"Ungekuwa Mzuri ungekuwa Umeolewa" kauli hii Wanawake wanapenda kuambiana inaukweli kiasi gani?

Hilo neno " uzuri" limebeba maana nyingi Sana katika huo muktadha wa wanawake kutukanana.

Kuna uzuri wa muonekano, uzuri wa tabia na akili.Mara nyingi hizi sifa zote huwa zinajumuishwa pamoja kwa kutumia neno " mzuri".
 
Wanawake wazuri wazuri wameolewa.
Yamebaki madunga embe yanahangaika
 
Uzuri wa Tabia, Nafsi na Roho ndo tatizo kubwa la wanawake wengi hasa wale wenye uzuri wa Maumbile na/au Akili.

Na kiukweli Mke mwema sio yule mwenye Tako kubwa wala mwenye GPA kali. So ieleweke tu uzuri unaohusishwa na kuolewa ni Uzuri wa Tabia, Nafsi na Roho maaana huu ndo unamfafanua mtu jinsi anavyoishi na jamii, familia na Mume.

Nirudie?
 
Fanya maarifa uolewe, huo mtazamo wako unapingana na uhalisia kwa sababu hauko sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…