Unpopular Opinion: Arsenal hatoshinda taji lolote msimu huu

Anajizima data tu... Arsenal hana mechi kwenye mashindano mengine hivyo ataweza kufocus zaidi kwenye Ligi. Man City hawezi kumfunga Arsenal mechi 2..... Yaani timu yake imepasuliwa halafu anaamini wengine hawatapasuka vibaya.
Nimeshakuambia, mwili mkubwa lakini akili zako ndogo, Europa ni mashindano ya Golf eeeh kiasi kwamba Arsenal hashiriki
 
Nilikuwa sijui kama Arsenal nayo huwa haipendwi kiasi hiki,niliamini man u na man city na liverpool ndo timu zisizopendwa na watu wengi kumbe hadi Arsenal

Kwenye timu tishio zilizobaki hyo Liverpool itoe sio tishio tena
 
Ili upate umaarufu ni lazima uiseme Arsenal. Hii unaonesha kuwa Arsenal ni tishio msimu huu

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Una kipaji kikubwa sana cha ujinga hongera kwa hilo

Kwahyo unavyoona Arsenal itasumbuliwa na hzo timu je huyo unaehisi atabeba hilo kombe yeye hatosumbuliwa na timu yoyote au sio.
 
Arsenal tuna mechi 2 tu ambazo zitakuwa ngumu kwetu ambazo tutacheza away Man City na Newcastle.

Zilizobaki zingine zote Ni vibonde wetu kuanzia kwa Chelsea, Liverpool,Man City( H)
 
Labda ueropa anaweza kumbwela ila epl anabeba tofauti ya point ni kubwa sana na sioni timu nyingine ya kumsumbua arsenal ukiachana na man city na man u ambae ashacheza nae game zote mbili.. chelsea na liver msimu huu hakuna kitu labda akimfata newcastle ndo anaweza kudondosha point maana the magpies msimu wa wamekua moto hao wanaobaki wote ze gunners anapiga
 
Arsenal tuna mechi 2 tu ambazo zitakuwa ngumu kwetu ambazo tutacheza away Man City na Newcastle.

Zilizobaki zingine zote Ni vibonde wetu kuanzia kwa Chelsea, Liverpool,Man City( H)
Safi, tukutane May
 
EPL umeanza kuangalia lini? Kuna mtu aliingoza point 15 na hakubeba ndoo
 
Nimekaa pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…