"Ungekuwa Mzuri ungekuwa Umeolewa" kauli hii Wanawake wanapenda kuambiana inaukweli kiasi gani?

"Ungekuwa Mzuri ungekuwa Umeolewa" kauli hii Wanawake wanapenda kuambiana inaukweli kiasi gani?

Hilo neno " uzuri" limebeba maana nyingi Sana katika huo muktadha wa wanawake kutukanana.

Kuna uzuri wa muonekano, uzuri wa tabia na akili.Mara nyingi hizi sifa zote huwa zinajumuishwa pamoja kwa kutumia neno " mzuri".
 
Wanawake wazuri wazuri wameolewa.
Yamebaki madunga embe yanahangaika
 
Uzuri wa Tabia, Nafsi na Roho ndo tatizo kubwa la wanawake wengi hasa wale wenye uzuri wa Maumbile na/au Akili.

Na kiukweli Mke mwema sio yule mwenye Tako kubwa wala mwenye GPA kali. So ieleweke tu uzuri unaohusishwa na kuolewa ni Uzuri wa Tabia, Nafsi na Roho maaana huu ndo unamfafanua mtu jinsi anavyoishi na jamii, familia na Mume.

Nirudie?
 
Kama ulivyosema wanaambianaga hivyo wakiwa katika hali ya kuchambana au kusutana kiufupi wakiwa kwwnye hali ya magomvi, ni ile ya akutukanae hakuchagulii tusi,

Kwa mujibu wa jamii zetu inaaminika kuolewa inaongeza heshima kwa mwanamke lakini kwa usawa tulionao ndoa haitoi uhakika wa kuishi kwa furaha wala kwenda mbinguni, kumdhihaki asie nayo ni kukosa kumakinika kwa muolewaji kwenye majukumu yake ya ndoa

Sio wanawake tu hata njemba zipo inazizomea pisi ambazo hazijaolewa sasa unajiuliza mtu km huyu anamtambia na kudhihaki mwanamke ni wivu au upunguani au nae ni mwanamke katika umbo la kiume
Fanya maarifa uolewe, huo mtazamo wako unapingana na uhalisia kwa sababu hauko sawa.
 
Back
Top Bottom