Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 15,966
- 26,404
- Thread starter
- #61
Ndio iko wazi nao wana hisia sana sanaaaNilichogundua ukimpenda mnyama na yeye anakupenda
Mnyama kukurudishia uovu ni mara chache ukimtendea wema nao wana hisia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio iko wazi nao wana hisia sana sanaaaNilichogundua ukimpenda mnyama na yeye anakupenda
Kuhusu hilo la mwanae ni ukweli nimewahi kushuhudia liveAlafu punda anasifa moja;
Ukim'bebesha mwanae mzigo haendi, utapiga viboko umuue, m'bebeshe yeye mizigo yote mwanae atembee free.
Nimewaona sana kule Usafwani(Mbeya) wakibebeshwa mahindi,mkaa na viazi.
Punda akifika lami ni mjinga sana, gari inakuja wala hakimbii anaficha tu kichwa anaacha mwili wote anagongwa.
Hapo kwenye punda umenikumbusha Hadithi za kiswahili (YouTube) punda alikuwa mvivu hataki kubeba mizigo kuvuka nayo mto, sasa siku moja akapata wazo kwakuwa mizigo ili kuwa ni chumvi.
Basi alivyo fika pale mtoni akaa kwenye maji chumvi yote ikayeyuka Punda alifurahi sana hakuhisi uzito kwenye mgongo wake, Hiyo ndio ikawa tabia yake .. Nimecheka sana
Kuku nao Wana akili sanahufugi kuku???
Ng'ombe ambaye mapembe yake yamekaa horizontally huwa wabishi sana kupigwa, wanaweza wakapigana siku nzima.Kitu namisi ni kuona zile battle za madume ya mafahali.
Tukiwa machalii wadogo tulikuwa tunachonganisha mafahali halafu tunakaa kuangalia battle.
Wale mafahali wanafikia hatua ya kuwa na bifu na unakuta wako busy kunoa pembe zao kwenye vichuguu.
Anaona kama unamhgasi kwenye nyumba yake..Kuna mda sijui anakuonaje ata wewe mwenye nyumba
Halafu kuna jamaa hapo ukimwambia anabisha eti uongoNg'ombe ambaye mapembe yake yamekaa horizontally huwa wabishi sana kupigwa, wanaweza wakapigana siku nzima.
Ng'ombe ambao mapembe yao yapo kama U na yamenyoka kiaina kwenda juu huwa wanapiga ng'ombe wengi sana sababu mapembe yao ni makali.
Ng'ombe hunolewa mapembe kwa kuwekwa viazi vya moto akiwa mvivu kujinoa mwenyewe.
Mbuzi ni mwoga sana wa maji usiombee mvua inyeshe ya nguvu ikakukuta machungoni ukataka kurudi na mifugo nyumbani, utapishana naye nchi 1 tu akiwa kwenye kichaka ila utapiga kelele hata kwa kilugha lakini huishia kukutizama tu usoni bila hata wasiwasi (lazima uloane au ukubali kuingia kwenye kichaka uchomwe na miba ili umtoe na akitoka hapo ataingia tena kwenye kichaka kingine yani ni pasua kichwa.
Ng'ombe akimzoea mkamuaji maziwa mmoja ni vigumu sana kusogelewa na Mtu mwingine la sivyo atamchoma mapembe na kumdhuru au kumuua. Bibi alipokuwa hayupo tulikuwa tunavaa nguo zake na kuimba nyimbo zake ili kumbembeleza akubali kukamuliwa maziwa.
Ng'ombe huogopa sana mvua ya upepo ambapo ukizubaa utawakuta hata km 10 mbali na machungoni ikiwa mvua ilikuwa nyingi sana na ya upepo huelekea huko huko kwenye upepo.
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Mpotezee tu, ila kingine ng'ombe huangaliwa sana na Mchungaji anapozaa asile ule mfuko wa uzazi aliomtolea ndama tumboni mwake, Mchungaji akichelewa tu ng'ombe akala basi huyo ng'ombe hufa mazima.Halafu kuna jamaa hapo ukimwambia anabisha eti uongo
MBWA.Wakuu
Tumekuwa tukifuga sana wanyama majumbani mwetu kwa miaka mingi hasa jamii za kiafrika.
Ingawaje tumekuwa tukiwatendea unyama uhuni wanyama tuwafugao.
Hapa nitaeleza kwa ufupi niliyoyajua na kuyaona kwa wanyama wa nyumbani hasa wafugwao na tabia zao ambazo ni very rare kuziona ..!
PUNDA.
Kwanza huyu hafugwi. Ndiyo HAFUGIKI. Why? Twende taratibu.
Panda amekuwa akifugwa kwa muda mrefu sana na binadamu
Akitumika kwa shughuli mbalimbali kama kulima.na kubeba mizigo mbalimbali.
Ingawaje kuna tabia zake ambazo ni rare sana kuziona utazijua tu punde ukimtendea vizuri yaani usiwe mkatili kwake.
Kwanza ana akili kuliko ng'ombe na wanyama wengine
Kuna kipindi wakati nipo mdogo kijijini kwetu Punda wetu baada ya kuona kazi nyingi sana mtindo mmoja na viboko vingi sana
Akaona bhana eeh! Chakufia nini? Akasepa zake kama miezi miwili hatumuoni.
Kumbe alikuwa kaenda tu nyumba nyengine usiku karuka zizi kaingia kukaa na ng'ombe katulia!
Mwenye mifugo kaamka asubuhi wala hajauliza sanaaa. Kampa chakula kidogo then kamuacha maana anajua wazi kabisa ukimpa kazi nyingi huyo punda anasepa zakeee..!
Baada ya miezi miwili usiku tena punda yule akarudi maskani kwa mtindo ule ule wa kuruka zizi asubuhi mnamkuta katulia zake ...!
Alipokuwa na ujauzito tulitegemea atazaa tu vizuri guess what??
Tuliona tu punda karudi kutokea porini hana tumbo kubwa tena na hana mtoto! Kamuacha wapi??
Ikabidi wazee wamzunguke na kuanza kumtandika viboko mfululizo mpaka punda yule alipoenda kuonesha alipomuacha mtoto ambapo tungechelewa tungekufa kajifia zake.
Najua unajua au hujui lakini punda anakula sana ukoko ukitaka ahamie kwako mazima mpe kila siku!
Next time nilipokuwa nimekaa tu kariba na zizi nikaona punda wetu mwengine aliyekuwa na mimba , anahangaika sana yaani hatulii !
Ukweli mimi yule punda alinipenda sana na hata nikiwa nimetulia alikuwa akinifuata na kuanza kusugua shingo yake miguuni mwangu , it was my best friend..!
Akanifuata mbio mbio then anageuka ananionesha mbususu yake, nikajua moja moja kwa huyu punda anataka kusaidiwa kujifungua na mimi bwana mdogo sikujua how to do it, ikabidi niwaite wajuzi waje kumsaidia mtoto atoke.. kwa kweli nilishuhudia namna wanyama wakizaa ni tabu tupu wanapata..!
Unatakiwa ujue kuwa punda ni mchungaji mzuri wa mifugo hasa ng'ombe na mbuzi, anaongoza njia na kuwaelekeza pa kupita mifugo sababu anakariri sana njia.
Pia anafukuza sana wanyama pori hasa fisi wanaokamata mbuzi [shughuli yake wanaijua vizuri]
NG'OMBE..
Huyu ni mnyama ambaye tuseme anashika nafasi ya pili kwa kuchinjwa akiongozwa na nguruwe!
Ng'ombe ni mnyama ambaye yuko so friendly na binadamu.
Iwapo tu ukimpenda na kumjali sio kila mara viboko noo
Kwa wasukuma.ni kawaida kukuta ng'ombe mmoja kavunjika pembe kwa viboko
Ng'ombe hawezi kujifungua mwenyewe au akiweza atazaa kwa tabu sana au ndama kufa!
Kama akikuozea sana atakufuata then atakeukia kukuonesha "bwana eeh mwanangu anataka kutoka nisaidie" then utatakiwa kumsaidia kumvuta ndama atoke [hili nimeshuhudia personal]
Watu wa dar kuleni nyama tu hivi hivi tu lakini mngejua namna wafugaji wanavyopata tabu.
Ndama anapotoka inatakiwa mmoja anyonye haraka kwenye pua'mdomo' maskio ili ndama asife otherwise mtampoteza..!
MBUZI
Huyu yeye anafugwa sana sana kwa kitoweo au biashara unakuta mtu kakwama anauza chap mbuzi mmoja kama 70k kutatua kamzozo fulani.
Mbuzi yeye ni muoga sana Hali inayopelekea kuwa na akili
Mara nyingi mbuzi hukaa zizini na mifugo mingine ili kusudi kutoa alert iwapo litatokea tatizo mfano fisi ameingia zizini ama lah
Yeye akiona tu labda kondoo amedakwa na fisi [fisi anapenda kondoo kuliko mbuzi] basi atapiga yowe "jamani baba mwenye nyumba eeh huku kuna muujiza tumevamiwa"
Na kikawaida mbuzi ana Saudi tofauti tofauti ndani ya mlio mmoja! Ndiyo' skia mzee iko hivi.
Mbuzi anatoa Sauti tofauti kabisa ikiwa kuna hatari' either akiona kitu ama akidakwa hata na fisi utajua tu.
Ana sauti ya maumivu, nk
Shida ya kondoo huwa nj jeuri hata akidakwa anataka kufa kiume halipigi kelele, ndio maana unasked watu wanasema kufa kikondoo hence muweke mbuzi na kondoo wakae zizi moja..
Unajua nini kuhusu wanyama?
Sasa kuna ndugu hapo alijisahau akamuacha ng'ombe ajifungue mwenyewe matokeo ndama akafaMpotezee tu, ila kingine ng'ombe huangaliwa sana na Mchungaji anapozaa asile ule mfuko wa uzazi aliomtolea ndama tumboni mwake, Mchungaji akichelewa tu ng'ombe akala basi huyo ng'ombe hufa mazima.
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Sio kweli miaka na miaka wazee wamefanya hivyo na wapo tuHiyo ya kumnyonya ndama kwa mdomo mnajiweka kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa, ni bora kumning'iniza kwa kumnyanyua miguu ya nyuma ili majimaji yachuruzike kutoka puani, kumpangusa pua na kitambaa na hata kumumwagia maji ya baridi ili aanze kupumua vizuri.
Vizuri mkuu ila yupi anakupa faida mapema..? More risk more profit.... chukua hiyo broKuku mimi sifugi hawana ishu
Hawawezi kustahimili mazingira magumu
Wepesi sana kushikwa na magonjwa kama mdonde
Wakinyeshewa tu na maji sana hata kufa anakufa ..!
Siwezi kuhimili hiyo pressure
Changia ujualo na wewe mkuuUzi moto sana huu, kuna wakati huwa nawatathmini wanyama nasema kweli Mungu fundi.
Mie experience yangu labda kwa kuku tu na mbwa ndo nimewafuga kwa muda mrefu sana.Changia ujualo na wewe mkuu
Maelezo mengi ila hujaeleza chochote kuonesha uongo wa mtoa Uzi dhidi ya ukweli wako, ndo nini sasa!Mengi hapa siyo ukweli. Yaani umefikia conclusion kwa mambo machache ambayo inaonekana na wewe ulisimuliwa au umekopi mahali na kuleta hapa. Utawapata tu hao hao waliozaliwa mjini na hawajui maisha ya hawa wanyama. Sisi wengine tuliozaliwa vijijini wanyama kama hawa walikuwa ni sehemu ya maisha yetu.