Unyanyasaji wa Polisi; Umewahi kupigwa, kuteswa, kudhulumiwa, kukomolewa au kubambikiwa kesi bila kosa? Weka mkasa wako hapa

Mwaka 2018 nilikamatwa na polisi Iringa mwaka bila sababu yoyote na bila kuambiwa kosa ninalokamatwa nalo ingawa baade walikuja kunibambikia kosa la matumizi mabaya ya barabara na kulazimisha ndugu zangu walipe faini ya elfu 30. Askari walionikama ni F.5117 PC Pastor Kuambiana, PC Fadhil na G.2729 ex-PC Steven Mchomvu (huyu ndio yule aliyekamatwa Januari 2022 akikusanya elfu 2 na elfu 5 za madereva pale check point Iringa, Jeshi la Polisi walimfukuza kazi)

Askari hao walinifanyia uharibifu wa gari, wakanifunga pingu, wakanidhalilisha na nikawekwa lock up kwa zaidi ya masaa 3. Wakati wananikamata nilikuwa na mke wangu, na rafiki yangu akiwa na mkewe. Nilifanikiwa kurekodi video ya tukio hilo, hata hivyo polisi walitaka nifute video hiyo kama sharti la kutoka lock up. Ndugu zangu waliifuta na kumbe Android 9 ilikuwa ina feature ya kuwa na DUST BIN ambako mafaili yaliyofutwa yanahifadhiwa huko kwa siku 30, nikafanikiwa kuirecover. Unaweza kuitazama hapa

Kwa kushirikiana na Manispaa ya Iringa, gari hilo lilishikiliwa kwa zaidi ya miezi 2 kwa maelezo kuwa nilipe Tshs. 840,000/= kama faini ya kuharibu mali za manispaa. Sikulipa faini hiyo na gari lilikuja achiwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa.

Picha ya kuonewa na hawa wasimamizi wa sheria na usalama wa Raia, bado ipo kichwani mwangu, walininyanyasa na kunikosea sana. Mwaka 2019 Nilifungua kesi ya madai kwa uonezi wao, kesi ambayo licha ya danadana nyingi imesikilizwa mwaka huu na hukumu itatolewa tarehe 11.11.2022 katika Mahakama Kuu ya Iringa mbele ya Mheshimiwa Jaji Kalunde. Nitashea hukumu hiyo humu pindi ikitoka.

Pichani ni Pc. Steven, mmoja wa maaskari walionikamata
 
Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    86.3 KB · Views: 5
  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    72.9 KB · Views: 5
Kwa bahati mbaya sana, wakitoka nje ya lile geti pale karibu na chuo cha ushirika barabara ya kwenda kcmc wanakuwa kama wamelishwa madawa ya wendawazimu
 
Mwaka 2018 nilikamatwa na polisi Iringa mwaka bila sababu yoyote na bila kuambiwa kosa ninalokamatwa nalo ingawa baade walikuja kunibambikia kosa la matumizi mabaya ya barabara na kulazimisha ndugu zangu walipe faini ya elfu 30. Askari walionikama ni F.5117 PC Pastor Kuambiana, PC Fadhil na G.2729 ex-PC Steven Mchomvu (huyu ndio yule aliyekamatwa Januari 2022 akikusanya elfu 2 na elfu 5 za madereva pale check point Iringa, Jeshi la Polisi walimfukuza kazi)

Askari hao walinifanyia uharibifu wa gari, wakanifunga pingu, wakanidhalilisha na nikawekwa lock up kwa zaidi ya masaa 3. Wakati wananikamata nilikuwa na mke wangu, na rafiki yangu akiwa na mkewe. Nilifanikiwa kurekodi video ya tukio hilo, hata hivyo polisi walitaka nifute video hiyo kama sharti la kutoka lock up. Ndugu zangu waliifuta na kumbe Android 9 ilikuwa ina feature ya kuwa na DUST BIN ambako mafaili yaliyofutwa yanahifadhiwa huko kwa siku 30, nikafanikiwa kuirecover. Unaweza kuitazama hapa

Kwa kushirikiana na Manispaa ya Iringa, gari hilo lilishikiliwa kwa zaidi ya miezi 2 kwa maelezo kuwa nilipe Tshs. 840,000/= kama faini ya kuharibu mali za manispaa. Sikulipa faini hiyo na gari lilikuja achiwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa.

Picha ya kuonewa na hawa wasimamizi wa sheria na usalama wa Raia, bado ipo kichwani mwangu, walininyanyasa na kunikosea sana. Mwaka 2019 Nilifungua kesi ya madai kwa uonezi wao, kesi ambayo licha ya danadana nyingi imesikilizwa mwaka huu na hukumu itatolewa tarehe 11.11.2022 katika Mahakama Kuu ya Iringa mbele ya Mheshimiwa Jaji Kalunde. Nitashea hukumu hiyo humu pindi ikitoka.

Pichani ni Pc. Steven, mmoja wa maaskari walionikamata
Mkuu ikikupendeza utashea hapa hapa kwenye huu uzi.
 
Wengi wao huwa ni mafukara tu wanategemea hongo zetu
 
Back
Top Bottom