Undani wa point pendwa ya Sarajevo assassination.

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2017
Posts
1,937
Reaction score
3,718
"Sophie! Sophie usife ishi kwa ajili ya watoto wetu".yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Archiduke Franz Ferdinand tarehe 28 June mwaka 1914 akiwa anakata roho baada ya kupigwa risasi.Akimtaka mkewe asife ili alee watoto ambaye naye alikuwa anahangaika kukata roho kwa kupigwa risasi.Ombi lake halikutimia kwa sababu wote walikata roho na kufariki siku hiyo hiyo katika mji wa Sarajevo Bosnia.Lakini kwa nini mtu aliyeheshimika tena aliyetokea familia ya kifalme afe kinyonge tena mchana kweupe kiasi hiki?

Archiduke Franz Ferdinand alizaliwa tarehe 18 December 1863 huko Graz Austria.Alikuwa mtoto wa kwanza wa Archduke Karl Ludwig ambaye alikuwa mdogo wake na mtawala wa Austria-hungary kwa wakat huo Franz Joseph.Akiwa na miaka 12 tu alianza mafunzo ya kijeshi mpaka kufikia kuwa major general alipofikisha miaka 31.Kifo cha mtoto wa pekee wa Franz Joseph aliyejiua mwaka 1863 kilimpatia nafasi kubwa ya kurithi utawala wa Austria-Hungary kutoka kwa Franz Joseph.Mwaka 1894 alianzisha mahusiano ya kimapenzi na Sophie Chottek na walioana July 1900.Archiduke Franz Ferdinand alipata watoto watatu na mkewe mpaka kifo kilipomkuta mwaka 1914.Lakini kwa nini apigwe risasi?

Uturuki kwa karne nyingi iliitawala Serbia tokea mwaka 1459 na Waserbia walianzisha mapambano mengi ili waondokane na utawala huo lakini haikuwezekana.Kuanzia mwaka 1912-1913 Warsebia kwa kushirikiana na Wagiriki na Wabulgaria walitimiza ndoto yao ya kujiondoa katika utawala wa Waturuki baada ya kuwashinda katika vita vya Balkan.Kutokana na ushindi huo majimbo ya watu wanaotumia lugha ya slav kama old Serbia,Macedonia etc yakawa chini ya nchi ya Serbia isipokuwa Bosnia na Harzegovina yaliyokuwa chini ya Austria-Hungary.Austria-hungary ilianza kuitawala Bosnia mwaka 1876 baada ya makubaliano na Urusi lakini miaka miwili baadae katika Berlin congress iliongezewa na Herzegovina hivyo kuanza kuyatawala haya majimbo yote mawili.

Serbia iliyachukulia Majimbo haya kama sehemu ya nchi yao hivyo wazalendo wa nchi hiyo walijaribu kufanya kila linalowezekana kubadilisha Bosnia na Harzegovina zinakuwa huru na kuwa sehemu ya Serbia.Utawala wa Austria-hungary kwa haya majimbo ulikuwa na uonevu mkubwa mfano watu wa Bosnia walizuiwa kusherekea siku kuu ya miungu yao iliyojulikana kama Sava's day.Pia walizuiwa kuimba wimbo wao Serbia folk song.hayo yote yalikuwa na uafadhari, mwaka 1908 walifanya kosa kubwa sana baada ya Austria-hungary kuamua kuyafanya majimbo hayo kuwa sehemu ya nchi yake.Hilo jambo lilipingwa vikali na Waserbia.

KUANZISHWA KWA UMOJA WA BLACK HAND.

Mojawapo ya watu waliopingana na uamuzi wa Austria-hungary alikuwa ni kiongozi wa jeshi Captain Dragutin Dimitrijev aliyekuwa maarufu kwa jina la "Apis".Kiongozi huyu aliazimia ni lazima ayarudishe majimbo haya Serbia.hivyo akaanzisha umoja mwaka 1911 uliojulikana kama "union or death" lakini baadae ulikuja kubadilisha jina ukajiita "Black hand".umoja huu ulikuwa na malengo makuu mawili.Kwanza,Kutengeneza utawala imara wa Serbia utakaounganisha Warsebia wote.Pili,Kila mwanachama lazima asaini fomu na kukubali kupoteza maisha yake ili malengo ya muungano yaende mbele.

Mwaka 1914 Austria-hungary ilitangaza ingefanya maonyesho ya kijeshi karibu na mpaka wa Serbia.Hii Waserbia ikiwemo muungano wa black hand uliokuwa umeimarika sasa walitafsiri hatua hiyo kama vitisho kwa nchi yao.Na ilipotangazwa tarehe 28 June mwaka huohuo kwamba archiduke Ferdinand angetembelea Bosnia katika mji wa Sarajevo ilizidisha hasira zaidi ukizingatia siku hiyo ilikuwa ni ya kihistoria kwa nchi ya Serbia wakikumbuka mapigano ya Kosovo yaliyofanyika mwaka 1389 wakipigana na waturuki .Kulikuwa na vitisho vilivyomtaka Ferdinand aahirishe safari yake lakini alivipuuzia.Wakati huo yeye akipuuzia nyuma ya pazia watu walikuwa serious wakipanga kummaliza.

Siku chache kabla ya tukio kijana wa miaka kumi na tisa aliyekuwa mwanachama wa kikundi cha Mlada(young Bosnia) kilichokuwa cha vijana wazalendo waliokuwa wanaumizwa na matendo ya uonevu yanayofanywa na Austria-Hungary dhidi ya Serbia.Alipewa siraha na chama cha black hand asafiri mpaka Bosnia akamuue Ferdinand.Lakini viongozi wa black hand waliongeza tena vijana wengine wawili wasaidiene.Kijana huyo aliitwa Gavrilo Princip wenzake ni Nedjeliko Carbonovic na Trifko Grabez.Walipewa masharti atakaefanikiwa kumuua na yeye ajiue.Lakini pia waliambiwa wakifika Bosnia wataungana na wengine wanne.Vijana hao walisafiri mpaka Bosnia tayari kwa kazi.

Siku ya tukio Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie walifika kwa treni wakipokelewa na umati mkubwa wa watu.Lakini ndani ya umati ule walikuwemo wauaji nao wamejipanga mmoja mmoja kuanzia kwenye kituo cha treni mpaka ukumbini ambapo angehutubia.Baada ya kushuka kwenye treni alikuwa na msafara wa magari sita huku la kwake likiwa la pili.Ghafla lilirushwa bomu lakini kwa bahati dereva alilikwepa likaipiga gari ya mbele likajeruhi watu wawili.Bomu hilo lilirushwa na Nedjelko Cabrinovic.Alipoaingia ukumbini alitukana sana kwa kukoswa na bomu akaahidi baadae angeenda kuwaona majeruhi.

Wakati anaanza kuondoka ili aende ukumbini aliamuru wapite njia isiyo ya katikati ya mji ili kukwepa umati wa watu.Dereva alipokata kona kuifuata hiyo njia pasipo kujua ndio upande aliokuwepo Gavrilo Princip hapo hapo aliwashambulia kwa risasi Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie wakafa palepale.
Lakini wakati anataka kujiua maaskari waliwahi kumkamta.

Tukio hili la kuuliwa Kwa Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie Chottek lilipelekea kuanza kwa vita ya kwanza ya dunia.Wengi tumeitumia sana hii point ya Sarajevo assasination shuleni kwenye somo la history katika causes of first world war.Huu ndio undani wake mambo yalivyokuwa.

Asanteni.
 
Ombi kwa mods naomba huu Uzi muuhamishie jukwaa la intelligence.
 
Hii point kwenye causes of first world war nliandika ya kwanza hii Sarajevo double marder
 
Mmh . Sioni point hapo yaani wewe umuue adui halafu na wewe ujiue? Unafaidika nini sasa?
 
Mmh . Sioni point hapo yaani wewe umuue adui halafu na wewe ujiue? Unafaidika nini sasa?
Mkuu labda umeelewa tofaut hii sarajevo assasination ni point maarufu ya causes of first world war.waliosoma history form four wanaijuavizuri

Ndo msingi wa title
 
Umenifundisha kitu mkuu...
Ngoja nipange Hivi kutoka mwanzo kurudi nyuma..

WW1>>>>>>Black hand>>>>Rosthchild Familly>>>>>Illuminat>>>>Nephellism bloodline>>>>>>RUCIFER.
 
Shukurani kwa kuuleta usomi huu wa historia katika lugha ya Kiswahili.

Kuna mjadala mkubwa kwa wanahistoria kujadili kama mauaji haya ndiyo yalisababisha vita vikuu vya kwanza, au yalikuwa ni catalyst tu iliyofanya chain reaction ianze mapema.

Kwa vyovyote, mauaji haya yalikuwa sehemu muhimu katika kuanza kwa Vita Vikuu vya kwanza vya dunua. Inawezekana kabisa.

Mauaji haya yasingetokea.

1. Vita vikuu vya kwanza visingetokea, au visingetokea kama vilivyotokea.

2. Mapinduzi ya Kibolsheviki Urusi yasingetokea, au yasingetokea kama yalivyotokea.

3. Kwa sababu Vita Vikuu vya Pili mwanzo wake uliendana sana na matokeo na mijataba ya Vita Vikuu vya Kwanza, basi kama Vita VikuuVya Kwanza visingetokea au visingetokea kama vilivyotokea, vya pili visingetokea au visingetokea kama vilivyotokea.

4. Kwa sababu wimbi la makoloni kudai Uhuru lilikuja baada ya matokeo ya Vita Vikuu vya Pili vya dunia (kisiasa na kiuchumi zaidi) i gewezekana kabisa kwamba bila ya Vita hizi kupiganwa, nchi nyingi za Aftika zingekuwa makoloni ya wazungu kwa miaka mingi zaidi ya ilivyokuwa. Wazungu waliona kuna matatizo ya gharama nyingi za kuendesha makoloni baada ya vita, na Waafrika wengi wakaamka kuona wazungu wanapigika baada ya vita, mambo haya mawili yalipangana vizuri jufanya wazungu wayaoe makoloni uhuru wa bendera huku wakijipanga kuyaendesha kwa mbali kutumia ukoloni mamboleo.

Kifupi, bila mauaji haya, dunia ingeweza kuwa tofauti sana leo.
 
Hii point ya Assassination of archiduke Ferdinand in Sarajevo the capital city of Bosnia. Ilinipatia marks nying kwenye HGL yangu. Nilikua naipenda sana hii point enzi hizo. Ck hizi kwa sababu ya kutofuatilia tena haya mambo nimeshaanza kusahau. Lakin nchi ya Bosnia & Herzegovina huwa naihusisha zaidi na Mshambuliaji wa zaman wa Manchester City Ila kwa sasa akikipiga ktk timu ya Roma pale Italy akijulikana km Eden Dzeko, streika asiyekuwa na spidi lakini anatupia sana kambani pale Italy.
 
Umenifundisha kitu mkuu...
Ngoja nipange Hivi kutoka mwanzo kurudi nyuma..

WW1>>>>>>Black hand>>>>Rosthchild Familly>>>>>Illuminat>>>>Nephellism bloodline>>>>>>RUCIFER.
Umeshaanza mambo yako ya conspiracy[emoji23]
 
Inaonekana vita vya kwanza na vya pili vya dunia viliisaidia sana Africa.Japo bado tunahangaika na ukoloni mambo Leo.
 
Inaonekana vita vya kwanza na vya pili vya dunia viliisaidia sana Africa.Japo bado tunahangaika na ukoloni mambo Leo.
Vita hizi ziliisaidia Afrika kwa namna mbili.

1. Zilifanya nchi za Ulaya zilizopigana vita kudhoofika kiuchumi na kufarakana kisiasa na kuona kwamba kuendesha makolonini gharama sana. Wakoloni walizoea kuwagawanya waafrika na kuwatawala (divide and rule), mkutano wa Berlin ulifanikiwa kwa kiasikikubwa kuwafanya wakoloni wagawane Afrika bila vita kubwa. Sasa wakoloni wenyewe walipogawanyika na kupigana vita, udhaifu wao ukaweza kuonekana vizuri zaidi.

2.Waafrika walioenda kupigana vita waliona kwamba wakoloni nao ni watu tu, wanapigwa vitani. Waliona kwa nini tunawapigania wao wakati wanatutawala? Na kama tunaweza kupigana vita kwa niaba yao, kwanini tusipiganie uhuru wa nchi zetu? Hapo ndipo utaona kwamba, watu waliotoka vitani, huko kwetu watu kama kina Sykes, waliporudi nyumbani walileta vuguvugu jipya la kudai uhuru. Japo wa bendera.
 
Safi sana mkuu ulivo andika uko sawa kabisa....nakumbuka stori kama hii niliwai soma kwenye kitabu kinaitwa the world history mwandishi ni winsel lewinsk....so exactly kabisa big up mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…