Vyuo vyote hivi vilivyojaa hapa Tanzania ama Duniani mtu ukapoteze muda wako UD kwa waalimu limbukeni na washamba?
Mimi ni vile tu sikua na uwezo, hata undergraduate nisingesoma Tanzania. Waalimu wengi wa vyuo Tanzania ni washamba, limbukeni, roho mbaya, mawazo mgando, fikra za kijinga na kizamani sana.
Wengi wamesoma master degree ulaya miezi 12 lakini wakija bongo wanakulazimisha usome miezi 18 na hiyo 18 utapata shida sio kidogo, mara nyingi ni zaidi ya miezi 24. Kuna mshikaji wangu alianza master degree hapo UD toka 2017 hajamaliza hadi leo, mara supervisor hayupo, mara miezi 3 hajajibu wala kusahihisha kazi ya mshikaji, mambo ya hovyo kabisa. Jamaa November hii anaenda kuanza master degree Nairobi upya.
Bora kusoma open university kuliko kua campus.
Vyuo vyetu bado vina waalimu wanaamini mitihani migumu ndio inakufanya uwe bora. Mwalimu anatangaza darasani eti mwaka huu nashika kadhaa, mwaka jana nilishika kadhaa, hao ni waalimu.
Mimi hakuna elimu nitasoma kwenye vyuo vya Tanzania tena hata kwa bunduki.