Unguja: Mke achoma moto gari ya mumewe baada ya kuoa mke wa 2

Unguja: Mke achoma moto gari ya mumewe baada ya kuoa mke wa 2

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja limeanza kufanya uchunguzi zaidi kuhusu tukio la Msimu Jaffari (33), kudaiwa kuchoma moto gari ya mumewe, ambaye wiki iliyopita alitoa taarifa ya kuongeza mke wa pili katika ndoa yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kesi hiyo imeripotiwa katika Kituo cha Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Kamanda Hassan alisema tukio hilo, limeripotiwa mwishoni mwa wiki huko Kitumba Wilaya ya Kati Unguja. Gari aina ya Spacio inayomilikiwa na Abdallah Hijji (43) ilitiwa moto usiku.

Mke wa kwanza wa mtu huyo, anatuhumiwa kufanya tukio hilo. Alisema taarifa za awali katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi, unaonesha kwamba Hijji alitoa taarifa kwa familia na mkewe wake wa kwanza, kwamba anakusudia kuongeza mke wa pili.

‘’Uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika hatua za awali unaonesha kwamba tukio hili linahusishwa na wivu wa kimapenzi, ambapo mume alimjulisha mkewe nia ya kuoa mke wa pili na kama unavyojua wanawake wengi hawapendi ukewenza. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na ukweli halisi wa tukio hilo,’’ alisema.

Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, kwa kuwahoji watu mbalimbali huko Kitumba, umeonesha kwamba Hijji aliongeza mke wa pili wiki iliyopita. Hatua hiyo ilimtia hasira mke wa kwanza, ambaye kabla ya ndoa hiyo alikuwa akitoa tahadhari kwa mumewe, kwamba asithubutu kuoa mke mwingine.

‘’Huyu mwanamke hataki ukewenza, kwa muda mrefu amekuwa akimuonya mumewe asijaribu kufanya kitu hicho na akifanya atajuta,’’alisema jirani ya Hijji, Haji Omar ambaye alidai amekuwa akishuhudia mara kwa mara ugomvi wa watu hao.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi utakapomalizika, jalada la kesi hiyo litapelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Chanzo: HabariLeo
 
Mkuu dini imeweka utaratibu wa kutoa taarifa. Kwa sababu bila taarifa hakuna zamu na kama hakuna zamu ni dhulma, lazima mke ajue unapolala

Dini haikuweka sharti kuwa aridhie.

Kuridhia na kutoa taarifa ni mambo mawili tofauti.

Hakuna mwanamke anaridhia kabisa uke wenza, ni jambo la wivu kwao.

Ndio maana dini haikuweka sharti la kuridhia wao mana tusingeoa kabisa.
Hivi siyo kwamba lazima mke wa kwanza aridhie kwanza ndipo mme unaongeza mke wa pili? Na kama ndivyo iweje jamaa aongeze mke bila kupata ridhaa ya mke mkubwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu ni kile kile tu ila uislamu ni dini ya uadilifu na maumbile.

Akichepuka huko akipata watoto hawatambuliki kisheria sasa hapo watoto wa kichepuko wamedhulumiwa.

Ila uislamu ukiwa na watoto wengi kwa wake wanne wote wanatambulika.

Kushare panauma. Bora mimi ni mkristo ndoa ni moja. Chepuka huko nje ila hauoi mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom