Unguja: Waziri Dkt. Stergomena afanya ziara kutatua migogoro ya ardhi kati ya jeshi na Wananchi

Unguja: Waziri Dkt. Stergomena afanya ziara kutatua migogoro ya ardhi kati ya jeshi na Wananchi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
LE2A6765_Easy-Resize.com.jpg

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amewatembelea na kuongea nao Wananchi wa maeneo ya Visiwa vya Unguja kuhusu namna watakavyoshirikiana katika kutatua migogoro ya ardhi baina yao na vikosi vya Jeshi.

Akiwa kisiwani humo, Stergomena alipata fursa ya kutembelea maeneo ya Unguja Ukuu, Kikungwi, Binguni, Ubago na Dunga yote ni kutoka Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Akiongea na wananchi wa maeneo hayo kwa nyakati tofauti, baada ya kusikiliza kero zao, Dkt Stergomena alibainisha wazi kuwa, Jeshi linahitaji maeneo makubwa ili liweze kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi. Hivyo basi, ni vyema wakashirikiana kwa karibu na Jeshi, kuheshimu mipaka pamoja nakuendelea kulinda maeneo ya Jeshi.

Aidha, katika kutimiza azima yake ya kutatua migogoro hii, Waziri amebaini kuwa maeneo haya yalikuwepo, lakini tatizo lililojitokeza ni kuwa maeneo haya yaliachwa bila usimamizi madhubuti hali iliyosababisha maeneo haya kuvamiwa.

Hivi karibuni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeendelea kuchukua hatua mbalimbali, katika kushughulikia suala hili na hatimaye kulimaliza kabisa, zikiwemo kupima maeneo yote yote ya Jeshi, kuyasajili kwenye Kamisheni ya Ardhi na kuyapatia hatimiliki. Hatua hizi zimefikia mahali pazuri.

Waziri amedhamiria kwa dhati kwa ushirikiano na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupima maeneo yote, kufanya tathmini pamoja na kulipa fidia, lengo ni kuhakikisha kuwa suala hili linapatiwa ufumbuzi wa kudumu bila kuathiri ustawi wa wananchi wa maeneo hayo.

Baada ya zoezi la upimaji na kufanya tathmini kukamilika, hatua inayofuata ni ulipaji fidia kwa walre wote wanaostahili kufidiwa. Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Waziri amewaomba wananchi hao kuwa na subira wakati suala hili likiemndelea kushughulikiwa na Serikali zote mbili.

Ziara yake hiyo, inafuatia maombi yaliyotolewa kwake na Waheshimiwa Wabunge wa maeneo hayo. Wabunge hao ni Khalifa Salum Seleman bunge wa Jimbo la Tunguu pamoja na Mwantumu Dau, Mbunge wa Viti Maalum kwenda jimboni humo kuangalia namna ya kutatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu.

Migogoro ya ardhi baina ya Jeshi na Wananchi imeanza tangu miaka 1990 kutokana na baadhi ya wananchi wasio wazalendo kuvamia maeneo ya Jeshi na kuanzisha shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ujenzi wa makazi, kilimo na ufugaji kinyume cha sheria.
 
Back
Top Bottom