JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa vita inayoendelea Nchini Ukraine imekuwa na madhara makubwa kwa watoto, ambapo wengi wao wanahitaji msaada wa kisaikolojia.
Watoto zaidi ya milioni moja wa Ukraine kwa muda wa miezi miwili wamekuwa katika mateso kutokana na makombora na mabomu ya mara kwa mara, kukosa chakula, kushindwa kwenda shule na kukos ahuduma muhimu.
UNICEF inasema hali hilo imesababisha majeraha makubwa kwa watotoreated a child protection crisis of extraordinary proportions.
Mashirika ya UN yameripoti kuwa kuna vifo vya raia wa kawaida 6,800 ambapo 3,300 kati yao waliuawa. Watu zaidi ya milioni 7 wamekimbia makazi yao ndani ya Ukraine na zaidi ya watu milioni 5 wamekimbia kuwa wakimbizi katika nchi Jirani, robo tatu wakiwa ni watoto.
Kabla ya Urusi kuanza kuivamia Ukraine, Februari 24, 2022 kulikuwa na watoto zaidi 90,000 walikuwa wakiishi katika taasisi, vituo vya yatima na taasisi nyingine mbalimbali nusu kati yao wakiwa ni walemavu.
Source: vioanews