Unayoyajua na usiyoyajua kuhusu wanyama wa kufugwa

Unayoyajua na usiyoyajua kuhusu wanyama wa kufugwa

Nguruwe
Hawa ni wasafi sana, Bandani huchagua upande wa kujisaidia. Muda wote watajisaidia kona hiyo tu hata usafisha na kufanya msbadiliko gani bandani, kwao hapo ndio choo. Sijaona kitu hii kwa wanyama wengine
Duh sijawahi sikia hili mkuu 🤣🤣
 
Ukienda kuwinda na mbwa porini na hilo eneo kukawa na chatu basi jua upo kwenye hatari ya kuliwa.
Chatu anapokua anawinda anatoa harufu ya kuvutia ambayo inamvutia mbwa, mbwa atasogea lakini akigundua kwamba ni chatu basi hukimbilia kwako na hapo ndo cha moto utakiona
Mbwa akiona chatu anafunguka mbio hatari
Mbwa niliwahi kuwapoteza wawili waligongwa tu na nyoka wa kawaida
 
.
Mie experience yangu labda kwa kuku tu na mbwa ndo nimewafuga kwa muda mrefu sana.

Hivi kuna mnyama wa kufugwa anapenda ngono kama mbwa dume?

Kuku wanatofautiana tabia kama binadamu, pia kuku wanamtambua binadamu mbaya, wanatoa ishara kwa namna tofauti ya milio yao.

Mbwa ni mnyama mzalendo zaidi anaweza kuwa rafiki kuliko hata binadamu, Unavyomfundisha ndivyo anavyokuwa.
Mkuu mm nafuga kuku wa kienyeji natamani kujua hzo ishara na hyo milio unayoizungumzia
 
Paka mnoko alafu anamdharau sana Mbwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani paka ni mnyama flani self-centered sana. Anahisi dunia inatakiwa izunguke kukidhi furaha zake.

Utakuta analala sehemu soft zaidi ndani,
anataka kula anachokula binadamu na akikamata panya anamchezea sana kabla ya kumla.
 
Hasa Mbwa ni mwepes kumtambua mtu mzuri na mbaya

na pia Mbwa anapokutizama sana machoni ana uwezo wakutambua ikiwa humpendi au unampenda

Ukiona Mbwa anakutizama sana machoni ujue anakusoma hvyo
Paka na mmbwa huwa hawapotei kabisa wakisafirishwa hata umbali gani ilimradi uwe mji huo huo..

1990s tulishawahi kuweka paka mmoja kwenye boksi kisha tukamsafirisha mbali sana kama km 70 alitupwa bwawani maana alikuwa anadokoa mno mboga jikoni na kunya hovyo hovyo, baada ya siku 4 tulipofungua mlango asubuhi 06:00 hrs alikutwa akiwa amelala nnje ya mlango mkuu wa nyumba.

Mmbwa, Poppy mbegu ya kizungu aliyotoka nayo Mzee Brazil na kuifuga Morogoro, alikuwa mkali sana na alisababisha majeraha kwa wanafunzi na baadhi ya Watu. Alikuwa anakodishwa kuwinda wanyama porini ila bado alileta balaa. Mshua aliamua kumuuzia Rafiki yake kuepuka balaa aliyekuwa akiishi umbali kama km 52 ila baada ya wiki 1 mmbwa alitoroka na kurudi home.

Paka anafundishika tabia njema ila usijichanganye kumfungia ndani ukiwa pekeyako eti umpige, atakuua na usijesema sikukuambia tukikutana paradiso.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Yaani paka ni mnyama flani self-centered sana. Anahisi dunia inatakiwa izunguke kukidhi furaha zake.

Utakuta analala sehemu soft zaidi ndani,
anataka kula anachokula binadamu na akikamata panya anamchezea sana kabla ya kumla.
Ila pia paka ni kiumbe kivumilivu sana kwa njaa na huwa kigumu sana kukiua. Wahenga husema ana roho saba ingawa siamini lakini kwa shughuli tulizokuwa tukifanya utotoni kuua paka shume mitaani hakika si kitu rahisi kuwaua.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Paka na mmbwa huwa hawapotei kabisa wakisafirishwa hata umbali gani ilimradi uwe mji huo huo..

1990s tulishawahi kuweka paka mmoja kwenye boksi kisha tukamsafirisha mbali sana kama km 70 alitupwa bwawani maana alikuwa anadokoa mno mboga jikoni na kunya hovyo hovyo, baada ya siku 4 tulipofungua mlango asubuhi 06:00 hrs alikutwa akiwa amelala nnje ya mlango mkuu wa nyumba.

Mmbwa, Poppy mbegu ya kizungu aliyotoka nayo Mzee Brazil na kuifuga Morogoro, alikuwa mkali sana na alisababisha majeraha kwa wanafunzi na baadhi ya Watu. Alikuwa anakodishwa kuwinda wanyama porini ila bado alileta balaa. Mshua aliamua kumuuzia Rafiki yake kuepuka balaa aliyekuwa akiishi umbali kama km 52 ila baada ya wiki 1 mmbwa alitoroka na kurudi home.

Paka anafundishika tabia njema ila usijichanganye kumfungia ndani ukiwa pekeyako eti umpige, atakuua na usijesema sikukuambia tukikutana paradiso.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Hii ya paka usijifungie naye ndani ni stori tupu haina ukweli.

Fikiria kwa uzito na umbo la paka awe amekasirika anaweza kukushambulia kwa namna gani ili akuue?

Kuna paka shume alikua msumbufu anaua vifaranga. Siku ikafika nikamkuta in action akakimbilia ndani nikafunga mlango nikawa nina fimbo tu mikono yote miwili.

Leo nipo hapa
 
Kitu namisi ni kuona zile battle za madume ya mafahali.

Tukiwa machalii wadogo tulikuwa tunachonganisha mafahali halafu tunakaa kuangalia battle.

Wale mafahali wanafikia hatua ya kuwa na bifu na unakuta wako busy kunoa pembe zao kwenye vichuguu.
[Alafu kenge mmoja anasema wanaume msiwe na wivu]
 
PAKA...
Huyu anafugwa sehemu nyingi sana sanaaa
Anatumika kama urembo pia kama mlinzi dhidi ya wadudu waharibifu kama panya,
Kiufupi hili beef Lao halitokuja kuisha hata iweje..

Paka naye ni kiumbe anayepends starehe sana, asilimia kubwa ya maisha yake anayatumia kulala tu .
Jamaa hana mambo mengi akishiba analala zake.

Shida ya paka anapenda kudeka sana utakuta kalala juu ya kitanda chako au Kanyea unga hasa wakiwa bado watoto..

Hii nimeshuhudia personal...
In our childhood, mzee aliletaga paka mkubwa kabisa akiwa kwenye mfuko,yule.paka alikuwa ni tofauti kabisa na hawa wa kwetu mitaani mkia wenye manyoya mengi, uzito mkubwa, manyonya mengi mwilini! Alipendeza kumuangalia for sure..

Shida yake alikuwa jeuri wa kiwango cha kutupwa na alikuwa na urafiki na mimi na mzee wangu tu!
Wengine lilikuwa linawapa chechi sanaaa..!

Sikumoja bibi yetu yeye alikuwa ametoka akaacha mkeka wake chini then akaenda zake, kurudi anakuta paka hilo letu limelala kwenye mkeka wake lime relax...!

Ikabidi achuukue mfagio alitandike guess what!

Nilishuhudia paka akituna kama mpira unavyojazwa upepo then akamrukia mzee yule kifuani!
Bibi wa watu mpaka chini akaenda anabaki anapiga yowe tu mpaka mzee akaja anasema "acha acha"ndipo akaacha yule paka then likaondoka kijeuri taratibu kabisa.

Paka yeye kamwe hutamuona akizaa However mimi nimeshuhudia kwa macho yangu, na wala hahitaji msaada wa mtu anatafuta palipo na privacy atazaa
Kitu kama hicho kwa paka ni very rare kwahiyo nikajifunza kitu tangu that day.

Ingawaje yule paka alipotelea tu mtaani hakuonekana tena maskani I think alishakufa huko ..

Remember kucha za paka ni sumu kwa mwili wa binadamu hivyo usipende kucheza michezo na paka maana tabia zake ni ngumu kujua hata ukiamuangalia usoni ngumu sanaaa.

Tujifunze kitu
 
MBWA..
Mbwa amekuwa akitumika kwa miaka mingi sana kama mlinzi wa Mali na usalama wetu majumbani mwetu .

Ingawaje pia amekuwa mistreated sana na wamiliki wanaomfuga but let me tell you that mbwa ni kiumbe loyal sana kwa binadamu hasa ukimtreat vizuri ndipo utajua tabia zake haswa .

Binafsi kijijini tuliwahi kuwa na mbwa ambaye kwa kweli sikuwahi kumskia akibweka tangu akiwa mdogo mpaka anakua mkubwa! Never seen that!

Hata wazee hawakujua shida ilikuwa nini? Ingawaje tulimpenda sana maana alikuwa stadi sana wakati wa kuwinda!

Binafsi mbwa wetu yule nilimpenda sana naye alikuwa beneath sana na mimi muda mwingi kiasi kwamba asiponiona atanitafuta mpaka nilipo either porini au lah atanitafuta au kunisubiri , licha ya yote hayo sikuwahi kumuona akibweka bado..!

But siku moja jioni kidogo nikiwa nimekaa sehemu karibu na kama kichuguu yule mbwa amekaa pembeni yangu nikiwa napuliza filimbi [ ni zile filimbi kama zenye matobo matobo ipo kama bomba then huwa zinatumika sana madrasa ninapenda sana na nadhani mbwa yule pia alikuwa anapenda nikipuliza maana alikuwa anatulia sana na kuniangalia akiwa pembeni yangu]


Sasa nilipoendelea kupuliza zaidi filimbi yangu akawa ananiangalia sana na kama anahema kwa nguvu dizaini kama mapafu yanambana then akasimama anahangaika nikajiuliza huyu vipi tena .!

Guess what for the first time ever mbwa yule alibweka kwa nguvu sana akiwa mpaka anaruka ruka kwa furaha sana!

Binafsi nikabaki nimepigwa na butwaa kubwa sana maana hakuwahi kubweka popote pale ..!

Tukarudi nyumbani ilipofika usiku nikiwa ndani moyo ukawa unawazia sana tukio lile, kwamba mbona simskii akibweka tena? Ana shida gani huyu huko nje?

Usiku sana kama saa 8 usiku nikastuka usingizini baada ya watu kuamka kwenda nje haraka, tuliskia mbwa anabweka nje! Huyu huyu ambaye huwa habweki ..!

Lakini kilio kile kilikuwa ni cha maumivu means ishara ya maumivu , maana mbwa hubweka kwa namna mbalimbali ili bwana wake ajue ..

Kutoka nje tunaona kwa mbaaaali fisi wawili wanasepa huku bado akilia kilio kile ambacho binafsi mpaka leo bado nakumbuka sana..!

Na huo ndio ukawa mwisho wake ...!
 
Anaona kama unamhgasi kwenye nyumba yake..
Yani kashenzi sana kanalala ile sehemu ambayo wewe unalala wewe.

Kuna mda kanakuangalia kwa kukushusha na kukupandisha kwa dharau .

Kuna kamoja nilikafuga kenyewe kalikua kanakaa kwenye zulia tu yani hakataki kugusa chini .

Then nikitokea kananiangalia huku kamelala kwa madharau makubwa as if kenyewe nika boss kangu. Ukiangalia hakakua na mchango wowote kwangu zaidi ya kula vizuri mda mwingne zaidi yangu na kulala tu .


Tofauti kabisa na mbwa ambae anachukulia tatzo lako ni lake, kuna mda ata ukiishiwa pesa mbwa anajua ,anashare na wewe huzuni . Tofauti na paka anakuona kama kituko.
 
Back
Top Bottom