Ununuaji wa views Youtube mambo hadharani

Ununuaji wa views Youtube mambo hadharani

Tunataka kujua mfumuko wa views umetokea wapi, ili kuondoa utata.

YouTube imeifanya dunia hii ya utandawazi (Globalization), limekuwa kama ''eneo la kijiji kimoja kidogo /au mtaa wa pili'' kiasi habari zinasambaa kila pembe ya ''kijiji cha Dunia'' kwa kasi kubwa.

Diamond Platnumz pamoja na crew nzima chini ya menejimenti yao wamelitambua hilo na kuitumia fursa iliyoletwa na YouTube ktk ''kijiji cha dunia'' kufanya kila ubunifu kuhakikisha kila ''mwana-kijiji wa Kijiji cha Dunia'' wanapata kuona kazi zao.

Hata wakifanya kazi za ''kiafrika'' mfano wimbo ''Salome'' au "Salima" by Tanzanian artist Linex featuring Diamond Platnumz wamelenga dunia kuanzia miji ya Lagos Nigeria, Libreville Gabon, Abdijan Cote d'Ivoire, Brussels Belgium, Minnesota USA, Ontario Canada au iwe Piga-Piga Club iliyoko ktk viunga vya Jiji la Tokyo, Japan n.k nyimbo hizo zinapigwa.

Mbinu kubwa naona hata majina yao (wasanii) yamekaa ki-Globalization, mfano Diamond Platnumz, Harmonize, Ray Vanny, Mkubwa Fela, Sallam, Mavoko (ma-Vocal), Babu Tale kwa kutaja kwa uchache ni majina ''friendly'' ktk mtandao. Wasanii wengi wanakuja na majina ya kisanii yanayowakwaza ''kimtandao'' hawako makini ktk uchaguzi.

Mfano ukiweka ''neno'' ''Diamond'' ktk ''search'' youtube, Rihanna wimbo wake Diamonds, Diamond Platnumz au Diamond are Forever n.k ''vinaibuka'' ktk search by default. Hiyo ni siri moja ya ''kujipanga kimkakati'' ktk hatua ya mwanzo tu ya kuingia anga za usanii siyo kwenda kichwa-kichwa.

Pili WCB wanaiona dunia ni ''kijiji'' hivyo hufanya juu chini kazi zao nyingi zinamlenga huyo ''mwanakijiji wa Dunia''. Wakati wasanii wengine Tanzania wao macho yao hawaoni Dunia kama kijiji wanaiona ni ''kubwa sana kuiteka'' hivyo mkazo wao ni kuwafurahisha ''wabongo'' bila kuilenga dunia. Ila Dully Sykes naona ameelewa somo la WCB wengine bado hawataki kujifunza.

Mfano Diamond anavyokikamata ''Kijiji Dunia'', kila unapozunguka ktk ''vichochoro vya Kijiji cha Dunia'' unakumbana wa watu lukuki pande zote ulimwenguni wana ''sample'' kazi zake Diamond Platnumz ktk video zao mfano hii hapa chini huko Poland au hata huko Colombia, Marekani ya Kusini ktk ''vilabu'' wanamjua SALOME youtube CLIP ''como bailan saida karoli tanzania'' (JESSENIA) :


Diamond Platnumz Ft Mr Flavour - Nana | Dance Class in Poland | By Sherrie Silver

Source: Sherrie Silver

N.B
Ngoja niishie hapa maana nikienda ndani itakuwa naweka wazi ''mkakati-kazi'' wa huyu Nguli wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz wa Tanzania , na biashara mambo yote huwezi ku-''share'' inabidi watu wamuangalie kwa makini Diamond pamoja na crew nzima ili wajifunze.
Dunia nzima inajiuliza huyu Diamond Platnumz ni nani maana anaibuka kila kona na hivyo ''kushinda'' YouTube kutafuta kazi zake na mwishowe ''mfumuko'' wa ''traffic'' YouTube kwa kutaka kuwa viewer wa kwanza ktk kila up-load mpya ya Baba T al-maaruf Simba a.k.a Dangote.


Source: M2i Tv Mayotte, Jimbo la 101 la Ufaransa (Comoro) Nov 26, 2016
 
Tunataka kujua mfumuko wa views umetokea wapi, ili kuondoa utata.
Ah! We jamaa acha mambo yako bhana!!! Unataka kufahamu mfumuko wa views umetoka wapi?! We nani bhana kakuambia kuna mfumuko wa views?Yaani Views 332,178 kwa siku 5 ndo unaona mfumuko??!!
 
Hizi akili zenu sijui zinafikiria nini?
Ngoja niwaache na ujinga wenu wa ki team, alafu mwambieni king wenu apeleke mziki wake nje ya kko, uyo anaenunua viewers sasa anaangalia soko la ulaya na america,
King anawaendesha sana. Hujamtaja msanii yoyote but King
 
Tunaweza bishana sana ila kiukweli haya mambo ya kununua views yapo sana na inawawia vigumu sana youtube kuzi detect, hata wakina rihanna, justin bieber walishtukiwa na views nyingi zisizo halali, kwa hiyo tukubali tukatae haya mambo yapo hata wewe leo hii unaweza kununua views kadri unavyotaka ni ela yako tu, mimi mpenzi wa nyimbo nzuri na sio shabiki wa ma-team kama utahisi hivyo, nakubali nyimbo za mond na za kiba pia, kwa hiyo sipo kuponda au kushabikia upande wowote, tunafahamishana tu.
Naona taabu tu ningekutafutia Report ya kiuchunguzi ambayo iliandaliwa na taasisi zaidi ya 5 huko duniani kuchunguza kampuni zinazotoa services kama Youtube kama vile YouTube wenyewe, Dailymotion, Vimeo n.k!!! Lengo la ile utafuta ni kufichua frauds mbalimbali including Fake Views!!

Kwanza niseme kwanza jambo moja... watu wanaposema Fake Views manake ni automated Views! Na wala hakuna atakayebisha kwamba hakuna Fake Views au Wajanja hawauzi Fake Views! Lakini nenda kwa yeyote yule ambae ni mtalaamu na atakuhakikishia, there's no way unaweza kununuaa malaki kwa malaki ya Fake Views halafu Google wasikushitukie... NO WAY! Kama una YouTube Channel unaweza kujaribu! Weka content yako, kisha enable monetized na baada ya hapo nununua Views 10,000 (am sure hawafiki hata $10)!!!! Baada ya hapo nenda kwenye channel yako... utawakuta hao views 10K! Usiangalie tena video yako kisha rudi baada ya siku 3 kama utawakuta!!!!

Halafu mnachoshindwa kujua ni kwamba, hao wanaodai kuuza Views ni wajanja janja wa kwenye mitandao! Yaani unaamini kabisa, Google na timu yake yote ile watashindwa ku-detect fake views kutoka kwa mtu ambae hata yeye mwenyewe channel yake haina millions of views lakini anataka kuaminisha watu kwamba anaweza ku-drive millions of views to your channel... yaani wewe utengeneze thousands of Dollars (incuding residual income) from Google Adsense lakini yeye apate $10 za mara moja; BASI!!!! Hivii hata hesabu za kawaida zinaingia hapo!!!
 
Ommy amefichua siri vijana wa mond mapovu yanawatoka.
Unachekessha ile mbaya... mi nakuona ki.laza tu katika hili manake mtu aliye smart anajua ni ujinga mtupu!!! Hapo ukiulizwa hata hao views wananunuliawaje nunuliwaje wala hujui...!
 
Unachekessha ile mbaya... mi nakuona ki.laza tu katika hili manake mtu aliye smart anajua ni ujinga mtupu!!! Hapo ukiulizwa hata hao views wananunuliawaje nunuliwaje wala hujui...!
Jamaa anijibu mwenyewe kha
 
Kwahiyo baada ya kuona hivyo inaonekana ndo kama ushaanza kuamini kwamba unaweza kununua malaki ya views halafu poa tu!!!!
Uwezekano huo unaweza kuwepo au usiwepo..
 
649ea7f6b3b91f3ee124a560e5d884ba.jpg


Watu wanaambiwa wanakataa haya Leo nataka msome wenyewe muamini kweli janja janja zinafanyika wcb

Views za youtube zinanunulika kabisa. Ningependa niwaoneshe mfano. WanaJF wenyewe mchague video niongezee views 5,000 za mfano.
 
Wakazi alipata Show ya big brother Africa Wale waandaaji waliona videos zake youtube alizofanya marekani.... So ukiwa na viewers wengi makampuni ni rahisi kukutumia kutokana na fanbase kubwa...[HASHTAG]#ujanjaujanja[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom