Paka na mmbwa huwa hawapotei kabisa wakisafirishwa hata umbali gani ilimradi uwe mji huo huo..
1990s tulishawahi kuweka paka mmoja kwenye boksi kisha tukamsafirisha mbali sana kama km 70 alitupwa bwawani maana alikuwa anadokoa mno mboga jikoni na kunya hovyo hovyo, baada ya siku 4 tulipofungua mlango asubuhi 06:00 hrs alikutwa akiwa amelala nnje ya mlango mkuu wa nyumba.
Mmbwa, Poppy mbegu ya kizungu aliyotoka nayo Mzee Brazil na kuifuga Morogoro, alikuwa mkali sana na alisababisha majeraha kwa wanafunzi na baadhi ya Watu. Alikuwa anakodishwa kuwinda wanyama porini ila bado alileta balaa. Mshua aliamua kumuuzia Rafiki yake kuepuka balaa aliyekuwa akiishi umbali kama km 52 ila baada ya wiki 1 mmbwa alitoroka na kurudi home.
Paka anafundishika tabia njema ila usijichanganye kumfungia ndani ukiwa pekeyako eti umpige, atakuua na usijesema sikukuambia tukikutana paradiso.
Sent from my CPH2387 using
JamiiForums mobile app