University of Dar es Salaam (UDSM) special Thread

Hostel first year chuo kitakupangia wewe utaenda kwenye notes board utacheki umepangiwa wapi na room no ngapi kama ni mabibo,main cumpos au hostel mpya pale mliman city.
Shukran mdau. Mabibo naskia ndio ipo mbali na chuo?
 
Ipo mbali kidogo ila kuna daladala za chuo nauli 400 au kama wewe ni bahili utakuwa unatembea aka shato pori. Uzuri wa mabibo huduma nyingi hasa za msosi zinapatikana tena kwa gharama nafuu mamantilie wamejazana huduma zinapatikana hadi saa sita usiku yaani pame changamka sio kama main campus.kwa kutembea ni ndani ya dkk 20 kwa usafiri dakk 7 kama hakuna foleni
 
Kutokea keepleft cha mlimani city hadi maeneo ya chuo ni kama umbali gani? Na je kati ya kukaa hosteli na kupanga kipi bora...?
 
Naomba nikujibu kwa uzoefu wangu, mwaka wa kwanza nilikaa hostel mabibo pale dah! niliona maisha sio poa kabisa ila mwaka pili nilipanga mambo yakawa safi sana.
 
Naomba uniambie changamoto zake kama hutojali.
Na wanawake sio tatizo pia?
 
Inategemea kama utakaa peke au na mwenzako ila changamoto kubwa ni pesa tu. Ukiwa na pesa utapanga mambo yako yawe sawa ila ukikosa na maisha ya mtaani noma japo inategemea unaishi vipi na majirani. Changamoto kubwa mkipanga wawili ni kupigana exile , mwenzako anaweza akaja na msichana wake akakaba hata wiki mbili kipindi hicho wewe unabangaiza kwa marafiki zako wengine kupata pa kulala.
 
Kutokea keepleft cha mlimani city hadi maeneo ya chuo ni kama umbali gani? Na je kati ya kukaa hosteli na kupanga kipi bora...?
Kutokea mliman city nikaribu sana huitaji usafiri wowote ni dakk chache uko chuoni

Kuhusu malazi mimi naona kukaa hostel kuna nafuu sana kwenye gharama ukilinganisha na kupanga maana umeme, maji, chumba, ulinzi wakutosha vyote nikama bure, discusion pia, kunamaeneo mengine sii rafiki kabisa kwa mwanafunzi kuishi.

Pia gharama za vyumba now ziko juu sana, pia unatakiwa uandae asset kama kitanda , godoro na vitu vingine vingi vya kutumia ambavyo kama ungekaa hostel ungevipata.

Pia ukiwa hostel usafi hasa wa mazingira kunawatu special wanafanya hadi chooni tofauti na ambavyo ukipanga huwa kunazamu za usafi, pia habari za kujipikia huwa kwangu naona kama usumbufu[emoji56] [emoji56] [emoji56]

Pia kunawatu wengi huwa wanasema kukaa hostel nikujilemaza na utoto mimi hilo napinga kozi kama wewe unataka kufanya ujasiliamali utafanya tu hatauwe wapi nakama huwezi huwezi tu, kunaambao wanapanga mwisho wa sikuu wanamaliza chuo bila hata nauli inabidi wauze asset walizo nazo kwa bei ya hasara wanarudi kijijini mikono mitupu soo fanya research uangalie njia gani iko poah kwa upande wako
 
Inategemea kama utakaa peke au na mwenzako ila changamoto kubwa ni pesa tu. Ukiwa na pesa utapanga mambo yako yawe sawa ila ukikosa na maisha ya mtaani noma japo inategemea unaishi vipi na majirani. Changamoto kubwa mkipanga wawili ni kupigana exile , mwenzako anaweza akaja na msichana wake akakaba hata wiki mbili kipindi hicho wewe unabangaiza kwa marafiki zako wengine kupata pa kulala.
Kwahiyo inawezekana kupanga mwenyewe hosteli? Au unazungumzia kupanga mtaani?
 
Asante joohs,
Vyumba vya hosteli mnakaa wangapi wangapi? Inawezekana kukaa mwenyewe?
 
Campus chumba mnakaa 2 plus kubebana mnakuwa 4. Kwa mabibo chumba ni cha watu 4 plus kubebana mnakuwa 8. (KUBEBANA ni kushare kitanda kimoja watu 2. MAISHA KUSAIDIANA NDUGU)
 
Campus ndio hizo alizofungua magufuli? Ziko umbali gani hadi udbs?
 
Naomba kuuliza hivi.
Ud ntasajiliwa nisipokuwa na cheti original cha form four? Original kimepotea. Nina soft copy pamoja na photocopy zake.
 
Yaani kwenye swala la cheti ndo usifanye mzaa narudia tena usifanye mzaa, hawakubali copy ya cheti chochote mimi wakati nafanya usajili nilisahau cheti cha kuzaliwa hosteli ila nilikuwa na copy yake ,vingine vyote nilikuwa navyo original na copy zake, kisa uvivu wa kurudi kukifata nikaenda kuwadanganya eti nimekisahau mkoani asee waliniambia wewe rudi tu huko ukakifate ndo ujekufanya usajili daa walejamaa wako serious zaidi ya unavyo fikiri
 
Naomba kuuliza hivi.
Ud ntasajiliwa nisipokuwa na cheti original cha form four? Original kimepotea. Nina soft copy pamoja na photocopy zake.
Lazma uwe nacho og lasivyo admission letter haupati msela wangu alkua hana cha four hakupata admission adi karbia na mwisho wa semester one ndo akapata cheti chake akaenda fata admission yake then akajisajili vizuri tu... Af kuusu hostel mi nmekaa hall 5 ***** pale jau maji adi uchote chini af omba usiwe na rum uko juu kabisa utapanda ngazi na ndoo zako adi usome nmbr ila mi nlizoea.. ila semista ya pili nilienda kupanga but changamoto za kupanga ni gharama za vitu tu ila ka mko wawili haina noma life linakua poa mambo ya kupigana exile ni nyie wawili mkubaliane maana kodi mmelipa wote.. af hostel za magu hauwezi kaa semista ya kwanza cause kuna waliolipia semista iliyopita ila hostel hazikufunguliwa so i think semester hii watafidiwa nyie wapya mtakaa mabibo na hostel za chuo ,,hostel za campus adi udbs sio mbali kutembea daika kumi tu.. ka unatokea mabibo unaambia daladala ikushushe utawala then daika mbili adi udbs ila kijana ukifika chuo fanya mchakato uhame iyo bba uingie bcom itayokufaa... Ka ukitaka kupanga nichek mwnyw natafuta mtu wa kupanga nae me niko second year... Natumain yote ushajibiwa
 
Yaani nakushauri anza mapema kukifatilia necta, kuna rafiki yangu alisahau cheti cha f4 kwenye gari asee mizunguko aliyo kutananayo sio ya nchi hii alizunguka huko necta, helsb, mpaka kuja kusajiliwa ilikuwa ishu pia bila kupata id huwezi sign boom hapo ndo kunashida sana ,na usipo sign la mara ya kwanza bodi haitumi tena fungu lako wana assume haupo chuoni sasa kufatilia mpaka ukapatiwa hiyo hela unaweza postponed mwaka
 
Jamani mwenye uelewa na kozi ya bachelor of science in physics,ina husu nin in general plz
 
Nashukuru sana mdau.
Usajili inakuwaga mwisho baada ya mda gani? Maana nikianza kufatilia saivi itanichukua zaidi ya mwezi kukipata nadhani.
Vyumba vizuri vya kupanga ni maeneo gani vinapatikana kwa bei nafuu?
Bba ina changamoto gani tofauti na bcom? Mbona wengine wanasema bba ndio inabeba hadi masomo ya bcom and acounts humo ndani yake? Nifafanulie kidogo hapo mdau.
 
Yaani nakushauri anza mapema kukifatilia necta, kuna rafiki yangu alisahau cheti cha f4 kwenye gari asee mizunguko aliyo kutananayo sio ya nchi hii alizunguka huko necta, helsb, mpaka kuja kusajiliwa ilikuwa ishu pia bila kupata id huwezi sign boom hapo ndo kunashida sana ,na usipo sign la mara ya kwanza bodi haitumi tena fungu lako wana assume haupo chuoni sasa kufatilia mpaka ukapatiwa hiyo hela unaweza postponed mwaka
Alichukua mda gani hadi kukipata cheti cha form four necta ?
 
Back
Top Bottom