Ama kweli mambo yanabadilika,St. Mathew leo ndo imefikia hatua hii😂😂😂🙌🙌. Miaka ile darasa langu la form four tuliofanya mtihani wa taifa tulikuwa 406,hiyo ni kidato kimoja tu,walimu walikuwa wakijituma sana,walikuwa wakipewa motisha ya safari za nje,magari na pesa taslim kutoka kwa mmiliki wa shule,sikuwahi kusikia lawama za hivi. Hakikia imenivunjavunja moyo.
Kwenye mambo haya inajihidhirisha makosa ambayo wazazi wengi wanayafanya,unakuwa na mali na vitega uchumi lakini huwaandai warithi wako katika kuzisimamia mali na vitega uchumi vyao,mzee Mtembei nilisikia alikuwa akiumwa,akapelekwa India mara kadhaa sifahamu hali yake kwa sasa ila chini ya usimamizi wake ilikuwa vyema. Baada ya kuumwa NASIKIA aliweka watoto na mke wasimamie na kasheshe zikaanzia hapo na sasa ni wazi wameshindwa kabisa au wanaiharibu kabisa.