Undani wa point pendwa ya Sarajevo assassination.

Undani wa point pendwa ya Sarajevo assassination.

"Sophie! Sophie usife ishi kwa ajili ya watoto wetu".yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Archiduke Franz Ferdinand tarehe 28 June mwaka 1914 akiwa anakata roho baada ya kupigwa risasi.Akimtaka mkewe asife ili alee watoto ambaye naye alikuwa anahangaika kukata roho kwa kupigwa risasi.Ombi lake halikutimia kwa sababu wote walikata roho na kufariki siku hiyo hiyo katika mji wa Sarajevo Bosnia.Lakini kwa nini mtu aliyeheshimika tena aliyetokea familia ya kifalme afe kinyonge tena mchana kweupe kiasi hiki?

Archiduke Franz Ferdinand alizaliwa tarehe 18 December 1863 huko Graz Austria.Alikuwa mtoto wa kwanza wa Archduke Karl Ludwig ambaye alikuwa mdogo wake na mtawala wa Austria-hungary kwa wakat huo Franz Joseph.Akiwa na miaka 12 tu alianza mafunzo ya kijeshi mpaka kufikia kuwa major general alipofikisha miaka 31.Kifo cha mtoto wa pekee wa Franz Joseph aliyejiua mwaka 1863 kilimpatia nafasi kubwa ya kurithi utawala wa Austria-Hungary kutoka kwa Franz Joseph.Mwaka 1894 alianzisha mahusiano ya kimapenzi na Sophie Chottek na walioana July 1900.Archiduke Franz Ferdinand alipata watoto watatu na mkewe mpaka kifo kilipomkuta mwaka 1914.Lakini kwa nini apigwe risasi?

Uturuki kwa karne nyingi iliitawala Serbia tokea mwaka 1459 na Waserbia walianzisha mapambano mengi ili waondokane na utawala huo lakini haikuwezekana.Kuanzia mwaka 1912-1913 Warsebia kwa kushirikiana na Wagiriki na Wabulgaria walitimiza ndoto yao ya kujiondoa katika utawala wa Waturuki baada ya kuwashinda katika vita vya Balkan.Kutokana na ushindi huo majimbo ya watu wanaotumia lugha ya slav kama old Serbia,Macedonia etc yakawa chini ya nchi ya Serbia isipokuwa Bosnia na Harzegovina yaliyokuwa chini ya Austria-Hungary.Austria-hungary ilianza kuitawala Bosnia mwaka 1876 baada ya makubaliano na Urusi lakini miaka miwili baadae katika Berlin congress iliongezewa na Herzegovina hivyo kuanza kuyatawala haya majimbo yote mawili.

Serbia iliyachukulia Majimbo haya kama sehemu ya nchi yao hivyo wazalendo wa nchi hiyo walijaribu kufanya kila linalowezekana kubadilisha Bosnia na Harzegovina zinakuwa huru na kuwa sehemu ya Serbia.Utawala wa Austria-hungary kwa haya majimbo ulikuwa na uonevu mkubwa mfano watu wa Bosnia walizuiwa kusherekea siku kuu ya miungu yao iliyojulikana kama Sava's day.Pia walizuiwa kuimba wimbo wao Serbia folk song.hayo yote yalikuwa na uafadhari, mwaka 1908 walifanya kosa kubwa sana baada ya Austria-hungary kuamua kuyafanya majimbo hayo kuwa sehemu ya nchi yake.Hilo jambo lilipingwa vikali na Waserbia.

KUANZISHWA KWA UMOJA WA BLACK HAND.

Mojawapo ya watu waliopingana na uamuzi wa Austria-hungary alikuwa ni kiongozi wa jeshi Captain Dragutin Dimitrijev aliyekuwa maarufu kwa jina la "Apis".Kiongozi huyu aliazimia ni lazima ayarudishe majimbo haya Serbia.hivyo akaanzisha umoja mwaka 1911 uliojulikana kama "union or death" lakini baadae ulikuja kubadilisha jina ukajiita "Black hand".umoja huu ulikuwa na malengo makuu mawili.Kwanza,Kutengeneza utawala imara wa Serbia utakaounganisha Warsebia wote.Pili,Kila mwanachama lazima asaini fomu na kukubali kupoteza maisha yake ili malengo ya muungano yaende mbele.

Mwaka 1914 Austria-hungary ilitangaza ingefanya maonyesho ya kijeshi karibu na mpaka wa Serbia.Hii Waserbia ikiwemo muungano wa black hand uliokuwa umeimarika sasa walitafsiri hatua hiyo kama vitisho kwa nchi yao.Na ilipotangazwa tarehe 28 June mwaka huohuo kwamba archiduke Ferdinand angetembelea Bosnia katika mji wa Sarajevo ilizidisha hasira zaidi ukizingatia siku hiyo ilikuwa ni ya kihistoria kwa nchi ya Serbia wakikumbuka mapigano ya Kosovo yaliyofanyika mwaka 1389 wakipigana na waturuki .Kulikuwa na vitisho vilivyomtaka Ferdinand aahirishe safari yake lakini alivipuuzia.Wakati huo yeye akipuuzia nyuma ya pazia watu walikuwa serious wakipanga kummaliza.

Siku chache kabla ya tukio kijana wa miaka kumi na tisa aliyekuwa mwanachama wa kikundi cha Mlada(young Bosnia) kilichokuwa cha vijana wazalendo waliokuwa wanaumizwa na matendo ya uonevu yanayofanywa na Austria-Hungary dhidi ya Serbia.Alipewa siraha na chama cha black hand asafiri mpaka Bosnia akamuue Ferdinand.Lakini viongozi wa black hand waliongeza tena vijana wengine wawili wasaidiene.Kijana huyo aliitwa Gavrilo Princip wenzake ni Nedjeliko Carbonovic na Trifko Grabez.Walipewa masharti atakaefanikiwa kumuua na yeye ajiue.Lakini pia waliambiwa wakifika Bosnia wataungana na wengine wanne.Vijana hao walisafiri mpaka Bosnia tayari kwa kazi.

Siku ya tukio Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie walifika kwa treni wakipokelewa na umati mkubwa wa watu.Lakini ndani ya umati ule walikuwemo wauaji nao wamejipanga mmoja mmoja kuanzia kwenye kituo cha treni mpaka ukumbini ambapo angehutubia.Baada ya kushuka kwenye treni alikuwa na msafara wa magari sita huku la kwake likiwa la pili.Ghafla lilirushwa bomu lakini kwa bahati dereva alilikwepa likaipiga gari ya mbele likajeruhi watu wawili.Bomu hilo lilirushwa na Nedjelko Cabrinovic.Alipoaingia ukumbini alitukana sana kwa kukoswa na bomu akaahidi baadae angeenda kuwaona majeruhi.

Wakati anaanza kuondoka ili aende ukumbini aliamuru wapite njia isiyo ya katikati ya mji ili kukwepa umati wa watu.Dereva alipokata kona kuifuata hiyo njia pasipo kujua ndio upande aliokuwepo Gavrilo Princip hapo hapo aliwashambulia kwa risasi Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie wakafa palepale.
Lakini wakati anataka kujiua maaskari waliwahi kumkamta.

Tukio hili la kuuliwa Kwa Archiduke Ferdinand na mkewe Sophie Chottek lilipelekea kuanza kwa vita ya kwanza ya dunia.Wengi tumeitumia sana hii point ya Sarajevo assasination shuleni kwenye somo la history katika causes of first world war.Huu ndio undani wake mambo yalivyokuwa.

Asanteni.

Ni kwann walikuwa na sharti la kujiua baada ya kumuua Archduke?

Hii point umenikumbusha history enzi hizo.....
 
Safi sana mkuu ulivo andika uko sawa kabisa....nakumbuka stori kama hii niliwai soma kwenye kitabu kinaitwa the world history mwandishi ni winsel lewinsk....so exactly kabisa big up mkuu
Yap hiko ni mojawapo ya kitabu ambacho ni source ya hii habari.Sema nimesahau tu ku acknowledge.Asante mkuu

Vile vile kwa wanaopenda kujisomea hicho kitabu ni kizuri sana kuelewa historia kubwa ya dunia.
 
Ni kwann walikuwa na sharti la kujiua baada ya kumuua Archduke?

Hii point umenikumbusha history enzi hizo.....
Kiukweli sijui sababu hasa ilikuwa ni nini.Japo alipohojiwa muuaji ndivyo alivyosema waliambiwa atakayefanikiwa kumuua na yeye .
.ajiue

Ila nadhan inawezekana Lengo lilikuwa ni kutunza siri.
 
Kiukweli sijui sababu hasa ilikuwa ni nini.Japo alipohojiwa muuaji ndivyo alivyosema waliambiwa atakayefanikiwa kumuua na yeye .
.ajiue

Ila nadhan inawezekana Lengo lilikuwa ni kutunza siri.
Mh bado maana kama ni kutunza siri kuna wengine walikuwa pamoja sio yeye mwenyewe alotumwa.

Nakumbukq walkuwa kam wanne. Hawa wasingeweza kutoa siri?
 
Vita hizi ziliisaidia Afrika kwa namna mbili.

1. Zilifanya nchi za Ulaya zilizopigana vita kudhoofika kiuchumi na kufarakana kisiasa na kuona kwamba kuendesha makolonini gharama sana. Wakoloni walizoea kuwagawanya waafrika na kuwatawala (divide and rule), mkutano wa Berlin ulifanikiwa kwa kiasikikubwa kuwafanya wakoloni wagawane Afrika bila vita kubwa. Sasa wakoloni wenyewe walipogawanyika na kupigana vita, udhaifu wao ukaweza kuonekana vizuri zaidi.

2.Waafrika walioenda kupigana vita waliona kwamba wakoloninaoni watu tu, wanapigwa vitani. Waliona kwa nini tunawapigania wao wakati wanatutawala? Na kama tunaweza kupigana vita kwa niaba yao, kwanini tusipiganie uhuru wa nchi zetu? Hapondipo utaona kwamba, watu waliotoka vitani, hukokwetu watu kama kina Sykes, waliporudi nyumbani walileta vuguvugu jipya la kudai uhuru. Japo wa bendera.

namba 2 returning of ex-soldiers like Dedan Kimathi and Warihui Itote (General China)
 
imediate cause au short term, long term au basic causes ni formation of allience, militarism, fear of revange, balance of power nk. kipind hicho nlkua nondo balaa. Thanx mtoa mada
 
Mwandishi asante kwa andiko lako japo hujasema ni kwa nini vita ya dunia ianze kwa sababu ya kifo cha huyo jamaa na mkewe. Washirika wa hiyo vita wanahusiana vipi na marehemu Franz?
Hii pekee haikuwa sababu ya kuwepo kwa vita vya dunia ila ilikuwa kama kichocheo cha kuanza kwa vita.Kwa ufupi ipo hivi

Kipindi hicho nchi za ulaya zilikuwa katika migogoro mikubwa sana.Mfano Ufaransa alikuwa na mgogoro na Ujerumani kwa sababu Ujerumani aliishinda Ufaransa katika vita ya Franco-Prussian war mwaka 1870 na Ufaransa kunyang'anywa makoloni yake mhimu ya Alsace na Lorraine.

Lakini kibaya zaidi kulikuwa na miungano ya majeshi(millitary alliances) ya nchi mbali mbali.Kulikuwa na Tripple entente ya Uingreza,Ufaransa na Urusi.Vilevile Tripple alliance iliyohusisha Ujerumani,Italia na Austria-hungary.Hili lilikoleza moto zaidi.

Kumbuka Archiduke alitokea familia ya kifalme na alitegemewa kuwa mtawala wa Austria-hungary baada ya kifo cha Franz Joseph.Hivyo kifo chake kiliikasirisha Austria-hungary wakaanzisha vita dhidi ya Serbia wakidai serikali ilihusika kumuua.Kwa sababu Austria-hungary alikuwa katika umoja wa majeshi na Ujerumani ikabidi Ujerumani aje kumsaidia Austria-Hungary.Kitendo hicho kiliikasirisha Urusi ikaona Serbia inaonewa nayo ikaamua kuisaidia Serbia.Kama nilivyokuambia mwanzoni juu ya ugomvi uliokuwepo kati ya Ufaransa na Ujerumani.Hivyo Ufaransa akaona ndiyo fursa pekee ya kulipiza kisasi na kurudisha makoloni naye akaingilia vita akiwa upande wa Serbia na Urusi.Kumbuka Uingereza naye alikuwa kwenye muungano wa kijeshi na Ufaransa na Urusi hivyo nae hakukaa mbali akaamua kuwasaidia wa upande wake.hivyo ndivyo vita ilivyoanza na ndio tukio hili lilivyochochea.
 
Inaonekana vita vya kwanza na vya pili vya dunia viliisaidia sana Africa.Japo bado tunahangaika na ukoloni mambo Leo.
Mkuu kwanini ziitwe vita ya dunia wakati zimepiganwa na wazungu peke yao??? Huko america ya kusini hta haikurushwa risasi au ndio wazungu wanatuburuza
 
Mkuu kwanini ziitwe vita ya dunia wakati zimepiganwa na wazungu peke yao??? Huko america ya kusini hta haikurushwa risasi au ndio wazungu wanatuburuza
Hata watu wa Dar wanadai Dar es salaam ndio Tanzania.Sijui sisi tulio nanjilinji,Simiyu,Mpanda na Kakonko tupo nchi gani.

Tuwavumilie tu hawa wazungu.
 
Hii pekee haikuwa sababu ya kuwepo kwa vita vya dunia ila ilikuwa kama kichocheo cha kuanza kwa vita.Kwa ufupi ipo hivi

Kipindi hicho nchi za ulaya zilikuwa katika migogoro mikubwa sana.Mfano Ufaransa alikuwa na mgogoro na Ujerumani kwa sababu Ujerumani aliishinda Ufaransa katika vita ya Franco-Prussian war mwaka 1870 na Ufaransa kunyang'anywa makoloni yake mhimu ya Alsace na Lorraine.

Lakini kibaya zaidi kulikuwa na miungano ya majeshi(millitary alliances) ya nchi mbali mbali.Kulikuwa na Tripple entente ya Uingreza,Ufaransa na Urusi.Vilevile Tripple alliance iliyohusisha Ujerumani,Italia na Austria-hungary.Hili lilikoleza moto zaidi.

Kumbuka Archiduke alitokea familia ya kifalme na alitegemewa kuwa mtawala wa Austria-hungary baada ya kifo cha Franz Joseph.Hivyo kifo chake kiliikasirisha Austria-hungary wakaanzisha vita dhidi ya Serbia wakidai serikali ilihusika kumuua.Kwa sababu Austria-hungary alikuwa katika umoja wa majeshi na Ujerumani ikabidi Ujerumani aje kumsaidia Austria-Hungary.Kitendo hicho kiliikasirisha Urusi ikaona Serbia inaonewa nayo ikaamua kuisaidia Serbia.Kama nilivyokuambia mwanzoni juu ya ugomvi uliokuwepo kati ya Ufaransa na Ujerumani.Hivyo Ufaransa akaona ndiyo fursa pekee ya kulipiza kisasi na kurudisha makoloni naye akaingilia vita akiwa upande wa Serbia na Urusi.Kumbuka Uingereza naye alikuwa kwenye muungano wa kijeshi na Ufaransa na Urusi hivyo nae hakukaa mbali akaamua kuwasaidia wa upande wake.hivyo ndivyo vita ilivyoanza na ndio tukio hili lilivyochochea.
Jamaa history ulipiga fresh coz unashusha nondo kama ilivyo na watu tunakuelewa big up.
 
Back
Top Bottom