Tunataka kujua mfumuko wa views umetokea wapi, ili kuondoa utata.
YouTube imeifanya dunia hii ya utandawazi (Globalization), limekuwa kama ''eneo la kijiji kimoja kidogo /au mtaa wa pili'' kiasi habari zinasambaa kila pembe ya ''kijiji cha Dunia'' kwa kasi kubwa.
Diamond Platnumz pamoja na crew nzima chini ya menejimenti yao wamelitambua hilo na kuitumia fursa iliyoletwa na YouTube ktk ''kijiji cha dunia'' kufanya kila ubunifu kuhakikisha kila ''mwana-kijiji wa Kijiji cha Dunia'' wanapata kuona kazi zao.
Hata wakifanya kazi za ''kiafrika'' mfano wimbo ''Salome'' au "Salima" by Tanzanian artist Linex featuring Diamond Platnumz wamelenga dunia kuanzia miji ya Lagos Nigeria, Libreville Gabon, Abdijan Cote d'Ivoire, Brussels Belgium, Minnesota USA, Ontario Canada au iwe
Piga-Piga Club iliyoko ktk viunga vya Jiji la Tokyo, Japan n.k nyimbo hizo zinapigwa.
Mbinu kubwa naona hata majina yao (wasanii) yamekaa ki-Globalization, mfano Diamond Platnumz, Harmonize, Ray Vanny, Mkubwa
Fela, Sallam, Mavoko (ma-Vocal),
Babu Tale kwa kutaja kwa uchache ni majina ''friendly'' ktk mtandao. Wasanii wengi wanakuja na majina ya kisanii yanayowakwaza ''kimtandao'' hawako makini ktk uchaguzi.
Mfano ukiweka ''neno'' ''Diamond'' ktk ''search'' youtube, Rihanna wimbo wake Diamonds, Diamond Platnumz au Diamond are Forever n.k ''vinaibuka'' ktk search by default. Hiyo ni siri moja ya ''kujipanga kimkakati'' ktk hatua ya mwanzo tu ya kuingia anga za usanii siyo kwenda kichwa-kichwa.
Pili WCB wanaiona dunia ni ''kijiji'' hivyo hufanya juu chini kazi zao nyingi zinamlenga huyo ''mwanakijiji wa Dunia''. Wakati wasanii wengine Tanzania wao macho yao hawaoni Dunia kama kijiji wanaiona ni ''kubwa sana kuiteka'' hivyo mkazo wao ni kuwafurahisha ''wabongo'' bila kuilenga dunia. Ila Dully Sykes naona ameelewa somo la WCB wengine bado hawataki kujifunza.
Mfano Diamond anavyokikamata ''Kijiji Dunia'', kila unapozunguka ktk ''vichochoro vya Kijiji cha Dunia'' unakumbana wa watu lukuki pande zote ulimwenguni wana ''sample'' kazi zake Diamond Platnumz ktk video zao mfano hii hapa chini huko Poland au hata huko Colombia, Marekani ya Kusini ktk ''vilabu'' wanamjua SALOME youtube CLIP
''como bailan saida karoli tanzania'' (JESSENIA) :
Diamond Platnumz Ft Mr Flavour - Nana | Dance Class in Poland | By Sherrie Silver
Source: Sherrie Silver
N.B
Ngoja niishie hapa maana nikienda ndani itakuwa naweka wazi ''mkakati-kazi'' wa huyu Nguli wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz wa Tanzania , na biashara mambo yote huwezi ku-''share'' inabidi watu wamuangalie kwa makini Diamond pamoja na crew nzima ili wajifunze.
Dunia nzima inajiuliza huyu Diamond Platnumz ni nani maana anaibuka kila kona na hivyo ''kushinda'' YouTube kutafuta kazi zake na mwishowe ''mfumuko'' wa ''traffic'' YouTube kwa kutaka kuwa viewer wa kwanza ktk kila up-load mpya ya Baba T al-maaruf Simba a.k.a Dangote.
Source: M2i Tv Mayotte, Jimbo la 101 la Ufaransa (Comoro) Nov 26, 2016