Ungekuwa kwenye nafasi hii, ungefanya maamuzi yapi?

Ungekuwa kwenye nafasi hii, ungefanya maamuzi yapi?

Carleen

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
7,982
Reaction score
27,272
Hi guys,

Mnawe kwa maji tiririka, mvae barakoa, mkunywe maji ya tangawizi na limao na mjifukize, narudia tena mpige nyungu..! (Msopenda thread ndefu sitotaka malalamiko, tafadhali beba tu huu ushauri na uende)

Enwei, kuna mpendwa wangu mmoja alikuwa ana date this gentleman for so long, lakini unluckily hakuwahi kujua kama this guy tayari alishapata mtoto na binti mwingine way back na mtoto yupo nyumbani kwao kijana.!

Kuna kipindi huyu kaka akawa anaforce huyu binti aende nyumbani kwao, (siyo ile official lakini) anataka aende tu kusalimia, binti akawa anagoma anahisi ni mapema sana lakini this guy akatumia ushawishi mpaka akamu win over,

Binti akafika kwa wazazi akatambulishwa kama rafiki, sababu ilikuwa ni mapema mno kwao wote wawili kusema tofauti, lakini binti alishangaa baada ya kukuta kuna this beautiful baby boy kafanana kweli na mpenzi wake, alikuwa anafanya home work, bad enough akampelekea the guy lile daftari huku akimuita 'Baba'.!!

This girl alikuwa startled, akamuuliza jamaa yake, na the guy akakubali kuwa he is my son, and issa only reason nilitaka uje nyumbani ufahamu hili nilishindwa kukuambia moja kwa moja, usingenielewa! to cut a long story short, binti alimaindi ila akaja kuelewa, and life goes on..!

Kama vile ambavyo hakuna aijuaye kesho, after a while this guy akapata mchongo ambao ulimlazimu awe nje ya nchi for like two years, every thing sorted out and the girl promised to wait..!!

The guy kweli akafanikiwa kusepa, after few months yakatokea ya kutokea wakapotezana hewani,(I think the guy did it purposely), hivyo kila mmoja akawa anaishi bila taarifa za mwenzie, Binti akaja akapata this very caring man (kwanini wanaume ambao huwa ni vifaa vya watu wanajua kujali hivyo eti.?), wakaanza safari ya mahusiano, 'asiyekuwepo machoni na moyoni sijui nini' naskia walisemaga waswahili.!!

Hapa kweli nikaamini shetani yupo na anatenda kazi yake kwa weledi, this girl got preggy, na baba yake mzazi ni mkali hiyo wanayoita pilipili kichaa irudi shule ikasome, kumuambia this man akasema 'I am sorry that I didn't tell you, I got a family, I've already married few years back, nipo tayari nitalea ila I don't have any other future plans with you honestly'..!

Hii maumivu yake ni maradufu kuliko ile ya kujigonga ukucha na pembe ya kitanda (I'm just saying najua vile inauma), maybe issa karma who knows, this man akaenda kwa kina binti akasema ukweli, Mzee akawaka mwisho wa siku akakubali matokeo kuwa haya maji hayazoleki, wacha tu yakauke.!

Binti akajifungua nyumbani kwao, mtoto kakua kua kamuacha kwa wazazi wake karudi zake huko duniani kuendeleza hustling, kila kitu kilifanyika kwao hivyo asipokuambia ana mtoto ni miaka 100 hutojua, labda kwa wale 'eksipati' wasiyoshindwa na jambo, ni alijua kumficha hasa..!

Maisha mengine kabisa yakaendelea, miaka aliyoahidiwa imepita haoni hata dalili ya that guy kurudi, lakini tayari ako negative kuhusu wanaume,
Siku isiyo na jina ikafika, akapigiwa simu na that guy he is back, na atakuja mkoa aliopo kumuona na kumuelezea what real happened, and shits he had been through.! Lady akafurahi but with a mixed feelings.!!

Hivyo wakaonana wakaongea yote, ila binti hakujaribu hata kwa bahati mbaya kusema yeye tayari ni Mama kwa kidume flani hivii.! Na ukizingatia everything is fine, the guy amerudi kumfuta machozi na kaamua anataka kufanya this thing ikuwe official.!!

Ladies; ungekuwepo kwa hiyo position ungeendelea kuficha siri mpaka uingie ndani ya ndoa ama utasema mapema achague moja?
Gents; ungekuwa kwenye nafasi hiyo ungemuelewa mpenzi wako ukaendelea na mipango ama ndiyo itakuwa mwisho wa mahusiano yenu.?
 
Hakuna kitu kibaya sana kama kumkana mwanao Kisa tu upate NDOA...waweza ona ni jambo la kawaida lakini ktk Ulimwengu wa roho hali ni viceversa...

Kumbuka kweli humuweka MTU huru na siku mwenza wako akijua una Mtoto na ulimficha jua kabisa kuwa, "supu umelitia Nazi"

Binafsi ningekuwa kwenye nafasi ya jamaa basi huyo binti simhitaji TENA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amwambie ukwel, Na sijaona kosa la binti mahusiano ambayo hamna mawasiliano huwez kuita mahusiano...

Asema alivyopotea hewan ikabd aendlee na maisha yake kama mwanadam wa kawaida naye ana mahitaj yake ya kimwili.

Though hujasema sababu iliyomfanya jamaa apotee hewan kwa muda wote huo ina maana hata familia yake walikua hawawasiliani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ningemwambia tu ukweli km kuachwa acha niachwe tu, mm ni binadamu mtu alipotea kwa miaka kadhaa na wala hakukuwa na mawasiliano sasa mm Malaika kukaa tu kusubiri usichojua kinakuja lini!! Akiniacha itakuwa basi Mungu hakupanga na siwez kuforce.

Na nitaishi tu sabbu ht kipindi hakuwepo niliweza kuishi
 
Najua nipo nje ya mada lakini inakuwaje mnapotezana for years kwenye hii dunia iliyojaa teknolojia mitandao mingi ya kuwezesha mawasiliano kati ya mataifa, kuna fb, insta,whatsap, skype na mingine mingi tu ukishaenda uko nchi za wenzetu ndio mawasiliano yanapotea?
 
IMG-20200501-WA0022.jpg
 
Amwambie ukwel, Na sijaona kosa la binti mahusiano ambayo hamna mawasiliano huwez kuita mahusiano...

Asema alivyopotea hewan ikabd aendlee na maisha yake kama mwanadam wa kawaida naye ana mahitaj yake ya kimwili.

Though hujasema sababu iliyomfanya jamaa apotee hewan kwa muda wote huo ina maana hata familia yake walikua hawawasiliani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena kama nilivyotaka kunena 😎, so hilo swali ulouliza hapo mwisho akijibu nistue🙇‍♀️
 
Najua nipo nje ya mada lakini inakuwaje mnapotezana for years kwenye hii dunia iliyojaa teknolojia mitandao mingi ya kuwezesha mawasiliano kati ya mataifa, kuna fb, insta,whatsap, skype na mingine mingi tu ukishaenda uko nchi za wenzetu ndio mawasiliano yanapotea?


Hapo ndo imakataa kabisa kuingia akilini.

Labda hii story Ni ya 1998
 
Najua nipo nje ya mada lakini inakuwaje mnapotezana for years kwenye hii dunia iliyojaa teknolojia mitandao mingi ya kuwezesha mawasiliano kati ya mataifa, kuna fb, insta,whatsap, skype na mingine mingi tu ukishaenda uko nchi za wenzetu ndio mawasiliano yanapotea?
Asante mkuu na nilifikiria Hilo pia kwan alienda sayari nyingine fwala wt hao waendelee na maisha mechi imeanza moja moja mwanzo ilikuwa moja bila
 
Labda ni back to 70’s kwa miaka hii ni chai tupu kuna njia ya mails, social networks nyingi tu, labda kama huyo mwanaume aliamua kwa sababu zake mwenyewe kumpotezea mwenzie
Mistari ya mwisho nadhani ina majibu ya maswali yako, hivyo ndivyo nilivyoamini pia ila huwezi mshauri hivii mtu aliyependa akakuelewa, Cc; Chindy..!

Turudi kwenye mada.!
 
Write your reply...Write your reply...BINTI HANA KOSA JAMAA NDO MWENYE MAKOSA COMMUNICATION NI NGUZO MUHIMU KATIKA MAHUSIANO SASA YEYE KAPOTEA BILA TAARIFA BINTI WA WATU APOTEZE MDA WAKE AMSUBIRIE TUUH JE KAMA ANGEKUWA AMEKUFA AU KASHAOA


BINAFSI NINGEKUWA MIMI HUYO BINTI NINGEPIGA CHINI NIKAMTAFUTA MWENGINE NIKAOA
 
Wanawake/ Mabinti wanakua na wakati mgumu sana kwa vile wao hupenda kwa dhati, shida ni kwetu tusio na huruma. Licha ya kushindwa kuwapenda kwa dhati, hata ile kuthamini upendo wao tu ili usimpotezee muda inatushinda. Mfano mzuri ni huyo jamaa aliyemzalisha binti wa watu na kujitutumua kwenda kwa wazazi, utasema aliambiwa hawana uwezo wa kutunza mjukuu.

Mwingine ni huyo jamaa yake, unamtelekezaje mchumba/rafiki bila mawasiliano kwa kipindi kirefu namna hiyo?

Binti aseme ukweli tu japo kuna wakati sio kila ukweli inabidi usemwe.

Kwangu huyo binti ni mvumilivu na mwenye hofu, angeweza hata aitoe hiyo mimba lakini kakubali kuchukua fedheha na adha zote hadi kajifungua ( Na hapa ndio napingana na wale wanaowakejeli na kuwadharau wanaowaita Single Mother japo hili jina silipendi).

Ningekua ndio huyo jamaa ningemuoa tu tuendelee na mipango ya maisha. Tatizo kwa nnavyowafaham wanawake itamsumbua sana kujisamehe na ataishi akijiona mkosefu siku zote, atahitaji msaada wa kisaikolojia na upendo wa hali ya juu kumpa furaha na amani ya kweli.

Mwisho, majibu yangu na mengine yoote yatakayotolewa hapa ni nadharia tu.

Haya mambo magumu sana yakikupata kiuhalisia, unaweza kujikuta unafanya maamuzi ambayo haujawahi kuyafikiria wala kuwazia.

Ni kama tulivyovamiwa na Covid kila mtu anakuja na suluhu yake.
 
Back
Top Bottom