Ungana nami leo ujifunze kutumia RCS Chats, mbadala wa WhatsApp katika kifaa chako cha Android

Ungana nami leo ujifunze kutumia RCS Chats, mbadala wa WhatsApp katika kifaa chako cha Android

Kwa waandishi wa habari hasa za uchunguzi, au mtu yeyote anaejali privacy, hii app siyo yakutumia, haina encryption kama whatsapp, japo ni nzuri.
kivipi mkuu
 
Kwa waandishi wa habari hasa za uchunguzi, au mtu yeyote anaejali privacy, hii app siyo yakutumia, haina encryption kama whatsapp, japo ni nzuri.
Privacy kila kona kwani unajihusisha na shughuli haramu mkuu?
 
Je, unatumia kifaa cha Android?

Je, unatafuta mbadala wa WhatsApp baada ya kuitumia kwa muda mrefu?

Ndiyo, inawezekana, ukiwa na Kifaa cha Android iwe Simu, Tablet huna ulazima wa ku download App ya WhatsApp, unaweza kupata Features zote za WhatsApp ikiwemo kutuma Picha, Video, GIF, Poll, Files, Voice na nyinginezo nyingi pasipo kutumia WhatsApp

Hatua ya Kwanza
Download Google Messenger, kama tayari unayo, hakikisha kama ndiyo hiyo kwa kubofya link hii


Baada ya ku download fungua na ifanye Default App yako ya SMS

Hatua ya Pili ni Verification



Nenda Settings
View attachment 3314902



Messages Settings
View attachment 3314903



Nenda General
View attachment 3314904



Nenda RCS Chats
View attachment 3314906



Washa RCS Chats, Verify namba utakayotumia, kama unazo mbili Verify Zote kama mimi, Washa Send Read Recipient, Washa Typing indicator, Washa Auto download file while roaming ikiwa utakuwa kwenye mazingira ya roaming network basi uendelee kama kawaida
View attachment 3314908
View attachment 3314910



Baada ya hapo Tazama namba ya Rafiki yako ambaye ameshajiunga pia, Chat naye, tuma Picha, Video na mambo mengine yataenda kama WhatsApp,

Feature hii utatumia MB badala ya SMS ni sawa na WhatsApp

Kufahamu kama namba ya rafiki yako imejiunga utaona RCS uwanja wa typing
View attachment 3314911
Na mimi natumia Yas ila inasema mtandao hau support rcs
Screenshot_20250917-075503_Messages.jpg
 
Kwa waandishi wa habari hasa za uchunguzi, au mtu yeyote anaejali privacy, hii app siyo yakutumia, haina encryption kama whatsapp, japo ni nzuri.
WhatsApp yenyewe encryption yake magumashi tu na wamefanikiwa kuwapumbaza watu hapo......Telegram kidogo hapo utakua umejificha , ndo maana Ufaransa walimkamata mmiliki wake maana walikua wanashindwa kudukua, ila WhatsApp kama kweli una issue sensitive hujikingi na kitu labda tu hapa kwetu sababu utaalam sio mkubwa ila WhatsApp nayo inadukuliwa vizuri na mambo yako yanafatiliwa
 
Binafsi ninatumia Samsung S25U line 2. Line one ni YAS, inakataa ku connect, inasema changamoto iko Mtandao wa YAS hausapoti hiyo feature, wakati kabla sija nunua S25U nlikuwa na GALAXY A55, ilikuwa inasaport line zote 2 vzuri tu. Nimejaribu kuingia kwenye international forums, nikakuta watumiaji wengi wa S25U wanalalamikia tatizo hili line moja kushindwa ku-connect RCS features.

Hivyo kuonekana kama vile S25U zina hiyo changamoto. Wengi wameamua kuziacha na ku-upgrade kwenda S26U.

Kama kuna mwingine mwenye hii changamoto naomba tufahamiane.
 

Attachments

  • Screenshot_20260708_035233_Messages.jpg
    Screenshot_20260708_035233_Messages.jpg
    208.2 KB · Views: 13
Back
Top Bottom