Wakristo wenye akili wanalijua hilo, tatizo kuna watoto waliozaliwa 2000+, hao ndio huwaambii kitu wakakuelewa.
Sasa we mtu anaabudu sanamu, ataelewa hilo?
Mtu kila jumapili anauziwa papai kutoka kimanzichana, anaambiwa limetoka kwa bwana (mungu) atakuelewa kweli.
Mtu kanisani kwake kuna nabii wa kike kavaa kisuruali kimemmbana, tena usishangae yuko mwezini lakini kuna msomi wa phd anamuamini kua huyo ni nabii.
Kiufupi kuna kundi la wakristo feki limeibuka hapa kati ambalo akili zao na mbuzi hazitofautini.
Ni bora mkatoliki utamuambia kitu atakuelewa, lakini sio hayo makanisa mengine.
Kimsingi Wakristo wasio soma biblia, unabii(vitabu vyenye kufafanua unabii wa Daniel na Ufunuo) na historia na kuunganisha hivi vitu vitatu bado itakuwa ngumu kunga'mua mambo yanavyokwenda. Watabaki kusema Israel ni taifa teule ukiwabariki nawe utabarikiwa.
Wakristo hao hawajui kuwa Mungu hana ubaguzi na huwabariki wote Wamchao bila kujali utaifa wao. Na hukumu zake zi juu ya wasiomcha. Rejea kupigwa Israel na kupelekwa utumwani Babel(Iraq ya sasa)kwa miaka 70 baada ya kumuasi Mungu. Rejea pia utume wa nabii Yona kwenda Ninawi (Sehemu ya Iraq na Syria) kuhubiri na Mungu akawasamehe.
Mpango wa Mungu wa kutumia uzao wa Ibrahim ilikuwa ni kutimiza kutimiza lengo kuu la Kuzaliwa Kristo, kueneza injili na kuukomboa ulimwengu kutoka utumwa wa dhambi, ulikuwa si kuwapendelea wayahudi na kuwaumiza wanadamu wengine.
Na ndiyo maana Paulo katika Wakorintho anasema sisi tusio Waisrael wa Kuzaliwa tunafanyika Kuwa Wana wa ahadi(wa Ibrahim) kwa kumkiri Kristo, lakini pia si wayahudi/Waisrael wote wa Kuzaliwa watafanyika Wana wa ile ahadi (hii ni kwa sababu ya kutokumtambua na kumkana Yesu Kristo).
Yeye mwenyewe Kristo anawaambia kwenye Mathayo 21:43, kwa kosa la kumkataa Masihi ufalme (baraka ) zimeondolewa kwao (wayahudi) na kupewa wengine wenye kuzaa matunda. Na hata akatabiri juu ya kuanguka kwa Yerusalem na kuharibiwa kwa hekalu, tukio lililo kuja kutimia mwako 70A.D yapata miaka 37 tangu kifo cha Yesu na mateso ya wafuasi wa Kristo huko Uyahudi.
Kuanguka huko kwa Yerusalem ndiko kulikofanya wayahudi kutawanyika ulaya na kwingineko duniani na taifa lao kusambaratika hadi hapo walipokuja kurejea mwaka 1946-48 takribani miaka 2000 kwa msaada wa Uingereza na Marekani.
Sasa niwaulize tu Wakristo wenzangu huo upekee, uteule na kubarikiwa kwa Israel kuko wapi hadi tufikie kushabikia unyama na mauaji ya wapalestina, eti tu kwa tafsri hafifu ya maandiko katika kitabu cha mwanzo; pale Mungu alipokuwa akimuahidi Ibrahim kuwa atamfanya taifa kubwa, atambariki yeyote atakayembariki Ibrahim na uzao wake na kumlaani yeyote atakaye mlaani Ibrahim na uzao wake. Wakati huohuo tukishindwa kuelewa kuwa Yesu alikuja kuwaokoa wanadamu wote wakiwemo hao wapalestina na wala hana ubaguzi kwa Myunani, wala Myahudi, wala Mrumi (rejea
matendo sura ya tisa na kumi).