Unyanyasaji wa kibinaadamu hasa kwa wezi siyo mzuri

Unyanyasaji wa kibinaadamu hasa kwa wezi siyo mzuri

Na uzuri hao wezi wanapokwenda kuiba wanakuwa wamejiandaa kuiba, kuua na hata kuuawa. Hivyo ni sahihi kupata kimojawapo ya kile walichokitegemea.
Huyo itakua hajawahi kuibiwa.

Kuna binti wa chuo aliuliwa na vibaka kisa tu alikua anapambana nao wasichukue vitu vyake asubuhi mtoto wa watu anaenda chuo.
Wakaona wamchome kisu ili asiwasumbue waibe hiyo simu binti akafariki hapo hapo, sasa hao viumbe gani wasio na utu.
 
Katoe ushahidi uone!!

Wanaogoma kwenda kutoa ushahidi sio wajinga. Ndio maana "wananchi wenye hasira kali" huwa wanamalizana nao. Polisi wenyewe mkiwaita wakaja wakakuta bado hamjawashughulikia wanawashangaa.
Unaunga mkono mauaji?
 
Umewahi kuibiwa?
Naona watu wengi hata hawajaelewa mada yangu! Nazungumzia vitendo alivyofanyiwa huyo mwizi kuwa sio vitendo vya kibinaadamu kabisa na tuvikemee visiwe vinahalalisha uovu zaidi kwenye jamii.
 
Nazungumzia hayo mateso waliyompa na sitayari wamemkamata? Kwanini wakoroge.cement wamnyweshe? Kwanini wamfunge mikono wamwagie petrol na kumchoma sio haki kabisa! Acha kutetea unyanyasaji wa kibinaadamu.
Siku wakikuvamia wakufinye vizuri na wachukue Mali zako kibabe ndio utajua ni Kwa nini hatunaga huruma na mwizi
 
Siku wakikuvamia wakufinye vizuri na wachukue Mali zako kibabe ndio utajua ni Kwa nini hatunaga huruma na mwizi
Ukimkamata mwizi mfikishe kwenye vyombo vya sheria achukuliwe hatua nasio kuchukua sheria mkononi za kumuua hapo tunatengeneza au tunabomoa!
 
Kuna mzee mmoja hivi ni katibu tarafa wa sehemu fulani, aliwapa ruhusa vijana(kimya kimya) wa tarafa yake kuwa wakikamata mwizi au wezi wawaue tu.
 
Aaaah!! Mie walipita na vyao mara mbili nakuta kastore kangu kapo empty. Since then nilibadili mtazamo. Acha wenye hasira kali wapite nao.
Vitu vyangu vya thamani havifikii thamani ya uhai.
Tena hao wanaoiba vitu vidogo ni shida tu zinawasumbua.
Nimeibiwa sana tena mmoja walitaka kumuua mbele zangu...niliwaambia wampige na kumwacha.
Niliwazuia kuua
 
Huyo itakua hajawahi kuibiwa.

Kuna binti wa chuo aliuliwa na vibaka kisa tu alikua anapambana nao wasichukue vitu vyake asubuhi mtoto wa watu anaenda chuo.
Wakaona wamchome kisu ili asiwasumbue waibe hiyo simu binti akafariki hapo hapo, sasa hao viumbe gani wasio na utu.
Lenie kwahyo vyombe vyote vya dola vipo kama polisi na mahakama lakini kwenda huko hutaki is it fair kweli?
 
Vitu vyangu vya thamani havifikii thamani ya uhai.
Tena hao wanaoiba vitu vidogo ni shida tu zinawasumbua.
Nimeibiwa sana tena mmoja walitaka kumuua mbele zangu...niliwaambia wampige na kumwacha.
Niliwazuia kuua
Watajua wenyewe bwana, acha liwakute lolote maana ndiyo maisha waliyochagua.
 
Huwa wanapelekwa mahakamani na hapo watu wengi hawaendi kutoa ushahidi ndio maana wanaachiwa Futuza unadhani ukienda kutoa ushahidi mahakamani, lazima ale mvua hata miaka 3 na itakuwa fundisho.
Nina mfano hai mwizi kavunja mlango kamjeruhi dada wa watu kaiba simu na fedha kakamatwa kapelekwa polisi haikupita hata masaa ma3 yupo mtaani tena anaongea mbovu hatari

Niambie siku akikamatwa Tena wanachukua hatua gani
 
Back
Top Bottom