha nguruwe kupenya
. Baada ya hapo huchukua samaki aliyochwa na kumfunga kamba na kumuweka nje ya banda la nguruwe waliyedhamiria kumuiba . Pindi nguruwe aipatapo harufu ya samaki huyo basi huwafuata wezi hawa mwenyewe kimya kimya mbaka machichioni . Na kubaki wakikushangaza mfugaji imewezakana vipi kumbeba nguruwe mkubwa kiasi kile bila ya nguruwe kupiga kelele ???.
- miwa ni miongoni mwa chakula kingine akipendacho nguruwe . Hivyo usije kulima shamba la miwa karibu na wafugaji wa nguruwe utawalaumu bureee tu.
Nimeona niongee haya machache lakini pia ntafurahi kuona na wengine wakiongezea mengine na kuufanya uzi huu kuwa uzi bora kabisa mwaka 2024.