- Thread starter
- #101
Kunyakuliwa, kujikuta Mbinguni katika Roho katika Ulimwengu wa Roho ni kawaida, nami imewahi nitokea,Vipi kama nikikwambia tayari walisha nyakuliwa, unafikri ukinyakuliwa na huku Duniani unapotea.
Yaania ananyakuliwa anakuwa yupo mbinguni tayari ila hata duniani anaonekana kama kawaida tu.
Angalia mfano wa mtu huyu aliyenyakuliwa,
2 Kor 12:1-4 SUV
[1] Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. [2] Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. [3] Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); [4] ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
Hapo ni Paul anajizungumza yeye mwenyewe, Hebu jiulize baada ya Paulo kunyakuliwa unadhani alitoweka huku Duniani?
Hata hakutoweka bali aliendelea kuwepo tu.
Kunyakuliwa ni Kuingia ndani ya Yesu, hakuna unyakuo physically utakaokutoa Duniani kukupeleka kule juu mawinguni.
Mbinguni siyo Geographical Area, Mbinguni ni katika Roho. Hata sasa upo Mbinguni ndani ya Yesu.
Lakini pia Unyakuo katika uhalisia wa watu kubadilika miili kumlaki YESU IPO kimaandiko,
Sasa kuamini neno la Unyakuo alioeleza Paulo, Kisha usiamini neno alilosema Yesu mwenyewe kwamba watu watanyakuliwa Hilo sasa ni tatizo lako binafsi.