University of Dar es salaam: Mnavyowafanyia wanafunzi wa masters na PhD mnakiua chuo, badilikeni

Njaa mkuu,stress za maisha,unafikiri Kabudi aliposema JPM amemtoa "jalalani"alikosea?!Wanazuoni wetu wanaishi maisha magumu,kamshahara kaduchu,wanaishia kufuga kuku,kitimoto,Ili kusongesha maisha.
Hasira zao wanazimalizia kwa wanafunzi
Mishahara yao sio midogo. Hayati jpm aliwatoa kwasababu walikuwa wamejazana pale na hamna kabisa wanachokifanya.
 
Umeongea ukweli mtupu. Yani wanapenda sana kunyenyekewa na hawajali muda kabisaaa.
 
Mkuu wachana na huyu, uongo mwingi. Ukisoma andiko lake kila mahala ni uongo tu [emoji23]. Pamoja na kwamba ni kweli Udsm kuna tatizo, ila haya ya huyu ndugu hayana uhalisia. Kwanza hii inayoitwa Academic block pale Udsm sijui ni ipi? Lakini sijui ni wapi alikokutana na hawa waliompa haya aliyoandika hapa. Ni either hakwenda Udsm ama waliompa taarifa hawakuwa wanaudsm. Mzee amepiga master miaka ya 1990 tena nje ila hawezi kujua namna bora ya kumsaidia mtoto wake amalize shule kwa utaratibu sahihi.
Mwanao anafanya Masters.

Halafu ukafunga safari kwenda naye kuuliza tatizo ni nini ?

Huyo ni mtoto au kopo pa rubisi.

Anyway, mzazi ni mateka wa Mbowe aliyepata zero Ihungo kwahiyo hakuna matarajio ya mtoto kuwa wa maana sana.
 
Thumbs up lady!!! Wanafikiria mapesa tunayotoa kusomesha wanafunzi yameokotwa. Wengi wetu huwa tunajibana sana ili tuweze angalau kuwakomboa watoto wetu kielimu. Leo mlecturer mmoja huko alete ushuzi kwa kweli inakera sana.
 
Mkuu unam dhalilisha mwanao,Level Ya Masters hawez tatua matatzo yake ya academic, had wee uingilie sa atakua lin??
Mimi naona yupo sahihi, pengine ameingilia baada ya Mwanafunzi kufanya jitihada za kuyatatua na wakamkwamisha. Na siyo dhambi mzazi kwenda kuhoji kuhusu mwanae kukwamishwa na MaDr uchwara wa hapo UDSM
 
Mwanao ana raha sana, mpaka master bado unamfuatilia mambo yake,me mwisho kufuatiliwa na mzazi ni class 5.

Hoja yako ina mashiko. Asipokuwa makini mwanao ataliwa kisamvu
Kama wazazi wenu walikuwa hawawezi kuwatetea mkaonewa poleni. Si hivyo kwa kila mtu.
 
Nimesoma Open sijawahi kusumbuliwa nilikuwa natoka Mkoa. Namtumia kazi akitaka nije anapanga siku atayokuwepo ananielekeza narudi narekebisha Hadi siku natetea nikavuka. Alikuwa pia ananielekeza Hadi kwenye simu anakuponda kidogo lakini anakuelekeza hasa spidi anayoyoitaka yeye. Hakuna rushwa Ila ni lazima uwe mnyenyekevu maana ' Mtaka cha uvunguni'. Walimu wote wanatabia moja ukijifanya unajua ndio mwisho wako.
 
Mwanao anafanya Masters.

Halafu ukafunga safari kwenda naye kuuliza tatizo ni nini ?

Huyo ni mtoto au kopo pa rubisi.

Anyway, mzazi ni mateka wa Mbowe aliyepata zero Ihungo kwahiyo hakuna matarajio ya mtoto kuwa wa maana sana.
Nimependa ulivyomjibu. Huyo mtoto wake na mzazi mwenyewe hakuna kitu.
 
Nilijaribu kusoma post graduate program nikashindwa kabla ya kuanza. pale wamejaa watu wengi ambao hawana haraka kabisa na kazi wala mambo ya maisha.
Ukiangalia sana, tabia ile ya U mungu mtu iliyojengeka kwa muda mrefu sana sasa, ndio inasababisha udumavu wa wasomi maana wanakwenda kusoma madesa, halafu waende taratibu na walimu wao, ili wafanikiwe kumaliza masoma. Kuna yanayoendelea pale mpaka aibu.
 
Mwanao anafanya Masters.

Halafu ukafunga safari kwenda naye kuuliza tatizo ni nini ?

Huyo ni mtoto au kopo pa rubisi.

Anyway, mzazi ni mateka wa Mbowe aliyepata zero Ihungo kwahiyo hakuna matarajio ya mtoto kuwa na akili ya maana sana.
aisee we dada sidhani Kama una akili timamu, halafu wewe ni mtu mwenye chuki inaonyesha
 
Udsm kama hujasoma undergraduate pale,ukaenda for postgraduate ukiwa huzijui system zao,utapachukia.ila kwa sie tuliosoma undergraduate pale huwa tunapeta tu.
 
Mkuu unam dhalilisha mwanao,Level Ya Masters hawez tatua matatzo yake ya academic, had wee uingilie sa atakua lin??
Ili ni tatizo kubwa sana kwa wazazi na watoto wa sasa. Tunalea watoto ambao hata kujitegemea hawawezi. Ulaya wanalea watoto wanajifunza kujitegemea mapema sana. Ndio maana hata wajukuu wa malkia Elizabeth wote wamepita jeshini ili kuwa ngangari. Ukute huyo dent wa masters anafuliwa boxer na house girl. Mie mwanangu alijiunga form five hapo Bagamoyo tu, siku shule inafungwa ananiambia nimfuate nikamwambia kwani huko hamna daladala? Mpk leo wala hajawahi kurudia

Nikulipie ada, nikununulie vitabu, nguo na kukulea halafu nikufuate na shule so hapa duniani mie nimekuwa dereva wako
 
Yaani elimu ya Tanzania kwakweli ni ujinga mtupu najuta kabisa yaani kosa walilofanya wazazi wangu sitafanya kwa wanangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…