Wakuu
Tumekuwa tukifuga sana wanyama majumbani mwetu kwa miaka mingi hasa jamii za kiafrika.
Ingawaje tumekuwa tukiwatendea unyama uhuni wanyama tuwafugao.
Hapa nitaeleza kwa ufupi niliyoyajua na kuyaona kwa wanyama wa nyumbani hasa wafugwao na tabia zao ambazo ni very rare kuziona ..!
PUNDA.
Kwanza huyu hafugwi. Ndiyo HAFUGIKI. Why? Twende taratibu.
Panda amekuwa akifugwa kwa muda mrefu sana na binadamu
Akitumika kwa shughuli mbalimbali kama kulima.na kubeba mizigo mbalimbali.
Ingawaje kuna tabia zake ambazo ni rare sana kuziona utazijua tu punde ukimtendea vizuri yaani usiwe mkatili kwake.
Kwanza ana akili kuliko ng'ombe na wanyama wengine
Kuna kipindi wakati nipo mdogo kijijini kwetu Punda wetu baada ya kuona kazi nyingi sana mtindo mmoja na viboko vingi sana
Akaona bhana eeh! Chakufia nini? Akasepa zake kama miezi miwili hatumuoni.
Kumbe alikuwa kaenda tu nyumba nyengine usiku karuka zizi kaingia kukaa na ng'ombe katulia!
Mwenye mifugo kaamka asubuhi wala hajauliza sanaaa. Kampa chakula kidogo then kamuacha maana anajua wazi kabisa ukimpa kazi nyingi huyo punda anasepa zakeee..!
Baada ya miezi miwili usiku tena punda yule akarudi maskani kwa mtindo ule ule wa kuruka zizi asubuhi mnamkuta katulia zake ...!
Alipokuwa na ujauzito tulitegemea atazaa tu vizuri guess what??
Tuliona tu punda karudi kutokea porini hana tumbo kubwa tena na hana mtoto! Kamuacha wapi??
Ikabidi wazee wamzunguke na kuanza kumtandika viboko mfululizo mpaka punda yule alipoenda kuonesha alipomuacha mtoto ambapo tungechelewa tungekufa kajifia zake.
Najua unajua au hujui lakini punda anakula sana ukoko ukitaka ahamie kwako mazima mpe kila siku!
Next time nilipokuwa nimekaa tu kariba na zizi nikaona punda wetu mwengine aliyekuwa na mimba , anahangaika sana yaani hatulii !
Ukweli mimi yule punda alinipenda sana na hata nikiwa nimetulia alikuwa akinifuata na kuanza kusugua shingo yake miguuni mwangu , it was my best friend..!
Akanifuata mbio mbio then anageuka ananionesha mbususu yake, nikajua moja moja kwa huyu punda anataka kusaidiwa kujifungua na mimi bwana mdogo sikujua how to do it, ikabidi niwaite wajuzi waje kumsaidia mtoto atoke.. kwa kweli nilishuhudia namna wanyama wakizaa ni tabu tupu wanapata..!
Unatakiwa ujue kuwa punda ni mchungaji mzuri wa mifugo hasa ng'ombe na mbuzi, anaongoza njia na kuwaelekeza pa kupita mifugo sababu anakariri sana njia.
Pia anafukuza sana wanyama pori hasa fisi wanaokamata mbuzi [shughuli yake wanaijua vizuri]
NG'OMBE..
Huyu ni mnyama ambaye tuseme anashika nafasi ya pili kwa kuchinjwa akiongozwa na nguruwe!
Ng'ombe ni mnyama ambaye yuko so friendly na binadamu.
Iwapo tu ukimpenda na kumjali sio kila mara viboko noo
Kwa wasukuma.ni kawaida kukuta ng'ombe mmoja kavunjika pembe kwa viboko
Ng'ombe hawezi kujifungua mwenyewe au akiweza atazaa kwa tabu sana au ndama kufa!
Kama akikuozea sana atakufuata then atakeukia kukuonesha "bwana eeh mwanangu anataka kutoka nisaidie" then utatakiwa kumsaidia kumvuta ndama atoke [hili nimeshuhudia personal]
Watu wa dar kuleni nyama tu hivi hivi tu lakini mngejua namna wafugaji wanavyopata tabu.
Ndama anapotoka inatakiwa mmoja anyonye haraka kwenye pua'mdomo' maskio ili ndama asife otherwise mtampoteza..!
MBUZI
Huyu yeye anafugwa sana sana kwa kitoweo au biashara unakuta mtu kakwama anauza chap mbuzi mmoja kama 70k kutatua kamzozo fulani.
Mbuzi yeye ni muoga sana Hali inayopelekea kuwa na akili
Mara nyingi mbuzi hukaa zizini na mifugo mingine ili kusudi kutoa alert iwapo litatokea tatizo mfano fisi ameingia zizini ama lah
Yeye akiona tu labda kondoo amedakwa na fisi [fisi anapenda kondoo kuliko mbuzi] basi atapiga yowe "jamani baba mwenye nyumba eeh huku kuna muujiza tumevamiwa"
Na kikawaida mbuzi ana Saudi tofauti tofauti ndani ya mlio mmoja! Ndiyo' skia mzee iko hivi.
Mbuzi anatoa Sauti tofauti kabisa ikiwa kuna hatari' either akiona kitu ama akidakwa hata na fisi utajua tu.
Ana sauti ya maumivu, nk
Shida ya kondoo huwa nj jeuri hata akidakwa anataka kufa kiume halipigi kelele, ndio maana unasked watu wanasema kufa kikondoo hence muweke mbuzi na kondoo wakae zizi moja..
Unajua nini kuhusu wanyama?